Saturday, November 25, 2017

NAOMBA SHAURI, MPENZI WANGU AMEBADILIKA.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30, nina mpenzi wangu wa muda mrefu toka 2014 japo mapenzi yetu yamekuwa hayana muendelezo muzuri kutokana na tabia za huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano yetu vizuri sana baadae mwenzangu alibadilika ghafla, nikaja kugundua alikuwa na mahusiano na wanaume wengine (zaidi ya mmoja) tukawa tumepotezana kwa mda kidogo coz alikuwa hapokei simu wala kujib text zangu alafu akawa ni mtu wa kusafiri sana kumbe alikuwa anasafiri na hao mabwana zake, siku nimekutana nae nilimuona na dalili za mimba roho iliniuma sana, mwanzoni alidanganya baadae akakubali akawa ametoa hiyo mimba akaomaba nimsamehe kwa sababu nampenda sana tena sana nikawa nmemsamehe.

Tukawa pamoja kwa mda mfupi baadae alianza tabia yake ya kuruka ruka na starehe kwa sana, niliamua kumuacha japo roho ilikuwa inaniuma alafu yeye hata hajali kila kitu kwake poa tu. Baadae alirudi akaanza kunitafuta akaomba msamaha kama kawaida yake, kupenda ni hatari sana jamani nilimsamehe tukaanza kuwa pamoja, alikaa kwangu kwa muda wa week, nikaanza michakato kwenda kutoa posa na mahari kwao.

Sasa alivyorudi nyumbani kwao akaanza tena unaweza mpgia simu anakuambia sipo nyumbani nipo kwa dada angu fulani, au kwa bibi nitarudi kesho, au nipo hospitali bibi anaumwa baadae simu inapotea hewani hata siku mbili akipatika anakuambia huku kijijini simu ilizima charge. Sasa kilichonichosha zaidi sasahivi hana hata hamu ya mapenzi kabisa tofauti na navyomjua mimi, huyu mpenzi wangu hapo awali alikuwa akiniona tu hutumii nguvu nyingi kumuandaa, lakini sasa hivi hata ukifanyeje hawezi kuwa tiyari hadi umpake mafuta kidogo. na unaweza kumuomba hata mwezi nzima anakuambia sijisikii, sina hamu.

Naomba ushauri wadau, nifanje ili aweze thamini hisia zangu, au hata kama nikimuacha nifanyeje coz nampenda sana huyu dada natamani awe mke wangu wa ndoa, kuna vitu huwa vinanifanya nimpende sana ni rafiki, mnataniana na kucheka, mpole ila sasa ndo hayo mambo yake, nilishajaribu kumuacha nashindwa nafuta namba kila kitu ila akinipigia tu au nikumuona tu nabadilisha mawazo.