Monday, October 30, 2017

HIZI NDIO NJIA PEKEE ZA MWANAUME KUJUA KAMA MTOTO ANAYEMLEA NI WA KWAKE KWELI.


utafiti uliofanyika na mahakama ya harare huko zimbambwe umegundua kua asilimia 72% ya wanaume walioenda kuhakikisha uhalali wa watoto wao waligundua sio wa kwao. wengi wa wanaume hao walikua wameshawalea watoto hao kwa muda mrefu sana na watoto wengine wakiwa watu wazima. hali hiyo imezua hofu kubwa kwa wanaume wengine ambao hawajapima kwa kuhofia majibu.
vipimo hivi vimevunja ndoa nyingi sana duniani, na mimi nasapoti kuvunjika kwa ndoa hizo kwani sio halali mwanaume  atokwe jasho kulea damu ambayo sio ya kwake bila kujua.

hali hiyo sio huko tu, hata hapa nchini kwetu kuna watu wengi ambao wanalea familia kubwa bila kujua wanalea watoto wa watu wengine na sio wanaume tu kuna wanawake wengi ambao wamebeba mimba wakiwa kwenye mahusiano ya zaidi ya watu wawili. hali hii hufanya wao kushindwa kujua baba mzazi ni nani hivyo huamua kusingizia mmoja wao ili mtoto apate matunzo.

nchi kama marekani, china, spain na israel baba anaruhusiwa kuwapima watoto wake bila kumuhusisha mama husika ila kuna nchi kama ujeremani kipimo hicho hupimwa kwa amri ya mahakama kwenye kesi husika. vipimo vifuatavyo hutumika kujua ukweli.

kipimo cha dna; kipimo hiki ni kipimo bora kuliko vipimo vyote yaani hakidanganyi hata kidogo, kwa sasa hupimwa kwa kuchukua mate kwa ndani ya mashavu kwa pamba maalumu. mate ya mtoto na mate ya mzazi hupelekwa maabara maalumu kwa ajili ya vipimo. matokeo huweza kutoka ndani ya siku mbili mpaka sita. matokeo hua ni aina mbili yaani asilimia sifuri 0% kama mtoto sio wako na  99.9% kama mtoto ni wako. kipimo hichi hapa nchini tanzania kinapatikana hospitali chache sana na kwa gharama kubwa hivyo ni ngumu kukipata kwa sababu ya gharama yake na hupimwa kwa amri ya mahakama. nchi zilizoendelea kipimo hiki hupatikana kirahisi sana yaani unakusanya mate wewe mwenyewe ukiwa nyumbani kwenye bahasha maalumu kisha unatuma posta na kuletewa majibu ndani ya siku mbili.

kipimo cha group za damu; kipimo hiki pia hutumika kujua uhalali wa wazazi husika hasa kwa nchi masikini sana kama zetu za africa ambazo ni ngumu sana na gharama sana kupata vipimo vya dna. kwa mfumo wa abo system kipimo hiki kinaangalia aina ya damu ambayo mama anayo, baba anayo na kuangalia kama mtoto ni wa kwao. yaani kwa maana nyingine kuna wazazi wa group fulani hawawezi kuwazaa watoto wenye group fulani kama ifuatavyo.

wazazi wenye group A kila mmoja wanaweza kuzaa watoto wenye group A na O na hawawezi kuzaa watoto wenye group B na AB
mzazi mwenye group A na mzazi mwingine group B wanaweza kuzaa magroup yote.
mzazi mwenye group A na mzazi mwingine group AB wanaweza kuzaa watoto wenye group A,B na AB lakini hawezi kumzaa group O.
mzazi mwenye group a na mzazi mwingine group o huweza kuzaa group a na o lakini hawawezi kuzaa group B na AB.
mzazi mwenye group B na mzazi mwingine mwenye group B huzaa group B na O na hawawezi kuzaa A na AB.
mzazi mwenye group B na mzazi mwenye group AB huzaa group A, B, na AB ila hawawezi kuzaa group O.
mzazi mwenye group AB na mzazi mwingine mwenye AB huzaa group A, B na AB ila hawezi kuzaa group O.
mzazi mwenye group AB na na mzazi mwingine na group O huweza kuzaa group A na B ila hawawezi kuzaa group AB na 0.
wazazi wenye group O wote huzaa watoto wenye group O tu na hawawezi kuzaa watoto wenye group A,B, na AB.
kipimo hiki kinapatikana nchi nzima hata kwenye maabara ndogondogo nchini tanzania kwa bei ndogo sana.

mwisho: kuna baadhi ya magonjwa yanaathiri mfumo wa binadamu[genetic diseases] yanaweza kusababisha watu wa group fulani kuzaa mtoto mwenye group ambalo si kawaida lakini ni mara chache sana, lakini pia kupima group la damu  vibaya kunaweza kuleta majibu ambayo sio ya kweli hivyo nashauri ukiona umepima ukakuta uko tofauti na mtoto ni vizuri kurudia vipimo tena au kwenda hospitali kubwa kuhakikisha na dna na pia wakati mwingine mtoto anaweza asiwe wako ila mkaonekana group ziko sawa kwasababu mwanaume aliyetembea na mke wako unafanana naye group za damu. hivyo dna ni ya uhakika zaidi na haina longolongo.