Monday, January 15, 2018

HIZI NDIO SABABU KUMI ZINAZOKUFANYA UENDELEE KUISHIWA NGUVU ZA KIUME



                                                                        
Nguvu za kiume ni nini? Huu ni uwezo wa mwanaume kusimamaisha uume wake na kustahimili kwa mda mrefu wakati wa faragha bila wasiwasi wowote…
Kama nilivyoongelea kipindi cha nyuma wanaume wengi wanasumbuliwa na tatizo hili kadri miaka inavyozidi kusonga mbele.
Idadi kubwa ya watu wamaekua wakihangaika sana na kudanganywa na waganga wa kienyeji kwamba watapona kabisa.
Lakini kuna sababu kadhaa za kibinadamu ambazo uchunguzi wa kitaalamu unaonyesha zinasababisha tatizo hilo kama ifuatavyo…
·         Uvutaji wa sigara:
Hii ina kimelea cha kemikali kwa jina la nicotin ambacho huharibu mishipa ya damu na ile ya fahamu na kukufanya kua mlegevu kabisa wakati wa tendo la ndoa…
·         Ulevi uliopitiliza:
Unywaji wa pombe sana huharibu mishipa ya fahamu yote ya binadamu, ndio maana mtu akishalewa hata akiumia hasikii kwasababu kwa kipindi kile mishipa hiyo ya fahamu haifanyi kazi sawasawa.
·         Kutokufanya mazoezi:
Mwili untegemewa kua safi sana pale damu inapozunguka kila sehemu na kusafisha kila kitu ikiwemo na sumu za vyakula tunavyokula. Usafi huu hufanya mwili kua safi kila Nyanja ikiwemo na nguvu za kiume hivyo kama hufanyi mazoezi huwezi kupata faida hizi.
·         Uzito uliopitiliza:
Kwa jamii zetu za kiafrika kitambi ni kama sifa, lakini naomba nikwambie mtu mwenye kitambi ni mgonjwa na husumbuliwa sana na tatizo la nguvu za kiume kwani uzito alionao humchosha sana na kulala akiwa hoi.
·         Kufanya ngono mara kwa mara na upigaji wa punyeto:
Hamu ya kulala na mwanamke ni kama ulaji wa chakula, tunaamini mtu mwenye njaa kali ndio atakula sana. Hivyo ukifanya ngono na kupiga punyeto mara kwa mara hutakua na hamu ya ngono na nguvu za kiume hutaziona kabisa.
·         Maumivu makali ya mwili na mgandamizo wa mawazo:
tendo la ndoa ni la starehe hivyo linaenda vizuri mwili ukiwa safi kabisa bila shida yeyote . kama unasumbuliwa na maumivu ya mwili ya aina yeyote ile au maumivu ya kisaikolojia kama kuachwa, kufiwa au kukosa kazi basi hautakua na nguvu za kiume za kutosha.
·         Njaa wakati wa tendo la ndoa:
Najua watu wengi watashangazwa na hii pointi, lakini napenda ujue kwamba mwili wa binadamu unajua kutoa vipaumbele. Kama una njaa sana mwili hautahangaika na nguvu zako za kiume kwasababu kuna mambo mengi muhimu ya kufanyika kwenye ubongo.
·         Kulala na mwanamke mchafu na ambaye humpendi:
Naomba utambue kwamba nguvu za kiume si mwili tu, bali hata saikolojia..
Nguvu za kiume huambatana na mapenzi kutoka moyoni kwenda kwa mwanamke husika na usafi wake binafsi. Usitegemee kulala na mwanamke huku umeshika pua kuzuia harufu kali afu upate nguvu za kiume.
·         Ugomvi wa mara kwa mara na mwenza wako:
Kama mahusiano yako na mwenza wako yana matatizo kimsingi mtakua mnaingia faragha na vinyongo moyoni , hali hii hupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa na kuendelea kuishiwa nguvu za kiume.
·         Kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume hovyo:
Dawa za kuongeza nguvu za kiume kama Viagra zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya watu flani na humezwa chini ya usimamizi wa daktari. Wewe unayezimeza hovyo unakosa imani na nguvu zako kiasi kwamba ukizikosa dawa hizo hufanyi kitu kabisa.
Mwisho:  tafuta suluhisho ya tabia nilizozitaja hapo juu na nguvu zako za kiume za mwanzo zitarudi na utaishi kwa amani, usidanganyike na waganga wa kienyeji watamaliza pesa zako.