Saturday, January 27, 2018

TURUDI CHUMBANI: MAMBO YATAKAYOKUFANYA UONEKANE BORA KWA MPENZI WAKO MUWAPO CHUMBANI.

Wapenzi ambao wapo katika uhusiano lakini hawajui mambo ya kufanya ili wawe bora kwa wapenzi wao. Mada hii itagusia pande mbili. Upande wa kwanza ni kwa wale ambao ndiyo kwanza wapo katika hatua za mwanzo kabisa na wapenzi wao na upande wa pili ni kwa wale ambao tayari wapo katika uhusiano lakini hawajui jinsi ya kuwafanya wawe bora kwa wapenzi wao.

Inawezekana wewe ukawa mmoja wao, sasa huna sababu ya kukata tamaa na kuona kuwa huna thamani tena kwa mpenzi wako. Kwa kufuatilia vyema vipengele 10 vifuatavyo, nina imani utakuwa mpya na penzi lako litazidi kudumu zaidi na zaidi.

1. MWANZO WA PENZI
Siku zote nimekuwa nikisisitiza kuwa, jinsi unavyoanza ndivyo utakavyomaliza! Kama ulianza vibaya uhusiano wako tegemea kumaliza vibaya, lakini kama

Kama unatarajia kuingia katika uhusiano na mpenzi mpya hakikisha hujionyeshi tofauti na hali yako halisi ilivyo! Jifunze kujikubali, hata kama unafanya kazi ambayo unadhani ni hadhi ya chini, mbainishe mpenzi wako hali halisi ilivyo. Kama anakupenda, kazi yako haiwezi kupunguza mapenzi baina yenu.

Ikiwa ndiyo kwanza mnaanza uhusiano, zingatia hili, na kama mpo katika uhsiano kwa muda mrefu ukagundua wazi kuwa kuna mahali ulikosea, anza kufanya mabadiliko kuanzia sasa. Bado hujachelewa, mwambie ukweli naye atakuheshimu kutokana na ukweli wako.

Kudanganya hakuna mantiki, kudanganya ni utumwa, usikubali kuingia katika utumwa au kifungo cha aina hiyo. Ukweli ni silaha ya kwanza katika mapenzi, anza hivyo kuanzia mwanzo na kama ulikosea, ulijisahau au hukujua, basi anza leo!

2. USIJICHUKIE
Itakuwa kichekesho kama utasema unampenda mpenzi wako wakati wewe mwenyewe hujipendi! Huwezi ukasema unamthamini mpenzi wako wakati thamani yako mwenyewe huitambui.

Naamini tunakwenda sawa, kama unashindwa hata kuoga na kubadilisha nguo safi nani atakayekupenda? Huwezi kuwa wa kisasa kama huzingatii usafi, hakuna atakayevutiwa na wewe kama wewe hutaki kujivutisha. Sio ajabu mpenzi wako akakutosa kwa sababu tu huna muonekanano mzuri kwa rafiki zake.

Nani atakayekupenda wakati wewe mwenyewe huonyeshi kama unajitambua?
Jikubali, jithamini! Kuwa msafi wakati wote, kauli zako ziwe safi siku zote mpenzi wako atakuwa huru kuwa na wewe. Isifikie hatua mpenzi wako akataka kutoka na wewe lakini akasita kwasababu hajui ukija utakuwa umevaa nguo za namna gani. Upo hapo?

3. MWONEKANO WAKO
Mwonekano wako unaweza kukuanisha jinsi ulivyo kwa wanaokutazama, wakati mwingine inawezekana ukatafsirika tofauti na ulivyo kutokana na jinsi unavyovaa na tabia zako zingine!

Lazima uwe kijana wa kisasa, kwa kuzingatia hilo unapaswa kuwa makini kwa kila kitu kinachoonekana kwa wanaokutazama. Jenga mazoea ya kutambua aina ya nguo na mahali ulipo, usivae nguo za ufukweni ofisini au nguo za mtaani ukavaa ofisini!

Wanaokuangalia wanapata taswira ya jinsi usivyo makini au makini kutokana na mavazi yako. Vaa nguo safi kila wakati, labda kama unafanya kazi ambayo inakulazimu kuwa mchafu, ila baada ya hapo unapaswa kuwa msafi. Ukizingatia hili utamfanya mpenzi wako afurahie kuwa na wewe siku zote. Amini popote ulipo, jinsi ulivyo ndivyo anavyoonekana mpenzi wako.
Itaendelea wiki ijayo.Credit kwa Joseph shaluwa