Friday, October 27, 2017

HIVI NDIO VYAKULA 11 VINAVYOPUNGUZA UNENE NA KUTOA KITAMBI.

                                    
                                 
makala iliyopita nilizungumzia vyakula vinavyoweza kusababisha mtu kunenepa sana... kama hukuona makala hiyo soma hapa  katika vyakula hivyo nilivyozungumzia kuna ambavyo ni muhimu kuepuka kabisa kama soda, biskuti, ice cream na kadhalika kwani havina umuhimu kabisa mwilini na kuna vingine vya wanga kama wali,ugali,tambi,viazi,mihogo huwezi kuacha kabisa ila ni muhimu kupunguza na kula kwa kiasi kidogo sana kulingana na shughuli zako. kupunguza uzito kunataka nidhamu sana ndio maana watu wengi wameshindwa kupungua na kukata tamaa  lakini sheria kuu ni moja, mazoezi sana na kula kidogo..bila kubadilisha mfumo wako wa maisha na kula kidogo huku ukifanya mazoezi kwa nusu saa angalau mara tatu kwa wiki hata ule dawa gani unaweza ukapungua baadae ukarudi palepale. lakini pamoja na hayo kuna vyakula ambavyo ni muhimu sana kuvila wakati unapunguza uzito kwani vinasaidia kuchoma mafuta ya mwili lakini vyenyewe pia vina nguvu au calorie kidogo sana kiasi kwamba hata vikiliwa kwa kiasi kikubwa sio rahisi kunenepesha.
mayai; mayai ya protini nyingi sana ambazo zinamtosha kifaranga kutoka ndani ya yai hilo akiwa mzima. kawaida protini hujenga misuli ikiliwa kwa kiasi kinachotakiwa.utafiti unaonyesha binadamu wa kawaida anatakiwa ale mayai angalau matatu kwa siku kuondoa uwezekano wa kuongeza cholestrol ambazo ni hatari kwa moyo. ukiamka asubuhi ukala mayai kama sehemu ya kifungua kinywa chako utakaa muda mrefu bila njaa..mayai nayozungumzia hapa ni yale anayotaga kuku mwenyewe hasa ya kienyeji.
mboga za majani; hizi ni kama mchicha, bamia, nyanya chungu,kabichi, spinachi, kisamvu, msusa na zingine nyingi...mboga hizi zina vitamini nyingi, fibres au nyuzi nyingi na  wanga kidogo hivyo zinaweza kuliwa kwa kiasi kukubwa na kujaza tumbo bila kusababisha unene lakini pia zinaitwa kitaalamu kama antioxidant yaani zinaweza kuondoa sumu mwilini.
samaki; samaki wana kiasi kidogo sana cha mafuta, wana protein nyingi ambayo itakuacha muda mrefu ukiwa umeshiba na kukufanya usile sana...lakini pia samaki wana kemikali ya omega 3 ambayo ni muhimu sana kwenye mwili kwani huzuia magonjwa ya moyo na kusaidia kazi ya kuchoma mafuta.
maharage; hichi ni chakula kizuri sana cha asili ambachi kimewakuza watu wengi,  kina protini ya kutosha pamoja na fibre yaani nyuzi ambazo ni muhimu sana. lakini pia nguvu au calorie yake ni kidogo sana.
maparachichi; wakati matunda mengine yana sukari nyingi, parachichi zina mafuta na nyuzi ambazo ni muhimu sana kwa afya ya moyo na kupunguza uzito. maparachichi pia yana mafuta aina ya oleic oil ambayo yanapatikana kwenye mafuta ya mizaituni au olive oil  na hua yana maji mengi na kumfanya mlaji kutoishiwa maji mwilini.
karanga na korosho; japokua vyakula hivi vina mafuta, mafuta yake ni salama sana hayanenepeshi kama mfuta yatokanayo na wanyama...tafiti zinaonyesha kwamba mafuta haya huweza kuongeza kasi ya uchomaji wa mafuta mwilini.
                                                   
matunda; matunda yote unayofahamu yanapunguza uzito isipokua machache yenye sukari nyingi kama ndizi mbivu na zabibu..tafiti zimeonyesha watu wanaokula matunda mengi hua wanakula chakula kidogo sana sababu mafasi kubwa ya tumbo inachukuliwa na matunda ambayo hayaongezi uzito.                                                  
nyama ya kuku; hasa kuku wa kienyeji ambao wanakuzwa kiasilia, huwa na protein nyingi sana ambayo inajenga misuli badala ya kuongeza mafuta mwilini, kuku wa kisasa wana kemikali nyingi sana ambazo zinahusiana na magonjwa hatari kama kansa na kadhalika. kumbuka kama unakula kuku kupunguza uzito usile ngozi yake kwani ina mafuta mengi.
mafuta ya maji; mafuta yanayokuja kwa mfumo wa maji kama korie, mafuta ya nazi na alizeti ni mazuri sana kwani yakiingia mwilini hubaki kwenye mfumo ule ule lakini mafuta yanayokuja kwa mfumo wa kuganda kama kimbo, blueband na siagi sio mazuri kwani yakifika tumboni huganda vilevile.
viazi mviringo vya kuchemsha; japokua watu wengi hawataki viazi hivi na kuamua kuvikaanga kila wakati ili wale kama chips lakini ni chakula kizuri sana kama unataka kupunguza uzito..vina sukari kidogo na kiasi kikubwa cha potassium..
maziwa; tofauti na watu walivyokua wanafikiria zamani kuhusu maziwa kwamba yananenepesha sana, utafiti umeonyesha maziwa yanasaidia kupunguza uzito kwani yana kiasi kikubwa cha calcium ambacho husaidia kuchoma mafuta mwilini.