Wednesday, December 27, 2017

HIKI NDICHO KITU ANACHOKIPENDA MWANAMKE KULIKO VYOTE DUNIANI.

Haya hii ya leo ngoja niwatobolee siri kidogo tu kwenye upande wa mapenzi. unajua wanawake bwana tupo kama mayai ukiyaminya kidogo tu huwa yanapasuka.. sasa wengi wanaume huwa wanabaki kuropoa “wanawake hawaeleweki” WANATAKA TUWEJE? Mwanamke huwa anapenda sana kuambiwa ukweli japo wengi wanadai eti bila kudanganywa hatuingiliki, Wanawake wengi hupenda kuspend muda wake zaidi na wake mpenziuliko na marafiki zake. Mwanamke hupenda mwanaume anaejali zaidi kuliko mbabaishaji “sasa wewe jifanye gogo tuone kama utapata mrembo” Jeuri ufanyiapo mwanamke dhahir huwa unamvunja moyo na hukushusha thamani yako pindi umfanyiayo yakawa yale yanayo mdharaulisha zaidi Mthamini mpenzi wako hata ukiwa na watu wengi, onyesha unajali kuwa nae karibu, hujiona wa pekee Mwanamke hupenda kusikilizwa japokuwa wanaume hujifanya vichwa na kutuona hatuna la kuongea lakini sio kweli ni fikra zenu tu. Msikilize mpenzi wako uone kama na wewehatokusikiliza Mwanamke huthamini sana msg za mpenzi wake kuliko simu apigiwayo na mwenza wake, maana kuona faraja zaidi pindi asomapo msg hizo zaidi ya kupoteza muda kusubiri apigiwe au akupigie. Msifie mkeo ama mchumba wako pindi apendezapo na kumpa faraja pindi aumizwapo. Msikilize mchumba wako na usitumie lugha ya ukali akuombapo ushauri bali jaribu kuchunguza zaidi nini atakacho kwako. Kila lililo dogo usilikuze bali lipe nafasi yake katika kutoa kipingamizi ama makubaliano.lasivyo utasababisha kutokujiamini.Onyesha unajali Mkumbuke kila wakati hata mara2 kwa siku Punguza jeuri na kauli chafu ukifananya kati ya hayo hutopata misukosuko mingi na kumbuka kujishusha endapo ufanyapo kosa na acha kutumia mabavu zaidi kuliko upole. haya jamani ni hayo tu labda utaona umuhimu wa mwenza wako zaidi ya kuliko kutoa lawama juu yake, wapendwa kama hamtojali kama kuna ambayo wakina kaka nao wanataka kutoa kero zao uwanja wenu.