Saturday, October 28, 2017

HIZI NDIO NJIA KUMI BORA ZA KUPATA SIX PACKS ZA TUMBONI

wanaume wengi na wananawake wachache hutamani kupata six packs tumboni katika kipindi fulani cha maisha yao lakini sio rahisi kupata six packs kwani inahitaji nidhamu ya hali ya juu. maana kwamba ukizipata leo sio rahisi na kuzitunza. lakini pia swala la six packs sio mazoezi tu ila kuna mambo mengine ambayo unatakiwa kuzingatia ambayo wafanya mazoezi wengi hawafahamu na hawajui. kitaalamu misuli ya six packs inaitwa rectus abnominis ambayo hukaa chini ya mafuta ya tumbo hivyo ili kupata six packs lazima mafuta hayo uhakikishe unayaondoa kwanza..sasa leo ntaenda kuzungumzia njia hizo muhimu.

kula vizuri; neno kula vizuri ni pana sana yaani linahusisha ulaji wa chakula angalau mara nne mpaka tano kwa siku kwa kaisi kidogo na sio kula milo mizito mitatu kama ilivyozoeleka ili kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta[metabolism].pia  kula vyakula jamii ya protini amabavyo hujenga misuli mfano nyama, samaki, mayai, maziwa, karanga, dagaa na etc na sio kula wanga mwingi ambao kimsingi huleta mafuta mwilini kama ugali, viazi, mihogo, wali, maandazi, chapati, keki na jamii zote za vyakula hivi.sio kwamba usile kabisa wanga ila kula kwa kiasi kidogo sana.sahani hapo chini ni mfano wa kiasi cha kula kwa sahani moja yaani mboga na matunda mengi na wali au ugali kidogo.


                                                              
kunywa maji mengi; angalau lita tatu kwa siku kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta na kuondoa sumu nyingi mwilini.lakini pia kunywa maji hayo kabla ya kula mlo wowote angalau nusu lita au lita kabla ya kula ili kujaza tumbo kwanza ili usishawishike kula chakula kingi.

                                                                  
pata usingizi wa kutosha; tafiti zinaonyesha watu wanaolala muda mfupi sana husumbua mfumo wao wa homoni kufanya kazi na matokeo yake watu hawa hujikuta wanakula sana kuliko kawaida na hii huongeza mafuta na kitambi.
                                                            

epuka msongo wa mawazo; katika maisha ya kawaida msongo wa mawazo ni kawaida lakini kuna njia mbalimbali za kupambana na msongo wa mawazo hasa kwa kutatua chanzo husika cha msongo huo. kwani msongo wa mawazo huwafanya watu wengine wale sana japokua kuna wengine hula kidogo sana wakiwa na msongo wa mawazo.
                                                                    

fanya mazoezi; ni muhimu kufanya mazoezi ili kuondoa mafuta na kuikaza misuli ya tumbo..mtu anaweza kutoa kitambi kwa kujinyima kula lakini hawezi kupati six packs kwani zinahitaji kukazwa na na mazoezi.unatakiwa kufanya ya ujumla kama kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea na kuruka kamba pia mazoezi ya maalumu ya tumbo kama roller na sit ups..kwenda gym ni vizuri zaidi kwani utapata moyo ukifanya mazoezi na watu wengine tofauti na kufanya peke yako.
                                              

        
beba chuma au push ups; watu wanaofanya mazoezi haya huwa na misuli mingi ambayo inaongeza kasi ya kuchoma mafuta mwilini kuliko watu wanene wenye mafuta mengi ambapo kasi yao ya kuchoma mafuta hua ni ndogo.
                                                              

usinywe pombe; unywaji wa pombe hupunguza sana kasi ya uchomaji wa mafuta ya mwili ndio maana ukiwachunguza wanywaji wa pombe sana hua hawakosi vitambi kwani hata wakila chakula kidogo mwili unakibakiza na kukifanya mafuta.
                                                                  

  
usinywe soda; soda moja ina kama vijiko 10 vya sukari, kiasi ambacho ni kikubwa sana kwa matumizi a kawaida ya binadamu. sukari hiyo hubadilishwa kua mafuta na kuongeza uzito mwingine na kitambi. jaribu kutumia juice za kutengenezwa kwa mikono na hakikisha sukari yake ni ya kawaida kwani hata juisi za viwandani zina sukari nyingi sana.
                                                                

kula mboga za majani na matunda kwa wingi; hizi zina kiasi kidogo sana cha mafuta kiasi kwamba hata zikiliwa kwa kiasi kikubwa hua hazina shida, lakini pia zinasafisha sumu mwilini na na kuongeza kasi ya mmeng'enyo wa chakula huku zikizuia kupata choo ngumu.
                                        

tumia virutubisho vya kujenga misuli; kuna virutubisho mbalimbali kitaalamu kama protein shakes ambavyo vimetengenezwa maalumu kwa kazi hii huaidia sana kujenga misuli ya tumboni na sehemu zingine za mwili kwa ujumla, huufanya mwili uwe na umbo zuri na kusaidia kukata six packs za tumboni.kama ukihitaji tuwasiliane.