Wanaume wanaougua maradhi ya kisukari huweza kuwa katika hatari kubwa ya kukubwa na upungufu wa nguvu za kiume kuliko wanaume wasio na maradhi hayo.
Inapotokea sukari haikudhibitiwa katika damu huweza kusababisha kuharibika kwa neva na misuli midogo inayodhibiti kusimama kwa uume.
Hata hivyo, mbali na sababu hizo za magonjwa pia kuna sababu nyingine za kibinadamu ambazo huweza kuchangia tatizo hilo la upungufu wa nguvu za kiume ikiwemo hizi zifuatazo ambazo huchangiwa na wanawake.
Usafi kwa mwanamke
Hali ya usafi ni muhimu hasa zile sehemu muhimu ambazo huusika kwenye tendo la ndoa endapo mwanamke atakuwa si msafi basi huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.
Naamini kwamba kila mtu hupenda usafi na wengi wetu tunafahamu kero za uchafu wakati wa tendo, kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu huweza kusababisha mwanaume kupoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa.
Mwanamke kuwa msafi ni muhimu sana, kuanzia mavazi na mwili pia hii itasaidia kuleta msisimko zaidi katika mapenzi.
Kutokuwa na uhodari na ujuzi
Wanawake wengi huhofia sana kuonesha ujuzi wao wa kimapenzi wanapokuwa na wapenzi wao, huku wengi wakiogopa kuhisiwa huenda ni wazoefu zaidi katika masuala hayo ya kimapenzi, lakini si kweli ujuzi na uhodari kwa mwanamke ni muhimu zaidi kwani huleta hamasa kwa mwanaume na hivyo kumsaidia kuepukana na shida ya upungufu wa nguvu za kiume.
Tatizo hili lipo zaidi kwa wanawake ambao tayari wapo ndani ya ndoa, wengi wao huwa hawajishughulishi kumsaidia mwanaume kupata mihemko zaidi na wala hawana ubunifu jambo ambalo humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea hisia zake mwenyewe pekee, hali ambayo si nzuri kwani mwanaume ikitokea atakuwa na mawazo au kuchoka hatoweza kupata mhemko kwasababu hapati ushirikiano toka kwa mwenzake (mwamke).
Karaha za maneno
Pale inapotokea mwanamke akawa ni mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi basi hali hiyo huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Jambo ambalo baadaye husababisha wanaume wengi kuanza kutoka nje ya ndoa zao.