Skin Tags ni vile vimaoteo vya ngozi vilaini vyeusi au brown ambavyo huota sehemu mbalimbali za mwili, kama vinavyoonekana hapa
Kwanini unapata Skin tags? Inasemekana mambo yafuatayo hupelekea kupata skin tags
1. kurithi 2.Baadhi wanahusisha skin tags na maradhi ya kisukari 3.Umri mkubwa 4. Msuguano wa ngozi, Mfano shingoni kutokana na uvaaji mikufu 5. Mabadiliko ya vichocheo (hormones) 6. Matumizi ya madawa yenye vichocheo ( steroids) bila kufuata ushauri wa daktari
Njia za kuweza kuondoa
1. Kutumia Tea Tree Oil
Mafuta haya yanasemekana kuwa na uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali ya ngozi pia hutumika katika vipodozi vingi. Yanafanya kazi kwenye virusi, bakteria na fangasi pia
Matumizi:
Chukua pamba kidogo loweka kwenye maji
Chukua matone kama matatu mimina kwenye pamba iliyoloa.
Paka kwa kuzungusha kwenye sehemu husika
Endelea kufanya hivi kila siku kwa siku 10 huku ukiangalia matokeo
2. Tumia Oregano Oil
Haya mafuta yanatajwa kuwa na uwezo wa kuua bakteria, kuzuia hali ya mzio (anti inflammatory properties) kwenye ngozi, kuzuia kuchakaa au kuzeeka kwa seli za ngozi pia yanatajwa kuwa na uwezo wa kutatua tatizo hili kwa haraka.
Matumizi:
chukua matone matatu ya oregano na changanya na mafuta ya nazi matone matano
Paka mchanganyiko wa mafuta haya sehemu iliyoathirika
Usitumie karibu na macho tafadhali
3.Tumia Castor Oil ( mafuta ya nyonyo) na Baking Soda
Mafuta ya nyonyo yanatumika katika kuondoa madoa na vitu visivyotakiwa katika ngozi na kutoacha alama. Yanatajwa kuwa na virutubisho kwa ajili ya afya ya ngozi.
Matumizi
Chukua mafuta ya nyonyo kisha weka baking soda kutengeneza uji mzito (paste)
Paka sehemu yanye skin tag kisha funga na bandage
Unaweza kuweka mafuta ya ndimu au limao kupata matokeo mazuri zaidi.
Fanya hivi kwa mwezi au mpaka pale kitakapopotea
4. Apple Cider Vinegar
Apple cider vinegar imetajwa kwamba inaweza kusaidia kwa kuharibu "tissue" ya skin tag, hii inafaa kwa vile vilivyoota shingoni.
Matumizi
chukuapamba chovya kwenye siki ya matofaa ( Apple cider vinegar)
paka pale kilipoota kwa kusugu dakika 5
Fanya kwa mwezi mmoja huku ukiangalia mabadiliko
5. Ganda la ndizi
Matumizi:
weka kipande cha ganda la ndizi sehemu iliyoathirika hlf funga na bandage/plasta
Hakikisha kwa ndani ndio kunagusana na skin tag
lala na kipande cha ndizi mpk asubuhi
Fanya hivi mpk kitakapopotea
6. Juice ya kitunguu
Inasemekana kitunguu kina uwezo wa kusinyaisha (shrinking) hizi skin tags pia kina asili ya asidi.
Matumizi
chukua vipande vidogo vya kitunguu
Loweka vipande vya kitunguu katika maji
Chukua maji yaji ya kitunguu na chumvi kisha paka kwenye sehemu iliyoathirika
Lala na mchanganyiko huo mpk asubuhi kisha osha na maji vuguvugu asubuhi
Endelea kufanya hivi kwa wiki moja
7. Maji ya limao
Maji ya limao yana asidi pia yana uwezo wa kuua baadhi ya vimelea, inasemekana yana uwezo wa kuvimaliza hivi vijipele.Matumizi
Tumia pamba kupaka maji ya limao sehemu iliyoathirika
baki na maji ya limao mpaka yakaukie hapo
Fanya hivi kwa siku kadhaa hadi wiki huku ukiangalia mabadiliko
8. Aloe Vera Gel (ute wa mshubiri)
Aloevera (shubiri) inasifika katika kutatua matatizo mbalimbali ya ngozi pia inasemekana inaweza kuondoa skin tags. MatumiziPaka ute wa aloevera kwenye sehemu iliyoathirika.
9. Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu kinasikifika kwa uwezo wa kutibu matatizo mbalimbali yanayoletwa na fangasi hata bacteria inasemekana kina uwezo wa kukausha skin tags kwa kuwa kuna vichocheo (enzymes).
Matumizi
twanga kitunguu saumu upate uji mzito
paka moja kwa moja sehemu iliyoathirika kisha funga na plasta
Unaweza kufanya mara mbili kwa wiki
10. Tangawizi
Tangawizi ina sifa zinazofanana na kitunguu saumu, inaweza kutumika kupambana na seli za skin tags.
Matumizi
Twanga tangawizi kama ulivyofanya kwa kitunguu saumu.
unaweza kukata vipande vidogovidogo
Tumia ndani ya wiki mbili utaona mabadiliko
11. Vitamini E
Inasemekana mafuta yenye vitamini E yana uwezo wa kuondoa skin tags.
Paka mafuta ya vitamin E sehemu iliyoathirika.
Unahitaji kupaka kwa wiki moja hadi mbili
Unaweza kupata matokeo mazuri ukichanganya kitunguu saumu na mafute ya vitamini E
12. Nanasi
Nanasi linasikifika kuweza kupausha muonekano wa skin tags na kisha kufanya zipotee.
Matumizi
Paka maji ya nanasi sehemu iliyoathirika
Paka kwa siku 8 hadi 10, usifute au kuosha baada ya kupaka
13. Rangi ya kucha
Inasemekana rangi ya kucha ikipakwa sehemu iliyoathirika kwa muda skin tag inapotea.
Nunua rangi ya kucha nzuri, tumia uliyonayo kupaka sehemu iliyoathirika
Paka mara 2 hadi 3 kwa siku
Baada ya siku chache utagundua skin tags zinakauka na kuondoka zenyewe
Iwapo skin tags zipo sehemu za siri au karibu na jicho epuka kutumia rangi za kucha hapo.
14. Kufunga uzi
Hii mbinu ni ya siku nyingi ambapo unafunga mzizi na kukaza mpaka kinatoka, hapa unaweza kutumia barafu kuweka ganzi ili usisikie maumivu.
15.Nail clipper au tuiser
Kwa vifaa hivi unaweza kukata kuanzia kwenye mzizi na kukiondoa mahali pake, Angalia ambavyo ngozi yako inareact kwa kuondoa kimoja kwanza.
Hizo ndio njia zinazozungumziwa, kazi kuzijaribu tu.