Friday, October 5, 2018

Kisa Cha Jane Na Rafiki Zake – Wakati Wa Mungu

Baada ya kumaliza chuo rafiki zake wote walipata kazi katika kampuni moja binafsI na Jane alibakia nyumbani akihangaika kuzunguka na Bahasha za kaki kutafuta kazi ofisi moja hadi nyingine. Hapo ndipo urafiki wao ulipoanza kuingia dosari kwani kila wakitoka basi mazungumzo ya rafiki zake hao yalikuwa ni kuhusu kazi na mambo ya ofisini na mara kadhaa walimtenga na kutoka wenyewe na kila alipouliza kwanini hawakumstua watoke wete walimuambia “Tulikuwa tunaongea mambo ya ofisini , si unajua siri za ofisi…”
Pamoja na yote hayo Jane alivumilia akijaribu kujiweka nao karibu kwani urafiki wao ulianzia mbali tangu wakiwa kidato cha tano mpaka chuo ambapo walisoma kozi moja nakuishi chumba kimoja wote watatu. Mwaka mmoja baadaye Fatma alichumbiwa na kuolewa na Boyfriend wake wa kutoka chuo na haikupita miezi mitatu Eva naye aliolewa na mfanyakazi mwenzake ambaye walianzisha mahusiano baaada tu ya kupata ajira.
Hicho ndiyo kilikuwa kipindi kigumu kwake kwani ndiyo wakati ambao mpenzi wake Prosper ambaye walidumu kwenye mahusiano kwa miaka mitatu tangu wakiwa chuo na kupata Scholarship ya kwenda kusoma Australia baada ya kumaliza chuo alipunguza mahusiano na kuanza kupost Facebook mpenzi wake mpya wa kizungu, Jane alipomuuliza alimuambia kapata mtu mwingine na asimsubirie.
Aliwahitaji sana marafiki zake lakini nao walimtenga na kumuona kama adui, kwanza hakuwa na kazi na pili alikuwa hajaolewa. Mara nyingi sasa walikuwa wakitoka na waume zao na kwakuwa yeye hakua hata na Boyfriend asingeweza kutoka nao kabisa. Mara chache ambazo alitoka nao walikuwa wakiongea kuhusu ndoa. ile hali tu ya kumuonea huruma kuwa hajaolewa ilimfanya ajisikia vibaya.
“Wewe mzuri Jane, na shape lako hilo nakushangaa unakuwa peke yako, si utafute hata mzee wa kupumzika naye akuondolee mawazo… Kuna Baba mmoja pale ofisini huwa anakuangaliaga ukija..sema nikuunganishe naye…” Sikumoja Eva alimuambia kiutani utani lakini alionyesha kumaanisha. Jane alijua wanamchora lakini hakukasirika, wakati huo alikuwa mpweke na aliwahitaji marafiki sana, alimjibu tu kwa upole “Wakati Mungu bado, nina hamu sana ya kuolewa lakinsiwezi lazimisha, wakati wa Mungu ukifika nitaolewa..”
*********
Kule ofisini mambo yalizidi kuwanyookea rafiki zake, miaka miwili baadaye Eva alipandishwa cheo kuwa mhasibu Mkuu huku Fatma akihamishiwa Morogoro kuwa meneja wa moja ola tawi la kampuni hiyo ambayo ilikuwa na matawi katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Arusha na Mbeya. Habari zile Jane alizisikia siku alipoenda ofisini kwao kupeleka barua yake ya ajira, alisikia kuna nafasi zilitangazwa pale na alipofika alitaka kuonana na rafiki zake ili angalau wampigie pande apate nafasi ya uhudumu.
Pamoja na digrii yake lakini aliamua kuomba kazi ya uhudumu kwani alishachoka kukaa nyumbani miaka mitatu bila matumaini ya kupata ajira, alijua kama angeweza tu kuingia kuajiriwa basi ungekuwa ndiyo mwanzo mzuri kwake katika kupata kazi anayoitaka. Alipoulizia ndipo alipoambiwa kua Fatma kashahamishwa na Eva sasa ni bosi, alielekezwa ofisini kwake na alipofika na kukutana na Secretary wake aliambiwa asubiri kama wageni wengine waliokuwa pale.
Alikaa nakusubiri huku akishangaa kuwa rafiki yake ambaye walilala chumba kimoja wakitaniana na kushea kila kitu alikuwa na secretary, alimshukuru Mungu kwa hilo na kumuombea. Alisubiri sana wageni wote waliingia na kutoka wakiruhusiwa na secretary ambaye alipiga simu kwanza, alibaki mwenyewe pale na ilipofika zamu yake kabla ya kuingia alikuja kijana mmoja wa makamo.
“Dada subiri kwanza, karibu bosi..” Secretary aliongea akimzuia kuingia na kumruhusu yule kijana, yule kijana alitembea mpaka mlangoni na kuufungua mlango, “Ulikua unaingia huku?” Aliuliza yule kijana. Bila kuongea kitu akiwa amechoka alitingisha kichwa kukubali “Basi ingia mimi nitasubiri..” Yule kijana alimuambia, Jane alikataa kwa heshima akimuambia aingie tu yeye hakua na haraka lakini yule kijana naye alikataa.
Baada ya kusikia neno Bosi Jane aliogopa kabisa akijua asipooonyesha nidhamua hata kazi hatapata hivyo alisisitiza aingie kuwani yeye hakuwa na haraka. Kijana alifunga mlango na kwa utani alisema “Basi kama na wewe hutaki kuingia tusubiri wote..” Huku akitabasmau Jane aliingia, alimkuta rafiki yake yuko bize na alimsalimia kwa bashasha lakini aliitikiwa kwa mkato bila bashasha yoyote, kabla hata hajasema chochote alimuambia “Naomba ongea harakaharaka maana nina kazi nyingi si unaona…”
Eva aliongea huku akimuonyesha lundo la mafaili. Mapokezi yale yalimfanya Jane kupoteza pozi kabisa, alikuwa akiongea na mtu ambaye akili yake haikuwa pale. Alizuga tu kuwa alienda pale kusalimia na ili asimsubirishe yule Kaka muda mrefu, aliaga na kutoka, Eva hata hakumsindikiza alinyanyua tukichwa kidogo akasema poa siku njema kisha akaendelea na kazi zake. Jane alitoka huku amenyong’onyea.
Pale nnje yule Kaka aliyeonekana mchangamfu alikuwa bado anasubiri. “Umeshughulikiwa?” Yule Kaka alimuuliza, “Ndiyo kaka ahsante…” Alijibu huku akilazimisha tabasamu. Alitoka taratibu, alipofika mapokezi aliwaaga vizuri, alitembea mpaka getini lakini kabla hajatoka mlinzi, alimuambia subiri kwanza. Jane alishangaa kwani hakua maefanya kitu kibaya, alisimama kusubiri na alipogeuka ndipo alipokutana na yule Kaka akija akitembea kwa mwendo wa kasi, sasa alikuwa na wasiwasi zaidi akihisi labda kuna kitu kibaya kafanya.
**********
“Samahani kwa usumbufu…” Yule Kaka alianza kuongea, kumbe baada tu ya yeye kutoka yule kaka alimfuata nyuma na alipomuona anaagana na dada wa mapokezi alienda moja kwa moja kumuuliza yule ni nani ndipo aliambiwa alileta barua ya maombi ya kazi na hapohapo alichukua simu ya mapokezi na kumpigia mlinzi akiamuambia asimruhusu yule jane kutoka, alimuita na kumuaomba arudi ofisini kwake.
Yule Kaka alikuwa ni Samwel, mtoto wa mmiliki wa ile kampuni ambaye alikuwa Uingereza kimasomo, ni miezi sita tu alikuwa amerejea na Baba yake ambaye alikuwa na makampuni mengine akimuachia kuendesha ile kampuni kama Mkurugenzi mkuu lengo lake likiwa ni kumuandaa ili kuendesha makampuni yake yote kwani alikuwa ndiye mtoto wake wapekee wakiume akaiwa na mdogo wake mmoja wakike ambaya bado alikuwa chuo.
Jane hakusita alirudi kwa wasiwasi na alipoingia Samweli liagiza kueltewa faili lake na akuanza kulipitia. “Mbona CV yako nzuri namna hii, hii GPA…halafu unaomba kazi ya uhudumu…” Aliongea kama utani, Jane alimuelezea namna kupata kazi ilivyokuwa ngumu, taratibu walianza kuongea mambo kadhaaa, Sam ambaye alikua muongeaji sana alipiga klila story na akujikuta wamezoeana, muda ulikimbia mpaka jioni iliwakuta pale.
Jane alipotaka kuondoka Sam alimuomba ampe lift kwakuwa hakuwa na usafiri akifikiria kusukumana katika daladala alikubali. Kilichofuatia hapo ni historia, Sam alivutiwa na Jane mara ya kwanza tu alipomuona na alipogundua kua si mke wa mtu hakupoteza muda, walijikuta wanaingia katika mahusiano, alimtambulisha nyumbani kwao ambao walitaka aoe harakaharaka. Kama mtoto wa wakwanza kila siku walikuwa wakimpigia kelele kuoa mama yake akitaka wajukuu.
Miezi sita baadaye walikuwa ni mke na mume, Sam alipanda cheo kusimamia makampuni yote ya Baba yake akisaidiwa na mkewe ambaye alipewa kusimamia kampuni ile ile waliyokuwa wakifanya rafiki zake Eva na Fatma. Hii ikimaanisha kuwa mbali nakuwa sehemu ya umiliki alikuwa bosi wao na walikuwa wanalazimika kuriporti kwake. Pamoja na yote waliyomfanyia lakini Jane hakubadilika aliendelea kuwachukulia kama marafiki zake ingawa walikuwa wanajitenga kwani walikuwa wanajisikia vibaya na hawakujiona tena kama watu wa hadhi yake. Jane alikuwa akiingia mpaka kwenye vikao vya bodi ya wakurugenzi wakati wao walikuwa ni wafanyakazi wa kawaida tu.
Jane sasa ana ujauzito wa miezi tisa na anakaribia kujifungua, Familia nzima ni kama imechanganyikiwa kusubiri mjukuu, Mama mkwe hataki hata anyanyue kikombe, wifi yake kila siku ni kuchagua majina mapya ya mtoto wa Kaka yake, Baba mkwe anafuraha zaidi kwani tayari ameshajua kua mjukuu wake wa kwanza ni wakiume anauhakika mali zake hazitaenda mbali. Fatma na mumewe bado hawajafanikiwa kupata mtoto, Eva ana mtoto mmoja na nimjamzito wa mtoto wao wapili, huku ndoa yao ikiwa mashakani kwani ameshamfumania mumewe zaidi yaa mara tatu na wafanyakazi wenzake lakini hana namna analazimika kuvumilia tu.
*******MWISHO
KILA GUMU, CHANGAMOTO UNAYOPITIA JUA KUWA KUNA WAKATI WA MUNGU, HUO UKIFIKA HATA SHETANI ATASIMAMA PEMBENI KUKUSUBIRI UPITE HAKUNA WA KUKUZUIA.