Sunday, November 12, 2017

SIFA 7 ZA MWANAMKE ANAEFAA KUWA MKE WA KUOA

1.HANA TAMAA ZA PESA
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yeye, huyu ni ‘wife material’.
2.HAYUKO TAYARI KUKUONA HUNA AMANI
Mwanamke ambaye unaona kabisa unapokuwa na matatizo anaumia, anahaha kuhakikisha anakurudisha kwenye hali ya kawaida, huyo anafaa kuwa mkeo
3.ANAPENDA WATOTO
Utajuaje kama ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo.Tazama pia saikolojia na malezi ya watoto
4.HESHIMA KWA KILA MTU
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia.
5.ANAJISHUSHA
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa. Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, na wewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia.
6.ANAKUONGOZA KWENYE MEMA
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya.
Kwa mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo.
7.ANAJUA MAISHA NA MAPENZI
Mapenzi yanachukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo mwanamke anayekufaa wewe ni yule ambaye anayajua mapenzi vilivyo lakini pia anajua maisha. Kama yeye ni mtaalam wa majamboz tu lakini linapokuja suala la mambo ya kimaendeleo hayumo, huyo hafai. Pia akiwa yeye ni mtu wa mambo ya kimaendeleo tu lakini linapokuja suala la mapenzi ni sifuri, pia hakufai.Endelea kusoma kila siku maishahalisi blog ili kupata vitu vizuri zaidi vya kuboresha maisha yako