Saturday, December 9, 2017

DALILI TISA ZINAZOMSHAWISHI NA KUMPA RAHA MWANAMKE KUFANYA MAPENZI

 
MPENZI msomaji wangu wa safu nalazimika kukuletea mfululizo wa safu hii kutokana na maombi ya wadau mbalimbali hasa wasomaji wa safu hii au mambo haya na wale wachangiaji katika mitandao mbalimbali ukiwemo mtandao wa MABADILIKO ambako pia mimi ni mmoja wao na ninaamini kuna kisima cha mawazo endelevu na somo hili la mahusiano tunaendelea nalo.

Nawashukuru wote tulioweza kuwasiliana mkipongeza safu hii kupitia simu zenu za viganjani na baadhi tukishauriana ili kuweka sawa na kusuluhisha baadhi ya migogoro ya kimahusiano ambapo leo kama nilivyowaahidi kuwa tutazitazama dalili za mwanamke anapotaka ngono.

Kwaza kabisa nikujulishe kuwa kitaalam mwanaume huwa anawaza ngono kila baada ya sekunde sita huku akiwa za mahala pa kufanyia tendo hilo wakati mwanamke huwaza ngono kila baada ya sekunde tisa na akikubali kuvua nguo ni lazima awe na sababu za msingi.

‘’Mimi sijisikii kufanya mapenzi’’ hii ni moja kati ya kauli ambazo wanaume huambiwa na ukisikia hivyo ujue si peke yako unayeambiwa hivyo na hii ni kauli inayolalamikiwa sana na wanaume wengi ambapo baadhi yao wamediriki hata kuchepuka wakidhani wenzi wao wamewachoka, hapana, bali mwanamke kuna wakati anatamani kufanya tendo hilo na makala haya inakufungua.

Wanawake wanapagawa na huhitaji kufanya mapenzi kuliko wanaume wengi wanavyodhani na ukijua mazingira hayo walai hautamwacha mwanamke wako naye hatatamani mwingine kwasababu wanawake wanajieleza wazi kuwa katika mazingira nitakayoyataja hapa chini yakifuatwa wanajisikia raha mno…

1.      Mfurahishe

Hali yeyote ya furaha kupita kiasi inamfanya mwanamke kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufanya mapenzi bila kizuizi chochote.

2.     Baada ya kuzozana
Kugombana ninakozungumzia hapa ni kule kwa pande mbili mnakwazana na baadaye kila upande ukatoa dukuduku zake hata kama kwa kufikishana kwa wakubwa kwa nia ya kupata muhafaka na baada ya hapo hakuna kitu kizuri cha kubadilisha upepo huo zaidi ya kukumbatiana, kubusiana kwa huba huku mkiziamsha hisia zenu.

Ukiona hata kama mwanamke wako analia au ameghafirika kwelikweli, mwache anyamaze au mnyamazishe huku ukimbembeleza hata kumfuta machozi kisha …….hapo tatizo linaisha na wakati huo wote kwa pamoja mtafurahia tendo hilo.

3.     Siku ya 14 (Heat Period)
Wataalam husema kuwa hiki ni kipindi cha joto kwa mwanamke, ni kipindi cha aina yake katika mahusiano ambapo mwanamke anakuwa na hisia nyingi wakati mayai yanapotungwa. Hivyo zikiwa zimepita wiki tatu baada ya kumaliza Afya yake ya ‘’uchinjaji kisha damu kukauka’’ wakati huu ni muhafaka kufanya mapenzi na hata kama mwanaume ni mbishi kiasi gani au umechoka mwanamke atakuamsha na kukutega na mara nyingine atakueleza kuwa anataka.

4.     Mapenzi ya Mbali.
Mapenzi ya mbali yanaweza kuwafanya mkawa na maisha yasiyokuwa na migogoro ya mara kwa mara huku kila mmoja akiwa anamtamani mwenzake huku kitu pekee kwa wakati huu wa utandawazi kinachoweza kuwaunganisha zaidi ni simu na internet.

Mkikutana siku hiyo kila mmoja anamtamani mwenzake na kama ni asubuhi mtaona siku haiendi haraka hasa kwa wale wenye familia na kama mtakuwa wawili katika chumba ama nyumba hiyo aaaaaaahhhhh hiyo niwape hongera kwasababu hamtakawia hata sebuleni.

5.     Wivu
Ninachozungumzia hapa si ule wivu wa kijinga bali nazungumzia wivu wa mwanamke anayejitambua na kujiamini kuwa anamtii, kumnyenyekea na kumshauri kwa hekima mwanaume wake lakini anapata wivu anapoona mwanaume huyo yupo na mwanamke mwingine hata kama si katika mahusiano. Si unajua kila mtu ana moyo wa nyama? Hasa ukipenda, weeeeeee acha tu!

Mwanamke anapoona mwanaume wake ananyemelewa na mwanamke mwingine na kumshawishi kimapenzi huona wivu sana na wanawake wanaojitambua badala ya kufoka huamua kuwaonyeshea wanaume wao kitandani kwa kuwapa mapenzi motomoto huku wakionyesha stahili na kuonyesha kujiamini kuwa ni wazuri kila upande yaani sura, maumbile na hata kitandani kuliko wale wanaomnyemelea.

Hapa siruhusu wanaume kuwa vicheche ama kuambatana na wanawake wengine bila sababu eti tu unataka mwanamke wako akuonee wivu hapana hii ni mbinu ya kuotea maana kumrusha roho mtoto wa mwanaume mwenzako si vema.

6.     Mwanamke kujinyima
Kadri mwanamke anavyozidi kukaa muda mrefu bila kufanya usodoma na ugomora, ndivyo anazidi kupata ashki ‘’Nyege’’ na mwanaume unapompata mwanamke aliyekaa muda mrefu hakika utafaidi na yeye pia atakuweka kwenye historia maana atajisikia raha sana baada ya tendo hilo.

Na mwanamke wa namna hii haitoshi kuwa mmefanya tendo la ndoa siku moja huyu atahitaji walau siku mbili vinginevyo ukimwacha atachepuka ingawa ni wachache wanaoamua kufa kisabuni na kuamua kutumia maji ya moto kujikanda.

7.     Mawazo
Mwanamke ambaye amekuwa na mawazo kwa muda mrefu akihitaji faraja na akakosa hatimaye Mungu na malaika wake wakamwangazia nuru na kujikuta mikononi mwa mwanaume anayeweza kumpa mapenzi yatakayomfariji hakika mwanamke hufurahia tendo hilo ambalo anahisi linakata kiu yake na kushusha pumzi.

8.     Mbunifu wa Mazingira
Wanaume wengi wanawanyima uhuru wa mazingira wanawake zao huku wakihoji ‘’ameyapata wapi haya’’ nakushindwa kujua kuwa huo ni moja ya mtego wa kutaka mapenzi.

Mwanamke anaweza kukutaka mfanye mapenzi jikoni, bafuni, sebuleni kwenye kiti au popote pale na kama amekupagawisha vizuri katika penzi la jikoni kuna siku mnaweza kujikuta mkiacha chakula kikiungulia huku nyie mkiwa mnatoa jasho la Afya na hapo mwanamke atafurahi kwasababu mtego wake wa kwale haujanasa chui.

9.     Muziki na Kinywaji
Kucheza muziki na wengine wale ambao wanapata kidogo kinywaji ni moja ya mambo ambayo yanasisimua mwili na kuamsha hisia za mahaba kwa mwanamke.

Hapa kwa mwanaume unaweza kumchukua mwanamke wako na kwenda naye kwenye kumbi za Muziki kwa Sumbawanga wakati ule sijui kwa sasa kulikuwa na ukumbi wa Upendo View, Mbeya zipo nyingi ikiwemo Mbeya Carnival, Pamodz wakati Dar es Salaam kumbi ni bwerere. Wakati mnacheza jaribu kugusana ama kupapasana taratibu hapo mwanamke yeyote mradi akikubali kupapaswa, mambo yanakuwa si mambo.