Saturday, December 30, 2017
NAMNA YA KUPATA MPENZI (UA LAKO LA MOYO)...SOMA HAPA KUFAHAMU NJIA..
Jambo la msingi unalopaswa kujua ni kwamba, unapoamua kumtafuta mpenzi wa kweli, lazima utakutana na hali ya kukataliwa kwa mara kadhaa, yani wote mkiwa wakataaji na wakataliwa (yupo utakaye mkataa na yupo atakayekukataa).
Watu wengine wanapokumbana na hali hii, hujikuta wakiwa ni wenye hasira, mawazo, aibu na kukata tamaa ya kuendelea kutongoza.Watu wengine hutafuta mtu mwingine haraka haraka ili kuziba nafasi ya kukataliwa, lakini wengine pia hushindwa kujizuia kurudia kuwakatalia watu wawili watatu, hivyo huamua tu kumkubalia mwanamke au mwanaume anapokuwa akimtongoza, hivyo kujikuta amedumbukia katika penzi lisilo na afya.
Unapokataliwa na watu kadhaa, usilichukulie swala hilo kuwa ni swala zito saaana, kwani watu wengine wanaweza kuwa wanaamua tu, kukukatalia kwa sababu za kijuu juu tu, zisizo na maana yoyote. Kwa mfano uoga, aibu n.k.Unapaswa kutulia na kutojutia kwa tendo hilo, bali changamoto kama hizi hukupatia uzoefu uzoefu katika mahusiano yenye afya.
Weka mambo katika mtazamo, usiweke asilimia kubwa ya muda wako katika kutengeneza mahusiano, bali jikite katika shughuli zinazokufanya upate furaha. Kama vile kufanya kazi zako, kuwa mwenye afya, kuwa na mahusiano mazuri na familia yako pamoja na marafiki. Utakapojikita katika kulinda furaha yako, maisha yako yatakuwa sawa na utaonekana kuwa na mvuto kwa watu wengine na hasa pale utakapokutana na mtu Special kwako.
Kumbuka kwamba hisia za mwanzo mara nyingi huwa sio zakuaminika, hasa unapokuja katika swala la kutongozana katika mitandao mbali mbali ya Internet, watu huwa hawaweki uhalisia wao mbele, bila kujali mmekutana wapi, lini, kivipi, chamsingi kabla ya kuwa karibu sana na mtu, nivyema ukawa naye katika hali mbali mbali kama vile, wakati wa shida na raha. Kwamfano utampima mtujinsi alivyokuchukulia wakati wa matatizo na wakati wa raha.
Kuwa mkweli na muwazi, jivunie ulichonacho, usitake mtu akupende kwa ndoto zako au matarajio kuwa mtu flani baadaye. Kwamfano unamwambia mpenzi wako kuwa baada ya mwaka moja nitanunua gari, au nitapata kazi au nitakuwa msanii. Inapaswa kupendwa vile ulivyo kwa wakati huo.
Kikubwa zaidi, wekeza kwanza katika mahusiano imara na sio kukimbilia kufanya mapenzi. Japokuwa katika zama hizi za kizazi cha sasa ni vigumu mtu kuchukua muda wa kumfahamu mtu kwanza. Unapaswa kuwa na mtu kwa takribani muda kadhaa ili mfahamu kama mnaendana kitabia au lah!.