Friday, December 1, 2017

NAJUTA! NAJUTA KUPENDA, NA NASIKITIKA KWA USALITI ALIONIFANYIA MPENZI WANGU"

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24,Mpare, Mkristo na nina boyfriend wangu mwenye umri wa miaka 30,Mkinga,Mkristo.Tumekuwa wapenzi kwa muda wa miaka mitatu (3).Lakini toka Christmas mwaka jana tumekuwa na migongano katika mapenzi yetu, yeye amepanga chumba kimoja, kwakuwa tulikuwa tunapenda sana nilikuwa huru kwenda kwake muda wowote ule, na funguo ninazo,

kazi zake yeye sometimes anaingia shift ya usiku kwa hiyo unakuta mimi nikienda anakuwa hayupo, au tunapishana, lakini mara nyingi tulikuwa tukionana nae juma mosi na juma pili.

siku zinavyozidi kwenda ndio akawa anazidi kubadilika, hana furaha na mimi hata nikienda kwake, hapo anapoka kuna mama wa makamo, ambae ndie mama mwenye nyumba,ambae ametokea kunipenda, na huwa ananishauri nimwambie boyfriend wangu kama kweli ananipenda basi anitambulishe kwa kwao,

wakati ndio tunaanza urafiki mimi na yeye, hakuwa na kazi yeyote ile, alikua akiishi na kaka yake, ila hali sikuipenda, mimi nilijitahidi nikamtafutia kazi ambayo ndio anaifanya hadi sasa, na badae kumsihi ahame akae kwake,

lakini yote hayo mchumba wangu huyu hakuwa ameyaona, siku moja aliingiza msichana mmoja ambae ni BARMAID(mfanyakazi wa baa) akalala nae, asubh wakati yle dada anatoka akakutana na mama mwenye nyumba, yule dada alistuka na kurudi ndani, yulekwakuwa ananipenda, siku nilipoamua kwenda kwa ajili ya kumfanyia mpenzi wangu usafi, yule mama aliniita na kunieleza lile tukio, nililia sana, niliumia na niliondoka bila kuuliza

lakini nilishindwa kuvumilia kabisa, usiku nikapiga simu kwa boyfrienda wangu ana kumuuliza, akakataa akasema sio mpenzi wake isipokuwa alikwenda kufata pesa yake, sikumuamni, toka pale mapenzi yangu kwake yakawa yamepungua sana,


Christmas 2009, ilikuwa ni majira ya usiku nilipigiwa simu na mtu ambae simjui, ilikuwa ni sauti ya mwanamke aliyenitolea maneno machafu na kuniambia tutabanana hapo hapo,haijalishi mimi na huyu mpenzi wangu tunamahusiano kwa muda gani ila kama nitakuwa nae mchana basi na yeye zamu yake ni usiku.Nilihisi maini yananitoka,kwanza nikajiuliza ni yule dada barmaid ameamua kunitusi hivyo au ni mtu mwingine tu katumwa??


Kumbe ni dada mwingine tena, ambae nae pia ni barmaid!, nliishiwa nguvu na kujiona nipo utupu kwani yule dada alinieleza kila nilichokuwa nafanyana na mpenzi wangu ikionyesha kuwa alikuwa pia ni mpenzi wake.Hadi mara ya mwisho tulipoenda kumsalimu wifi yangu yule dada alikuwa anajua kila kilichokuwa kinaendelea.Na matusi mengine ya kashfa kama"Wewe unanuka,unajipendekeza kwa ndugu zake, mwenyewe anasema hana muda na wewe, ameshanipata mimi ninamridhisha, hujui mapenzi mshamba tu!na isitoshe hapa nilipo ameshanivalisha pete na ni mjamzito.Akidai kuwa mimba yake ina miezi miwili.


Nilichanganyikiwa wala sikulala, nikaamua kumpigia simu boyfriend wangu tena kujuwa kama ni kweli, matokeo yake simu ilipokelewa na yule mwanamke na kunijibu kwa jeuri, Anti!mbona lakini unakuwa sio muelewa?naomba uniachie mpenzi wangu na hatutaki usumbufu saizi, hapa tulipo tunajazia VIUNGO vya mtoto wetu, kama MIGUU na VIDOLE"


nililia sana, hadi mama yangu alishtuka na kuja kunigongea, niliogopa kumueleza mama ukweli kwakuwa ana pressure, hivyo nilidanganya kuwa nimeota nimepata ajali, basi mama aliniombea na kwenda kulala,
toka pale nikaamua kumsahau, nakuanza maisha mapya, nilichokifanya ni kwenda kupima afya yangu tu!
na nikaamua kuendelea na masomo yangu tu!,


baada ya muda akaanza kunisumbua tena ili turudiane, nilliona kero nikabadili namba ya simu, lakini aliitafuta kwa marafiki zangu na kuendelea kunisumbua kwamba turudiane nae,


Nipo kwenye mawazo sana, kwakuwa nilimpenda sana huyu kaka, na mafanikio yake mengi yametokana na juhudi zangu, amenitenda yasiyostahili, sasa hivi ndio anataka nimrudie tena, naombeni mnishauri maana sijui hadi sasa nifanye nini.