kitaalamu matibabu dawa kujichubua yalitakiwa yatolewe kitaalamu kwa ajili ya kuondoa mabaka ya ngozi na kuondoa makunyazi ya uzee lakini chini ya usimamizi maalumu wa daktari na matumizi yake yawe ya muda fulani tu kama dozi ya dawa lakini hali hii imekua tofauti kwani kemikali hizi zimekua zikitumika bila usimamizi na kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji.
kwa hapa tanzania tafiti zinaonyesha zaidi ya asilimia 70 ya wanawake hutumia dawa za kujichubua na huku asilimia mbili mpaka tano ya wanaume hutumia pia.
kuna aina tatu ya madawa hayo, dawa za kumeza, dawa za kupaka, dawaza kuchoma sindano na njia ya upasuaji lakini kwa hapa kwetu wengi hutumia za kupaka na wachache za kunywa.
watu wengi wamekua wakiiga wasanii wa nje kama marekani huku wakishindwa kujua kwamba wale pale wanafanya vile kwa usimamizi wa madaktari bingwa wa ngozi na kwa dozi maalumu ili wasipate madhara yeyote.
serikali imekua ikijitahidi kuyapiga marufuku madawa hayo bila mafanikio kwani watu wengi huyapitisha na kuyatumia kwa magendo wakidhani wanaikomoa serikali bila kujua wanajiua wenyewe.
yafuatayo ni madhara yatokanayo na kujichubua ngozi..
kansa ya ngozi;dawa za kujichubua zina kemikali kuu mbili yaani hydroquinone na mercury, lakini dawa nyingi zinazopatikana mtaani zina mchanganyiko wa steroids, tretinion, na hydroquinone. kemikali hizi ni moja ya vyanzo vikuu vya kansa ya ngozi na kuharibu maini.
kuongezeka kwa weusi wa ngozi; matumizi ya kemikali kama hydroquinone 2% kwa muda wa miezi mitatu mfululizo huweza kusababisha ngozi kua nyeusi zaidi na kukataa matibabu yeyote ya kuirudisha kwenye hali yake ya kawaida. lakini pia matumizi makubwa ya vipodozi hivi husababisha sehemu kama za vidole, miguu na masikio kua nyeusi zaidi kuliko sehemu zingine.
magonjwa ya ngozi; tafiti nyingi zilizofanywa na madaktari wa ngozi zimegundua kwamba watu wengi wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi kama upele, miwasho, fangasi na aleji ni watu wanaotumia kemikali hizi hatari za kujichubua.
kuharibu watoto tumboni; kemikali za kujichubua zina uwezo wa kuingia mpaka kwenye kizazi cha mama mjamzito, hali hii huweza kusababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye upungufu wa viungo fulani vya mwili kama mkono mmoja au mguu mmoja.
upofu; kemikali za kuchubua ngozi ambazo hupakwa usoni zina uwezo wa kuharibu macho na kumfanya mtu awe kipofu kabisa, mimi binafsi nimeshuhudia watu waliopata upofu sababu ya kujichubua ngozi.
michirizi ya ngozi; kwasasa kuna wanawake wengi sana wanasumbuliwa na tatizo la michirizi ya ngozi, japokua michirizi hii huletwa na unene auujauzito lakini kujichubua pia moja ya vyanzo vikuu vya hali hii.