Tuesday, December 26, 2017

Usifakamie Mapenzi Eti Unaondoa ‘STRESS’

KARIBU mpenzi msomaji wa XXLove tupeane elimu ya mapenzi ambayo tunaamini ‘yana-rani’ dunia. Wiki iliyopita tulizungumzia mpenzi ambaye akipendwa inakuwa ni karaha, akichuniwa pia inakuwa ni shida, sijui anataka afanyiwe nini?
Leo nitazungumzia baadhi ya watu kufanya faragha kuwa ni sehemu ya kuondoa ‘stresi’ (msongo).
Kama ulikuwa hujui, kwa taarifa yako hata faragha yenyewe haihitaji stresi, sasa unakuwa mtu wa ajabu unapofanya mapenzi kwa maana ya kuondoa stresi. Huwezi kufanya jambo hilo katika hali nzuri na kiwango kinachotakiwa kama utakuwa na stresi. Ndiyo maana wapenzi wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wapenzi wao hawawaridhishi wanapokuwa faragha.
Kuna kitu kinaitwa amani ya moyo. Kiukweli kama huna amani ya moyo ni vigumu kufurahia tendo unapokuwa faragha. Amani ni kila kitu, iwe kazini, shuleni, kwenye familia, kwenye nyumba za ibada, vyuoni na kwingineko.
Huwezi kufaulu mtihani vizuri katika masomo yako kama huna amani ya moyo. Ndivyo ilivyo kwenye uhusiano. Kama huna amani hiyo, huwezi kufanya mapenzi kwa raha na kutegemea kufurahia tendo hilo.
Nasema hayo kwa sababu badala ya kufikiria lile tendo, wewe unawaza madeni unayodaiwa. Unawaza ulivyochambwa na Ashura. Unawaza riba ya mkopo uliochukua. Unafikiria kesi uliyonayo mahakamani, kodi ya nyumba na mambo mengine kibao.
Wapo wengine wanaokurupuka na kufanya mapenzi wakati hawajala au wamekula ila hawajashiba. Hili ni tatizo. Huwezi kulifurahia penzi ukiwa na njaa wakati nguvu (calories) zinazotumika kwenye faragha huwa ni kubwa sana.
Kwa maana nyingine kutokujiandaa katika zoezi la faragha ni tatizo kubwa sana. Tendo hili halihitaji kukurupuka hovyo bila maandalizi ya kiakili na kimwili.
Kama kuna kitu kinachohitaji utulivu na muda, basi ni suala zima la faragha, wengi wamejisahau na kufanya faragha kitu cha kawaida, mtu akiwa na stresi zake anaamua kwenda kuzimalizia kwa kukutana faragha na mwenza wake. Huwezi kukutana kula tunda ukiwa na stresi.
katika hali ya kawaida huwezi kufanya mapenzi ukiwa na hasira, kazini umevurugwa, kwenye daladala umetukanana na konda, halafu unafika nyumbani unataka kukutana faragha na mwenzi wako. Hiyo haiwezekani kuwa faragha nzuri inayotakiwa. Kaa chini kwanza, pumzika, ondoa mawazo yote ya kazini na kwenye daladala. Weka kwanza kando deni la kodi ya nyumba na ada ya shule kisha fanya mambo yako, ukimaliza chukua mawazo na matatizo yako, endelea nayo.
Tukutane tena wiki ijayo kwenye mada nyingine nzuri, pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook kwa ushauri na maswali kuhusu elimu ya mapenzi.
-GPL