Saturday, October 20, 2018

DALILI 10 MWANAMKE ULIYENAYE ANAKUSALITI

Kwenye dunia ya mapenzi ya sasa kuna mambo mengi sana ambayo huwaliza kama sio kuwakosanisha wapenzi na mwisho wa siku wakaachana na kuacha simanzi mioyoni mwao, Miongoni mwa mambo makubwa yanayosababisha wapenzi kuachana ni pamoja na USALITI.

Kwa leo tujaribu kuangalia kwa upande wa wanawake, ni kitu gani/ni dalili gani ukiziona basi ufahamu kuwa mwanamke uliyenaye anakusaliti na kuna uwezekano usiwe na maisha marefu ya kimapenzi naye.

Hizi ni baadhi ya dalili kuwa mwanamke uliyenaye amechoka aina ya mapenzi unayompa na anataka kuondoka na anakusaliti ikiwa ni njia mojawapo ya kutimiza nia yake;


1.       Kama akianza ghafla kujijali kupita kiasi kwa muonekano wake basi unatakiwa kuanza kumtilia shaka, kwa kipindi chote mmekuwa pamoja amekuwa ni mtu wa muonekano unaoendana nawe lakini ameanza kutafuta muonekano mpya na tofauti kabisa na ule ambao umeuzoea na unaoupenda, anaweza kuwa ameanza kuwa na muonekano tofauti kwa sababu amepata mtu ambaye angependa awe vile, anaweza kuwa mfanyakazi mwenzake, mwanafunzi mwenzake, mfanyabiashara mwenzake na hata bosi wake.


Ameanza na kwenda gym ili kuweka mwili kwenye shape tofauti na ile uliyoizoea na unayoipenda wewe, amekuwa ni mtu wa make up hata kama anataka kwenda kununua vocha tu dukani nje, anza kuwa makini na mienendo hii, inaweza kuwa ni mabadiliko ya kawaida na pia inaweza kuwa mabadiliko yasiyo ya kawaida.

2.       Mwanzoni alikuwa ni mtu wa kuwapenda watu wako wa karibu wakiwemo ndugu zako na marafiki zako lakini kwa sasa amepunguza kabisa kuwa nao karibu kama sio kuacha kabisa, anakuwa anaogopa na kuwa na wasiwasi kwa kuwa nao karibu tena atashtukiwa kuwa anakusaliti kwa hiyo anaona njia nzuri Zaidi ni kuwa na excuse kila mara marafiki zako au ndugu zako wanapomhitaji kuwa naye siku za kawaida au weekend au hata kuwasaidia kwenye baadhi ya vitu ambavyo mwanzoni ilikuwa ni rahisi kutoa msaada kwao.

3.       Mabadiliko mengine utayaona kwenye kufanya mapenzi, mlishazoea kufanya mapenzi mara mbili kama si mara tatu kwa wiki na amekuwa ni mtu muwazi na anafurahia sana mapenzi lakini ghafla anaanza kuwa ni mtu wa kukimbiakimbia linapokuja suala la kufanya mapenzi, anakuwa hayupo comfortable na haonyeshi kuyafurahia tena mapenzi yenu, 
      
      Kwa manaume kama anaenda nje ya mahusiano na msichana huwa anapenda Zaidi kufanya mapenzi na huyo mpya aliyempata lakini pia haoni aibu kufanya na wewe mwanamke wake wa zamani kiasi kwamba unaweza kutokufahamu upesi kama anakusaliti/Inachukua muda, lakini kwa mwanamke hali ni tofauti, akianza kukusaliti hata akiwa kwako anakuwa anajisikia vibaya na kama umemzoea kupita kiasi utamshtukia kuwa hayupo sawa.
Kutokutaka kufanya mapenzi nawe ni dalili tosha kuwa hayafurahii tena mapenzi yenu na haridhiki nayo,anaona kama unamghasi tu na anatamani aondoke.


4.       Mwanamke aliyekuchoka ana anayetamani kuondoka kwako kwa kuwa amepata mtu mwingine ataacha kukujali kama zamani, vile vitu ulivyozoea akufanyie vitapungua sana kama sio kuisha kabisa, ataanza kuwa na sababu ukimwambia akusaidie kitu, kama alizoea kuja kwako na kufanya usafi wa nyumba basi itapungua kama sio kuisha na hutakumbushwa vitu muhimu vya kimaisha vya kufanya na kuna wakati unaweza kumkosea na akakuacha tu bila kuhangaika kukurekebisha kama zamani.

5.       Mwanamke anayekusaliti ataanza kupunguza ule uwazi aliokuwa nao kwako, kuna baadhi ya mambo ambayo alikuwa anayafanya kwa uwazi sana mbele yako lakini kwa sasa ataanza kuyafanya bila uwazi na kuna wakati asikushirikishe kabisa, mwanzoni alikuwa anaweza kuacha simu au laptop mbele yako na asiwe na wasiwasi lakini kwa sasa anakuwa ni mtu wa kujifichaficha na anaziwekea password simu na laptop na hata uongeaji wake wa simu unakuwa tofauti na zamani na anakuwa ni mtu wa kuwa bussy muda mwingi na simu kuliko zamani akiwa mbele yako/mkiwa wote.

6.       Zamani ilikuwa rahisi sana kumpata pale unapomhitaji iwe face to face au hata kwa simu, lakini hali kwa sasa imekuwa tofauti. Amekuwa ni mtu wa kuwa bussy kila wakati na kuna wakati unapiga simu haipokelewi na unaweza kukaa masaa nane ndo unajibiwa meseji yako na hali hii inatokea mara kwa mara na kila ukimuuliza alikuwa wapi kujibu simu au kujibu meseji anakujibu hakuisikia ikilia au iliisha chaji. Fahamu hapo kuna mtu mwingine amechukua nafasi yako na unatakiwa kuanza kujiandaa kwa safari mpya.


7.       Kuna jina jipya la mwanaume limekuwa halikauki mdomoni kwake na ukimuuliza maswali kumuhusu huyo mtu amekuwa ni mtu wa kumponda kwa sababu hataki umjue vizuri na hataki uendelee kumuulizia akijua utamshtukia, unatakiwa kuanza kufuatilia nyendo zake kwa huyo mtu kwani ni dalili tosha kuwa ameanza kutoka nae au yupo njiani kutoka nae, ukimuuliza Zaidi atakwambia ‘’ni rafiki tu’’ na usiwe na mashaka naye.
8.       Zamani ilikuwa ukimkosea anakuwa ni mwelewa na anachukua muda mfupi kukusamehe na kuendelea na furaha yenu ya mahusiano, lakini kwa sasa amekuwa ni mtu wa kukutafutia makosa kila wakati na ikitokea umekosea kidogo tu ataufanya ugomvi wenu kuwa mkubwa kuliko maelezo na anakuwa ni mtu wa lawama tu bila kutafuta suluhisho la ugomvi wenu, ukianza kuona dalili hizo hakikisha unaanza uchunguzi mapema ili usije kulia mwenyewe.

9.       Kuna wakati mwanamke akitaka kukusaliti anaanza kuwa interested sana na ratiba zako za kila siku kiasi kwamba unaweza kudhani anakujali kupita kiasi kumbe anataka kufahamu muda Fulani utakuwa wapi ili aweze kukusaliti vizuri, njia nzuri ya kumkamata ni kumwambia utakuwa sehemu Fulani na utachelewa lakini ukafanya kitu tofauti na ulichomwambia, unaweza kukuta unaliwa chakula chako na ulikipika mwenyewe, kuwa makini.

10.   Zaidi ya yote, dalili mojawapo kuwa mwanamke wako anakusaliti ni pale Unapoanza kuhisi ndani ya nafsi yako kuwa mambo hayaendi sawa kwenye mahusiano yenu kama zamani, hisia zako zinakuambia kuwa inawezekana mwanamke wako akawa anakusaliti, hii ni dalili nyingine kuwa kuna kitu unatakiwa kukifanya kwenye mapenzi yako, kuna wakati hisia huwa zinasababishwa na mienendo tofauti ya mtu wako na mara nyingi hisia hukupeleka kwenye ukweli.