Sunday, May 13, 2018

Wanawake njooni hapa ! mjionee madhaifu yenu

Hii ni maalum kwa wanawake tu!

Wanaume ni wachafu sana hawafui nguo zao za ndani huzirudia mara kwa mara na hii huwa sababu maradhi kama ya fungus kuwasumbua mara kwa mara. Kazi ya kufua ni yako wewe mwanamke hakikisha unafua nguo za ndani za mpenzi wako

Wanaume hawafui mataulo. Mara nyingi huwa yana harufu nzito. Wanaweza kutumia taulo hata mwezi mzima bila kulifua. Kazi ya kufua ni yako wewe mwanamke fua taulo za mpenzi wako.

Wanaume hawapigi mswaki wanapomaliza kula mlo wa usiku hivyo midomo yao hutoa harufu mbaya sana. Mkumbushe mpenzi wako kupiga mswaki kabla ya kulala

Wanaume hawaogi usiku. Hulala wakinuka jasho haswa ile mikoa ya baridi au wengine hata sehemu za joto. Mwanamke mkumbushe mpenzi wako kuoga walau kabla ya kulala

Wanaume hawafui soksi hali hii huwafanya miguu yao kuwa na harufu mbaya na kuleta kero kwa jamii, we mwanamke fua soksi za mpenzi wako

Wanaume hawanyoi nywele za sirini mara kwa mara zinapokuwa ndefu. Ewe Mwanamke hii ni kazi ya mikono yako mwenyewe. Mnyoe manywele ya huko mpenzi wako

Wanaume wengi hawapaki mafuta sehemu mbali mbali za miili yao. Sehemu kama makalioni na miguuni. Hii huwafanya ngozi za maoneo tajwa kuwa kavu na ngumu zilizozeeka. Sehemu za makalio huwa na vipelevipele na ngozi ya eneo hili huwa kama ganda la limao. Ewe mwanamke mpakae mafuta mpenzi wako makalioni na miguuni ili kusaidia uchakavu wa ngozi usiendelee

Wanaume hawatoi pesa hadi waombwe. Ewe mwanamke usiache jambo hili likupite hata dakika moja. Muombe pesa mpenzi wako mara kwa mara kadri iwezekanavyo.