Monday, December 25, 2017

Kukataliwa na Mpenzi Wako Kunaweza Kuwa na Madhara Kwenye Uhusiano Wako wa Baadaye.

2FED2E4700000578-3390809-image-a-25_1452280702575
Watu hubeba mzigo mzito baada ya kukataliwa pale wanapochukulia kama ni kitu kinachowaonesha namna walivyo kama watu, watafiti wamebaini.
Wanasema hisia hizo hasi zinaweza kuwa mzigo kiasi cha kuweza kuharibu uhusiano wa baadaye. Huzuni ya kukataliwa inaweza kukaa kwa miaka na kusababisha matatizo, wamebaini.
Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Stanford.
“Hali ya kuachwa na mtu uliyedhani anakupenda kisha wakabidilisha mawazo, kunaweza kuwa tishia kwa kwako na kunaweza kuwafanya watu wahoji wewe ni mtu wa aina gani,” alisema Lauren Howe, daktari wa saiokolojia kwenye chuo hicho