Monday, December 4, 2017

Mambo Muhimu 11 Unayopaswa Kumwambia Mpenzi Wako Kila Siku.

Kutengeneza uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye changamoto kubwa. Japo hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na rahisi ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako yakaujenga zaidi. Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa couple itakayowapa wivu marafiki zetu.
1. Nakupenda
Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.
2.Nilikuwa nakuwaza
Ni muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3. Siku yako ilikuaje?
Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa pamoja.
4. Nakuunga mkono
Mpe moyo mpenzi wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingine upande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe couple tu, kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha uhusiano wenu.
5.Umependeza
Picha na OGS Studio
Kama umekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mpenzi wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ‘gauni hilo limekupendeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.
6. Samahani
Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye uhusiano wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mpenzi wako. Omba msamaha hata kwa vitu ambavyo sio kosa lako.
7. Hakuna kama wewe
Mpenzi wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi hamkupaswa kuwa kwenye uhusiano. Mfanye mpenzi wako ajue kuwa yeye ni bora na hakuna kama yeye.
8. Napenda mawazo yako
Mwambie mpenzi wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona ana akili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.
9.Nakuheshimu
Kama ulivyo uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu kwako na mpenzi wako. Mpe nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye mambo yanayokutatiza. Mtu anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha na salama, vitu ambavyo ni muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.
10. Napingana na hilo
Sehemu moja wapo ya kumheshimu mpenzi wako ni kumjulisha pale usipokubaliana naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu anayekubaliana na kila kitu na hakuna mwanamke anayetaka kuzaa watoto na mwanaume asiye na msimamo. Mnaweza kuwa timu, lakini nguvu ya timu yoyote ipo kwenye mawazo na matendo ya kila mmoja. Kuwa na maoni yako na yaseme kwa mtindo wa heshima. Kumpa mpenzi wako mtazamo tofauti kunaweza kumsaidia kupata suluhisho kwa tatizo ambalo hakuwa ameliwaza.
11. Usiku mwema
Tunaishi kwenye wakati ambapo mawasiliano ni rahisi mno. Kwa kubonyeza tu kitufe tunaweza kutuma ujumbe kuvuka bahari, hivyo hakuna kisingizio cha kushindwa kusema ‘usiku’ mwema.
Haimjulishi mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia inamjulisha kuwa unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa kama mmejibizana, maliza siku na kishindo chanya.