Sunday, April 8, 2018

KISA NA MKASA - USHAURI KWA WADADA

Nawasalimuni nyote ndugu zangu!!

Niwakati mwingine tena ningependa ku-share na nyie mkasa huu ulionipata!

Nilikua na boyfriend wangu ambaye wakati akiwa chuo mimi nilikua nafanya kazi, tumeishi pamoja sasa yapasa miaka 4 ikiendea na miezi 7, kwa kweli nilimpenda mwenzangu kutoka moyoni, shida yake ilikua yangu, huzuni yake ilikua yangu, familia yake ilikua yangu, katika kipindi chote tulicho kuwa pamoja sikuwahi kujuta hata siku moja, alikuwa ni. . ..
mwepesi kuomba msamaha anapokosea, nikasema jamani nimepata mume, baada ya kumaliza chuo, niliendelea kumsaidia kutafuta kazi pamoja na kutunza familia yake, mpaka siku alipopata appointment ya kuanza kazi sehemu fulani, nikamshukuru Mungu nikasema sasa tutasaidiana na mwenzangu.

Mpendwa huwezi amini, siku hiyo nikiwa katika harakati zangu za kulitumikia Taifa nikashangaa msg imeingia, kila nikiisoma sielewi, imeandikwa hivi, "IT IS MY HARDEST TIME SINCE MY HEART IS TROUBLED!! WHAT AM IN AND WHAT AM PASING THROUGH, IT IS VERY DIFFICULT SINCE IT IS IN THAT WAY, MY MOUTH FAIL WHAT 2SAY, MOYO UNANIUMA LAKINI LAZIMA NIKWAMBIE, NIMEPATA MSICHANA MWINGINE, I HAVE TO MARRY HER".

Sikuamini mboni za macho yangu, niliona kama lens ya miwani yangu imeharibika, nikavua miwani nikaifuta nikafikicha macho yangu, then nikarudia ile msg lakini haikuwa na mabadiliko, niliona kama ni mchezo wa kuigiza, niliona kama haiwezekani, siku yangu iliharibika, nikajirudia nyumbani mnyonge kama kinda la shomoro lililonyeshewa na mvua.

Mpendwa, huwezi kuamini baada ya siku mbili tu kupita, rafiki yangu mmoja aliniletea kadi ya harusi akiwa na tahamaki kubwa, akaniambia hivi umesikia fulani anataka kuoa? na kadi yake hii hapa nimepewa ya mchango, sikusema neno, nakumbuka ilikua cku ya jumanne, ilipofika jumapili baada ya ibada, binti mmoja akanifuata akaniuliza dada na wewe unakwenda kwenye kikao cha mtu fulani?? (akimtaja huyo aliyekuwa boyfriend wangu),baada ya hapo nikampigia simu mama mmoja rafiki yangu ambaye anahusika na mambo ya ndoa pale kanisani, nikamwambia kumbe mtu fulani anataka kuoa? akajibu akaniambia eeh anataka kuoa, nikamwambia kumbe alikua na mchumba, akanijibu ndio, mbona tangu mwaka juzi aliniletea mchumba wake akamtambulisha kwangu?? sikua na la nyongeza nikakata simu baada ya kuongea nae mambo mawili matatu hivi.

Wasichana wenzangu, nadhani mtakua mnajua hali ambayo napitia kwa sasa, kwa kua hata kama ww hukupitia hali hiyo, basi ndugu yako au rafiki yako alipitia hali ninayopitia kwa sasa!! nilirudi nyumbani nikalia sana, nikamuuliza Mungu kwanini umeacha jaribu hili linipate mimi, kwanini umeacha aibu hii inipate mimi, je kupenda ni dhambi? nililia niliponyamaza nikamwambia Mungu, sitaki kulia tena kwa sababu ya mwanaume, hakika nimetambua kuwa adui yako ni wa nyumbani mwako, ni kweli nimepoteza muda wangu mwingi, ni kweli nimekataa wanaume wengi walio taka kunioa, lakini jambo moja ninajua wewe ni MUNGU WA NYAKATI NA MAJIRA mimi nitasubiri tena!

Hili ndilo lililonipata mwaka huu, nilitaka niwashauri wasichana wenzangu mambo haya
1. usimwamini mwanaume wa aina yeyote, hata akuite majina gani mazuri.
2. Take a good care of yourself,
3. Love n dont count on anybody on that, at the end of the day it's u who live ua life! Live the life u want!
4. Usikubali relation ya muda mrefu hata siku moja
5. Yarudie rudie maneno haya moyoni mwako "Dear God, I want real love and to be loved unconditionally. Please forgive me of my sin and show me what is real love. I surrender my heart to you and ask that you take control of my life now. Thank you.