Friday, January 5, 2018

ABOUT LOVE; MBINU MPYA ZA WANAWAKE WA SIKU HIZI WANAO SAKA NDOA KWA NGUVU...NI NOMA SANA

Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi
anaondoka... 
Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka...
Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Hny nitunzie nimesahau hereni zangu mezani  
Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadha,na ole wako uvihamishealipoacha,kesi zinaanza...
Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza...Anahamia taratibu.. Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa
ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na 'Foundation'... My Brother,huna haja ya kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO....
Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my days',Zamaninilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku hizi kuna Missed days,ukiambiwa hivi tu ju imekula kwako, inawindwa ndoa...