Monday, April 9, 2018

HAWA NDIO WANAWAKE. . . USIULIZE NINI MANAKE NNINI?

Siku ya kwanza atakuja na chup* mbili, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi anaondoka... Siku ya pili anakuja na khanga, anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka... Siku ya tatu anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Honey nitunzie nimesahau hereni zangu mezani 'Siku ya nne anakuja na nguo mbili na vipedo vya kubadilisha na viatu pea mbili, anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack, asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo.. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadhaa, na ole wako uvihamishe alipoviweka, kesi zinaanza... Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza... Anahamia tartiiibuuu... Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na 'Foundation' ...My Brother, huna haja ya kuuliza,Ndo kashahamia huyo....Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my days', Zamani nilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku hizi kuna Missed days, ukiambiwa hivi tu jua imekula kwako, inawindwa ndoa.... 
Wanaumee, Mpoo?? Msiseme  sikusema.