MAPENZI: Wanaume Wengi Hawajui Faida za Kuwa Na Uhusiano na Wasichana Wenye Tabia Za Kiume (Tomboy)
Tomboy ni nani? Tomboy ni mwanamke anaependa sana mambo ya kiume, wengine wanawaita majike dume, kitu kimoja ambacho wanaume wengi hawajui sio kila mwanamke anaependa kujitupia pamba za kiume au anapenda kufanya mambo Fulani ya kiume ni msagaji. Wapo ambao wameamua kufanya hiyo staili yao ya maisha, wapo ambao wanajiona wabaya na wanadhani hawawezi kupendwa na mwanaume yoyote, wapo ambao waliumizwa kwenye mapenzi na wanajaribu kujiweka kiume ili wasipate tena wapenzi.
Hawa mnaowaita madume jike pia ni wanawake na wanahisia kama wanawake wengine, wanapenda kama wanawake wengine ila kwa sababu wanajiweka kama wanaume inakuwa vigumu kumtamkia mwanamme kama wanampenda na kutokujiamini, wengine wanajiona sio wanawake kamili. Na nina amini wanaume wanamchango mkubwa kuwabadilisha wanawake wa aina hii kuwa kama wanawake wengine bila kutumia nguvu. Kuna faida kadhaa kutoka na mwanamke wa aina hii.
Sio Mwanamke wa kioo kila mara;
Wanawake wa aina hii hawapendi kujiremba sana, kwahiyo hutoboreka wakati wa kutoka nae akipiga tshirt na jeans maisha yanaenda, hatokusumbua kutengeneza nywele wengi wao wanapenda kukata nywele au kuweka dreads hautokuwa na gharama za kumpeleka saluni.Sio wanawake wa kupandika kucha wala kope wanaweka kila kitu simple.
Hutomkuta kwenye Vigenge vya Umbea;
Wanawake wa aina hii huwa hawana marafiki wengi wa kike, hawapendi umbea umbea na kupiga soga kijinga, kwahiyo hawezi kuwa na mashoga wa kijinga wanao shauriana ujinga na mambo yasiyo ya maana.
Waaminifu;
Sio wanawake wanaofwatwa na wanaume wengi,kwahiyo mwanaume ambae atajitokeza kwake na kumpenda huwa anampa mapenzi yake yote na kama unajua mapenzi na kumjali na kumuonyesha mapenzi ya dhati kabisa basi utashangaa,wanawake wa aina hii ni wepesi kubadilika na kuwa kama wanawake wengine watavaa nguo za kike na kuwa kama wanawake wengine ili uzidi kuvutiwa nao.
Mtafanya Mambo mengi pamoja;
kwa kuwa anapenda mambo mengi ya kiume mtajikuta mnaangalia mpira pamoja mnacheza game za Tv pamoja na kunywa mkitoka pamoja na washikaji na hii itawafanya muwe wapenzi ambao pia ni marafiki, kitu ambacho wapenzi wengi hawana. Kuwa na mpenzi ambae pia unaweza kumchukulia kama rafiki ni kitu kinachowafanya wapenzi muwe kama mapacha inaongeza chachu ya mapenzi yenu.
Hawana Drama za kijinga;
Wanawake wa aina hii, hawapendi drama nadhani mnawajua Drama Queen hao ni wanawake wanapenda kufeki mambo, kitu kidogo wanajidai kupanick, kujizimisha na kujitia presha lakini Tomboy ukifanya kitu atakuambia na hawajui kuigiza wako real, na ni wanawake waelewa kuliko wanawake wengine wanaojivalia kidada.