Thursday, October 11, 2018

HIZI NDIO NJIA SABA ZA KUACHA PUNYETO KABISA


Karibuni tena wapendwa wasomaji wa blog hii ya siri za afya bora na kama kawaida leo tena unapata shule nyingine ambayo namatumaini inaendelea kukujenga kiakili na kiafya..
Makala iliyopita niliongelea madhara yanayosababishwa na kupiga punyeto kama hukusoma hii hapa  lakini nilipokea simu nyingi ambazo zilitaka pia niongelee suluhisho au jinsi gani mtu anaweza kuacha punyeto kabisa
Punyeto kama tulivyoongea ni tatizo la tabia na linaweza kudhibitika kabisa kama matatizo mengine yeyote. FANYA YAFUATAYO....                                                   

  •  Acha kuangalia video za ponograph: video hizi ndio chanzo  kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo  na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto hivyo  kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako..                                                                                                                                                                            Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.
  •  Epuka kukaa nyumbani peke yako; mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
  • Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa, kuumwa kichwa na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.
  • acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema ivoivo, kama unaacha acha mara moja.
  • Tafuta mpenzi kama huna kabisa: ukiwa na mpenzi madhara ya punyeto kama kupungukiwa nguvu za kiume yatakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto. pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.
  • anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine:hii itakufanya ue bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko,  pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala.