Thursday, October 26, 2017

HIZI NDIO NJIA TISA ZA KUFANIKIWA KWENYE MAZOEZI YA KUJAZA MIILI KWA WANAUME..


wanaume wengi wa umri wa miaka 18 mpaka 40 hupendelea sana kufanya mazoezi ya kubeba vyuma au kupiga push ups ili kua na miili mikakamavu, nguvu, kupunguza uzito na kua na miili inayovutia wenyewe wanaita SEXY BODY. sasa katika harakati zakupata miili hiyo kuna makosa mengi hua wanayafanya na wengine hushindwa kupata miili hiyo na kukata tamaa kabisa. lakini kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia ukiamua kufanya mazoezi hao na kufanikiwa. 
kua na malengo; mara nyingi watu wanaenda gym bila malengo yeyote, yaani hajui anaka aweje ndani ya muda gani hii huwafanya kupoteza uelekeo baada ya wiki moja tu ya kuanza mazoezi. jipangie kwamba nataka kua na kifua kipana au mikono iliyojaa au kukata tumbo ndani ya muda fulani na hakikisha muda ulioweka haya mambo yanawezekana.. kama unaenda gym ili ufanikiwe kwa muda wa wiki moja ujue unapoteza muda. 
chagua kifaa na uzito sahihi;kutumia vifaa vya gharama sana au kwenda gym ya gharama kubwa sana haitakufanya upate mwili haraka ili uchaguzi mzuri wa mazoezi na vifaa. hakikisha uzito uliochagua basi unaweza kupiga mara 15 kwa raundi moja, kama unabebea chuma afu unapiga tano unashindwa basi hiyo sio size yako. 
usifanye peke yako; ukianza gym hakikisha kuna mwalimu au mtu mzoefu ambaye atakua anakuelekeza uanzie wapi halafu uishie wapi..kuanza kufanya mazoezi mwenyewe utakua unayafanya vibaya. yaani kushika chuma vibaya, kufanya mazoezi vibaya na kukaa vibaya kwenye zoezi fulani. lakini pia mazoezi ya wengi huleta hamasa ya kuendelea kuliko kufanya peke yako nyumbani. 
polepole ndio mwendo; mazoezi yote duniani yanafanyika kwa mwindo mkali kupata mafaniko lakini kwenye kubeba chuma ni tofauti kidogo kwani unatakiwa ufanye taratibu yaani kupandisha na kushusha sio haraka kama wanavyofanya wengi na kama umefanya utafiti utagundua ukifanya taratibu maumivu ndio yanakua makali zaidi na hiyo ni dalili nzuri. 
pumzika: hakikisha unapata pumziko la angalau dakika tatu au nne pale unapohama kutoka kwenye zoezi moja kwenda lingine yaani kutoka kwenye zoezi la mkono kwenda kwenye kifua kwani utafiti unonyesha mapumziko yake ni muhimu sana kwa mafanikio.lakini mapumziko sio hayo tu ni vizuri kwenga gym angalau siku tano mfulululizo kwa wiki wanaoanza na kupumzika siku mbili kwa wiki.mapumziko yale yataleta faida kuliko kwenda kila siku. 
kua na mpangilio mzuri wa mazoezi; ukienda gym afu ukatumia mashine zote kuna uwezeano mkubwa uko unapoteza muda.weka ratiba kwamba leo nafanya zoezi la mkono. fanya mazoezi yote ya kujaza mkono yanayopatikana pale afu mwishoni ndo unaweza kugusa kifua kidogo na tumbo kidogo. siku ya tumbo fanya mazoezi yote ya tumbo afu mwishoni ndio gusa kidogo na mengine. ukiyafanya yote kwa mpigo kwa kiwango kimoja, matokeo hautayaona.
chakula; umeshaona watu wanabeba chuma kila siku ila bado wana vitambi? au mtu ana bidii sana kwenye mazoezi lakini mafanikio hayaonekani? chakula ndio msingi wa kila kitu kwani mwili ule unaouona kwa baunsa ni chakula kitupu na ukimnyima hicho chakula kwa wiki moja tu utamshangaa atakavyoisha.vyakula vinavyojaza mwili yaani nyama na mifupa ni aina ya protini kama nyama, samaki,dagaa, karanga, korosho, maziwa na kadhalika lakini ukifanya mazoezi haya huku unakula sana ugali,wali,ndizi,mihogo,viazi na kadhalika utaambulia kitambi tu.sijasema usivile hivo ila kula kidogo.
                                                           


virutubisho; kuna virutubisho vinauzwa kitaalamu wanaita protein shake, mchnganyiko huo unakua na protein nyingi sana kuliko ile inayopatikana kwenye chakula cha kawaida na mara nyingi hua kwa mfumo wa unga, hivyo mtumiaji huchota unga ule na kuchanganya kwenye maziwa. matokeo yake hua ni mazuri sana sana.unaweza kuwasiliana na sisi ukihitaji virutubisho hivi.

                                                                    
usikate tamaa; hii ni point ya mwisho na ya msingi sana, kiufupi ukikata tamaa kwenye kitu chochote ndoto zako zimekua zimeishia hapo,  mafanikio yeyote huletetwa na uvumilivu mkubwa wa muda mrefu ambao mwisho wake utakuletea majibu.