Friday, January 5, 2018

ABOUT LOVE: UTATA ! MKE WANGU ANANISHAURI NIMUOE RAFIKI YAKE! USHAURI WAKO PLEASE


Siku ya jumatatu hii iliyopita baada ya kupata chakula cha jioni na watoto kwenda kulala ndipo akanijia na hiyo"surprise" ambayo sitasahau maishani mwangu. Aliniambia kama ninaweza nimuoe tu huyo rafiki yake maana ana miaka takriban 34 sasa, na ni"bila bila"(kakosa mume).Kwa kuwa sisi watu wa mkoa wa Mara kimila tunaruhusiwa ata wake wanne, hivyo kumuweka ndani itakuwa nimempunguzia aibu ya kukosa mume huyo mwanamke waliyeshibana sana, sasa machale yamenicheza, naona kama wife ameshtukia "issue ya kuchepuka" sasa kanitega aniingize kingi.Najiuliza sijui ni mpe jibu gani wife aisee, naombeni busara wakuu wenzangu maanake naona kama "nimekamatika vile"