Friday, October 5, 2018

Unataka Kupendwa Anza kwa kujikubali Wewe Mwenyewe, Jipende Wewe Mwenyewe Kwanza

Kama hutajikubali mwenyewe, ukafurahia muonekanekano wako, ukasema hivi ndiyo nilivyo kama unanipenda twende kazi na kama hunipendi nipotezee basi hata kama ukipendwa na ulimwengu mzima haitasaidia kitu. Wanawake tunajali sana kuhusu muonekano, yaani namna tunavyoonekana kwa watu hasa wapenzi wetu ndiyo kila kitu kwetu. Tunatumia muda mwingi kujaribu kuuridhisha ulimwengu na namna tunavyoonekana kuliko kujiridhisha wenyewe.
Nijambo zuri kupendeza kuwa na muonekano mzuri na kuvutia, lakini kama mwanamke unapaswa kujua nini maana ya kupendeza, kuwa na muonekano mzuri na kuvutia? Kuwa na matako makubwa haimaanishi kupendeza, kwa mweupe haimaanishi kupendeza, kuwa mrefu haimaanishi kupendeza, kuwa na nywele ndefu haimaanishi kupendeza, kuwa na kucha ndefu haimaanishi kupendeza?.
Kupendeza ni ile hali ya kuufanya muonekano wako kuwa bora zaidi, kuvaa nguo kutokana na umbo lako, kuwa msafi na kunukia. Kuwa na muonekano ambao hautakufanya ujihisi vibaya au kila saa kujishukushuku. Wanawake wengi hasa mabinti siku hizi wanachanganya vitu wanadhani kujikoboa na kuongezea makalio ndiyo kupendeza, wanadhani kuvaa nguo fupi na kuka auchi ndiyo kupendeza.
Kupendeza na kuvutia kunaanzia katika nafsi yako, umepigwa pasi huna tako la mwendo kasi unaangalia na kusema ni nguo gani nikivaa itanipendeza na itanifanya kuwa comfortable. Yaani sio unavaa tight za mahips halafu ukitongozwa unaanza kuwaza namna ya kuivua, sisemi usivae lakini uvae ukiwa unajiamini hata wakati wakuvua uwe na uwezo wakusema hapa niliongezea ili iendane na nguo flani.
Lakini sio uvae kisketi kifupi halafu kila saa unaona aibu na kujiona uko uchi, vaa kisketi kifupi kwakua unapenda na unajiona unapendeza zaidi na si kwakua ulimwengu mzima unataka uvae hivyo au kwakuwa baby anapenda hivyo, no vaa kinachokufanya ujisikia vizuri. Jisikie vizuri kuhusu wewe kabla ya kutaka wengine wafurahie kukuona.
Mungu angejua wanaume wote wanapenda makalio makubwa angeumba wanawake wenye matako makubwa tu, angejua wanapenda weupe angeumba wazungu tu lakini anajua kuwa kila mtu anapenda chake hivyo kama Mungu hajakupa makalio makubwa na akaja mwanaume anataka makalio ya mwendo kasi muambie Baba umekosea njia humu pasi tu, kama kifu chako cha mwendo kasi na yeye anataka saa sita muambie umekosea njia.
Huna haja ya kujibanabana kuweka kila kitu feki katika mwili wako mpaka ukitoka bafuni anasahau ni mwanamke gani ameoa. Hambu anza leo, jikubali ulivyo na jipendezeshe kutokana na muonekano wako, kama marafiki zako hawapendi waambie wakatafute marafiki wengine kama bwana wako hependi muambie akatafute mwingine kwani hujajiumba wewe, acha kujionea aibu umzuri hivyo hivyo ulivyo jikubali.
Wengine unakuta ni wake za watu, upo na mwanaume kakupenda mpaka kakuoa lakini bado huridhiki unadhani labda umbaya au unajisikia vibaya akiongea na wanawake wengine eti kisa wewe si mweupe, huna sijui kifua cha namna gani? Kuwa na wasiwasi na kutokujikubali kutamsukuma kutokukupenda, kama wewe mwenyewe hujipendi unadhani ni nani atakupenda? Hembu jipende na tambua kua namna ulivyo ndiyo Mungu alivyotaka.