Sababu kubwa ya kwa nini watu wa kisasa wanachukia urafiki na uchumba ni kwa sababu kila mtu anavutia mwingine lakini hakuna mwenye kutumia nguvu na akili ya kutaka kumjua zaidi mtu anayevutiwa naye.
Sio kwamba mvuto hauko pale , upo, Lakini hakuna nguvu wala akili ya katika yote. kuanzia kwenye meseji za kawaida zilizo rahisi kwa ajili ya kupata muda wa kuwa pamoja, Kila mara kuna kitu kinakosekana , kitu fulani hakiko sawa na kila mara inaonekana kuna ugumu katika kukutana .
Mvuto ni wa muhimu lakini mvuto bila ya kutumia nguvu na akili hutaweza kufika popote.
Nguvu ina maana , kujaribu, ina maana ya kuwa na muda wa pamoja hata kama unaogopa , Ina maana kumpa mtu nafasi kabla ya kuamua kama hujawa tayari.
Nguvu ni jinsi ya kuonyesha kumpenda mtu , ni jinsi unavyoenda kuongea naye ili kumfahamu , na ni jinsi unavyoenda kutaka kuwa pamoja kwa muda wa kutosha na kuonyesha kuwa unataka kushirikiana naye katika maisha.
Nimekuwa nikiweka hisia za kimwili na mvuto juu kuliko kitu chochote, Na pale ninapofikiria ni vya muhimu. Nimetambua kuwa havitoshelezi bila ya kuongeza nguvu zako na kutunza maneno unayosikia kutoka kwao . kufahamu kuwa mtu kukupenda haitoshi kama hutajiongeza.
Nafahamu maoni ya wengi ni kuhusu kiwango cha mtu kilingane na kiwango cha mwingine, ni kweli lakini haina maana kuwa hakuna maendeleo kwa sababu hakuna mawasiliano ya kutosha. Ina maana ya kutumia uwezo zaidi wa kiakili, kujua mbinu mbalimbali.
Kwa sababu kama utaweza kutumia nguvu na kutambua kuwa ni wewe pekee ndio unajitahidi lakini upande mwingine hakuna, hapo itakuwa ngumu kuendelea. Ni ngumu kuendelea kwa sababu mwingine hatumii nguvu kukutafuta ili muweze kukaa pamoja na kufahamiana. Huwezi kutunza kama hupati ushirikiano.
Kwa hio Wakati mwingine sitaangalia mvuto tu au hisia tu, Nitatazama nguvu iliopo. Nitaangalia mtu mwenye kutafuta muda wa kuwa na mimi. Mtu ambaye haogopi kuuliza maswali, Mtu ambaye hasubiri muda sahihi wa kuniomba kutoka naye. Nitatazama mtu ambaye anajaribu , mtu anayeweka nguvu na kunifanya mimi niongeze nguvu zaidi.
Kwa sababu hicho ndicho kila mtu anakihitaji . Uhakikisho. Tunahitaji kujisikia kukubalika na kutazama jinsi kila kitu kinavyoendelea. Kutazama kitu gani kinatokea unapoongeza nguvu ya pamoja. Kutazama jinsi mahusiano yatakavyokuwa mazuri.