Na kitu kikubwa kitakacho athiri mahusiano na mwelekeo gani hayo mahusiano yatachukua huwa ni kiwango cha maongezi ambacho kitatumiwa baina yako na huyo msichana moyo wako ulioangukia, kiwango cha maongezi baina yenu ni vizuri kuangaliwa maana ndo kiini kikuu iwapo ukaribu baina yenu utakuwaje na mahusiano yataendeleaje.
Ili mapenzi yaive na kunoga, maongezi baina ya wapenzi wapya ndo nguzo kuu ya kuongeza viungo na mbolea kwenye penzi linalo chipukia, maongezi huimalisha kuelewana na kuongeza hamasa ya kumjua zaidi mpenzi wako mpya na kuongeza ukaribu baina yenu, ila pia maongezi haya haya yanaweza kubadilisha uhusiano mzima na kuutoa kwanye hali ya hamasa na kuleta hali ya kutotaka kuendelea tena na mahusiano na hali hii hutokea zaidi kwa mwanamke kuliko mwanaume.
Kuna utofauti mkubwa wa hisia kati ya mwanaume na mwanamke na jinsi mapenzi yanavyotushika moyoni, na kwa utafiti uliothibitishwa na watafiti wa saikolojia na tabia husema hisia kwa mwanaume hutegemea zaidi kile anachokiona kuliko sababu yote ile nyingine, ila kwa mwanamke hutegemea zaidi kile anachokisikia kuliko sababu yote ile nyingine, ndo maana mwanaume hupenda kwa macho huku msichana hutungozwa kwa maneno mazuri.
Hakuna kitu kinachomuongezea hamasa msichana kama ile hali ya kutokujua, hali hii humfanya msichana kutamani zaidi kumsikia mwanaume anaeonyesha kumtaka na kuongezea hamasa zaidi za kihisia na kufanya aingiwe na upendo juu ya huyo mwanaume bila yeye mwenyewe kujua.
Hivyo ili kumtengenezea hali hii ya sintokujua, si vizuri iwapo maongezi kwenye mahusiano mapya yakapitiliza kupita kiasi, tengeneza hali ya kufanya azidi kutaka kujua, azidi kuwa shauku ya kukuelewa, kutaka kupata picha yako nzima ya maisha yako.
Watu wengi huwa hawajui ni jinsi gani ya kufanya mahusiano yakuwe na kutengeneza muungano wa hisia kati yake na msichana alie nae hasa wakati wa mwanzo wa uhusiano, japo huwa inategemea zaidi ni aina gani ya mapenzi tokea mwanzo umeyaanzisha.
Kuna aina kuu tatu za mahusiano, aina ya kwanza ni mapenzi ya simu, aina ya pili ni mapenzi ya mtandaoni na aina ya tatu ni mapenzi ya ukaribu, mapenzi ya kuonana ana kwa ana, uso kwa uso. Na kwa aina hizo zote, aina ya kwanza na ya pili siku zote huwa ni ngumu kufanya mapenzi yakuwe na kutengeneza muungano wa hisia kati yako na msichana.
Kiuhalisia kuna tofauti kubwa kati ya kuongea na mtu kwa njia ya simu, kuchati na kuongea nae ana kwa ana maana mawasiliano huwa ni asilimia 7 tu maneno na asilimia 93 ishala ambazo hazitumii maneno, wakati hizo ishala ambazo hazitumii maneno zikiwa na asilimia 55 ya ishala za mwili na asilimia 38 ni jinsi mawimbi ya sauti yanavyosikika. Kwa hivyo ukiongea na msichana kwa simu au kuchati ni vigumu sana kujenga mahusiano na kukuza hamasa zake kama vile ambavyo unaweza fanya ukiwa naye uso kwa uso, na njia ya uso kwa uso inakuwa na faida viambatanisha kama denda na mambo mengine zaidi ya hapo kukuza uhusiano na kuufanya kuwa mara dufu kwa muunganiko wa kimwili na kiroho.
Hakikisha maongezi yako yasiwe mengi na hata kama ya kiwa mengi, yafanye kwa kukutana pamoja na kumwambia yote moyo wako unayojisikia ukiwa unamwangalia machoni na kumpa mazuri na mema ya hii dunia