Monday, December 11, 2017

UPENDO NI NINI...........???????

 upendo ni nini
Neno hili (Upendo) sio kitu cha mchezo, wewe unaweza kuwa ni mtoto, mwanafunzi hujajipanga bado utaratibu wako wa maisha unatakiwa uwe makini sana katika jambo hili, unajua kuwa Upendo unauwezo mkubwa sana wa kutoa ufahamu wa mtu na kuharibu utaratibu wa mtu? 

Upendo unapoingia ndani ya moyo mtu anauwezo mkubwa wa kukutoa katika mipango yako, upendo ukikolea watu wanauwezo wa kusahau familia zao, masomo, kazi zao, na utaratibu wake wa kila siku unaharibika, upendo unatakiwa kuheshimika na kila mtu unatakiwa kutembea katika upendo kwa unyenyekevu mkubwa, utiifu na adabu maana sio jambo la mchezo, usichukulie jambo hili kitoto unatakiwa unapoamua kufanya maamuzi ya kupenda au kupendwa unatakiwa uwe na maswali (14) hayo ya msingi

Mambo ya msingi ya kujiuliza kuhusu upendo

1. Upendo ni mzuri sana kama utajua maana na kusudi la Mungu kuweka pendo ndani ya mtu.

2. Upendo unatesa

3. Upendo unaua

4. Upendo unakondesha

5. Upendo unaharibu maisha

6. Upendo unaharibu utaratibu wa mtu

7. Upendo unanyonga maisha

8. Upendo unaathiri akili ya mtu

9. Upendo ni gharama

10. Upendo ni shule

11. Upendo ni maisha ya mtu.


Kuna aina sita [6] za upendo


1. Philotheos - upendo wa mungu; (2timoth 3:4)

2. Philoxenos - kupenda wageni (xenia…..hospitality)

3. Philagathos - kupenda kitu kizuri; (titus 1:8)

4. Philarguros - kupenda pesa; (luke 16:14 and 2timoth 3:2)

5. Philautos - kumpenda mtu mmoja; (2timoth 3:2)

6. Philedonos - kupenda starehe; (2timoth 3:4)

Unajua ni vizuri sana kama utapenda mahali unapopendwa kuliko kupenda mahali usipopendwa, unatakiwa uwe na ufahamu mkubwa sana wa mapenzi kabla ya kuyaingia unaweza kupoteza ndoto zako za maisha, maaana mapenzi yanauwezo mkubwa sana wa kuharibu maisha yako. 

Mabinti wengi na vijana wamejikuta wameingia katika mchezo huu wa mapenzi wakiwa na akili za kitoto huku wakijua kuwa upendo ni kitu cha kawaida leo wanalia sana kutokana na maumivu waliyoyapata. 

Maswali Kumi na nne (14) ya kujiuliza kabla ya kuchukua uamuzi wa kupenda au kupendwa

1. Kwa nini ninapenda?

2. Upendo ni nini?

3. Je huyu anayenipenda anajua maana ya kupenda?

4. Je amenipendea nini?

5. Je ana malengo gani juu ya maisha yangu?

6. Amejipanga vipi juu ya makwazo yatakavyo jitokeza baadaye?

7. Je amenipenda love au ananitamani LIKE?

8. Je ana ujasili wa kukabiliana na mazito mbeleni katika maisha?

9. Je yupo tayari kunishika, kuniongoza, kunishauri, kunifundisha nisiyoyajua, atakuwa na muda na mimi na ataniombea?

10. Je ataheshimu mawazo yangu na hisia zangu?

11. Je ni mcha Mungu? Na anamuelekeo juu ya MUNGU?

12. Je historia yake ikoje na ametoka wapi?

13. Je kuna mipaka ipi katika upendo wetu?

14. Je ameathika kweli juu yangu?


Kwa nini tunapenda na tunapendwa?

Hakuna anayependa bila sababu na hakuna anayependwa bila sababu zinazomfanya.Mtu kupenda au kutopenda hata Mungu alikuwa na sababu za kuupenda ulimwengu hata Kumtoa mwana wa pekee ulumwenguni. Kupenda sio dhambi na kutopenda sio dhambi.

Upendo ni sehemu ya maisha na ni Mungu ambaye ameweka kwa mwanadamu Hivyo.

Upendo umetoka kwa Mungu sio mtu ameamua kupenda jua kuwa upendo ni sehemu ya maisha hata wanyama wanapenda na wana wivu wao kwa wao lakini upendo wa mwanadamu ni kubwa na unanguvu kuliko wanyama.

Sababu kwanini Unapenda na kwanini Unapendwa na ninani Unatakiwa kumpenda

(1) Kwa sababu naitaji kufarijiwa 

(2) Kwa sababu naitaji kukamilishwa [mwanzo 2;18-]

(3) Kwa sababu upendo ni nature

(4) Kwa sababu ni mpango wa Mungu

(5) Kwa sababu nahitaji kupendwa.