Friday, December 1, 2017

KWA UPUUZI HUU MADADA WA KAZI WATAENDELEA KUVUNJA NDOA ZA WATU ,MPAKA AKILI ZIWARUDI

Kila siku na kila mahala ukipita au ukibahatika tu kukutana na akina Dada na akina Mama waliopo katika Ndoa au hata Mahusiano tu ' lawama ' zao kubwa ni kwa hawa Dada zetu wa Kazi nyumbani maarufu kama ' mabeki tatu ' kuwa wanashiriki kwa kiasi kikubwa sana katika kuwaharibia ' mahusiano ' yao kwa ' kubanduana ' na Wapendwa wao hasa Wachumba au Waume zao.

Kinachonisikitisha na hata kunishangaza pia ni Kitendo cha hawa hawa Dada / Mama zetu wao kuelekeza tu ' lawama ' zao kwa ' mahausigeli ' pasipo hata wao wenyewe ' kujitathmini ' ni wapi huwa wanakosea kwani ' kimantiki ' haiwezekani Mahusiano yao au Ndoa zao ziharibiwe bila sababu ' maalum '.
Katika chunguza chunguza yangu ya ' kutukuka ' kabisa ya kutaka kujua labda ' tatizo ' ni nini niliamua kulifuatilia ' kiumakini ' mno hili jambo na nikagundua mambo kadhaa ya ' kipuuzi ' ambayo Dada zetu walio katika Mahusiano au Mama zetu walio katika Ndoa zao huyafanya ambayo kwa kiasi kikubwa Mimi binafsi nawasapoti 100% ' mahausigeli ' kwani wanatumia ' upopoma wa kutukuka ' unaofanywa na hawa wenye Wachumba / Waume zao.

Mambo yenyewe ya ' kipuuzi ' ni kama yafuatayo:

1.Mama / Dada anaenda kuajiri ' hausigeli ' mzuri kuliko hata yeye tena kwa kila kitu.

2.Mama / Dada anaruhusu ' ukaribu ' wa ' kupitiliza ' wa Baba / Mchumba na ' Hausigeli '.

3.Mama / Dada anamruhusu ' Hausigeli ' kuvaa ' vimini ' mbele ya Baba / Mchumba.

4.Mama / Dada anaruhusu ' Hausigeli ' amfulie ' Nguo ' Baba / Mchumba.

5.Mama / Dada anaruhusu ' Hausigeli ' awe na mazoea ya kuingia ' Master Bedroom '.

6.Mama / Dada anaruhusu ' Hausigeli ' aandae ' Chakula ' cha Baba / Mchumba huku yeye akiwa ' busy ' anatizama ' Isidingo ' na ' akitiririka ' na WhatsApp.

7.Mama / Dada anajifanya kuiga mambo ya ' kizungu ' kwa kuonyesha ' manjonjo ' yake ya ' Kimahaba ' tena mbele ya ' Hausigeli ' kitu ambacho huwafanya ' Mahausigeli ' wengi kuweza kuangalia ' udhaifu ' wao na pale Wao wakija ' kutongozwa ' tu akina Baba / Wachumba huwa hawakatai na ikifika wakati wa ' kubanduana ' huyu ' Hausigeli ' atamfanyia Baba / Mchumba ' manjonjo ' yake yote hivyo kumfanya kuonekana bora zaidi na hapo ndipo mwisho wa ' mahaba niue ' kwa akina Dada / Mama na kubaki kulaumu tu na kulialia.