Hakuna cha labda atabadilika, labda ana hasira, labda flani kamuwekea dawa, labda marafiki zake ndiyo wanamdanganya, labda nikwasababu niko hivi, labda nikwasbabu niko vile, labda nikwasababu hajanijua vizuri au sababu nyingine yoyote ile ambayo unaitumia kujipa moyo.
Wanaume wameumbwa tofauti na wanawake, wakati mwanamke anaweza kusema sitaki akimaanisha kuwa anataka ila tu uongeze nguvu katika kumbembeleza na kuongeza vishawishi, mwanaume anaposema sitaki, sikutaki anamaanisha hataki, sikutaki.
“Kuna wanawake wengi wapo kwenye mahusiano ya labda atabadilika, wapo na wanaume ambao wameshawaambia kua hawatawaoa au hawana mipango ya baadaye nao lakini bado wana ng’ang’ania wakidhani kuwa watabadilika.
Nikweli wanaweza kubadilika lakini mara nyingi huwa ni kwa muda, watakuwa na wewe kwa muda hata kwenye ndoa lakini ipo siku kile kilichowafanya wakuambie kua sikutaki kitaibuka na utaishia kuumia. Kwa kawaida wanaume wanakuwa wawazi na humaanisha kile wanachokisema.
Hapa naomba mnielewe kidogo, haimaanishi kuwa eti kwakua mwanaume kakuambia sikutaki ndiyo ukimpa mwili wako atakataa. Hapana, kwa mwanaume kuna kutokutaka kuwa na wewe na kutokutaka kufanya mapenzi na wewe. Hapa wanawake muelewe kabisa mwanaume hahitaji kukupenda ua hata kukutamani ili kuweza kufurahia mapenzi na wewe.
Inawezekana hata humtamanishi, akikuangalia anasikia kichefuchefu lakini mizuka yake ikimpanda atakufumua na ukimkatia kiuno atakusulubu na kesho ukitaka tena atakupa mechi ya nguvu lakini hilo lisikudanganye eti kwakuwa unamfurahisha kitandani labda ndiyo atakupenda.
Wanaume wana vichwa viwili na kila kichwa hufanya kazi wakati mwingine bila kushirikisha mwenzake hivyo usijipe moyo eti kwakuwa kichwa cha chini kikikuhitaji anakupigia simu ukadhani labda na kichwa cha juu kishakukubali. Kama kakuambia wazi hakupendi na hana mpango na wewe, dada, furahia mechi tu na waza maisha yako.
“Wadada wengi hujichanganya na hata kubeba mimba wakidhani watawashika, utamshika kwa muda tu ila kama hakuepndi atalea mwanae na kutafuta wakuoa anayempenda. Atakuwa anakuita kila siku kwakua unampa mechi kali lakini akisha sema sikutaki, siwezi kukuoa kimbia, anaweza kukuoa lakini usiwe mke wake ukawa mfanyakazi wake.
Ukalazimishia ndoa kweli, ukatafuta na waganga au ukabeba mimba na kwakua ni mstaarabu akakuoa. Lakini kukuoa haimaanishi kuwa ni mkewe, inamaanisha tu ni mwanamke anayeishi naye kwajaili ya kufanya naye mapenzi na kumsaidia kazi za nyumbani.
Utajikuta unaingia kwenye ndoa ya mateso na hutakuwa na wakumlaumu. Akisema sikutaki, kimbia kabisa acha kujipendekeza anamaanisha hakutaki kweli. Wapo wenzako wengi ambao walijaribu wakidhani watawabadilisha wakaishia kujipotezea muda wakaachwa na wale ambao walifanikiwa kuolewa lakini wameishia kuwa wafanyakazi wa ndani.