Wednesday, November 15, 2017

Mume Wangu Amerudiana Na Mpenzi Wake Wa Zamani Nifanyeje?

Habari ndugu, mimi ni Mama wa miaka 28. Nimeolewa na nina mtoto mmoja. Mume wangu anamiaka 40. Kabla sijaolewa tulika kwenye mahusiano miaka 5. Kwakeli nilimpenda sana nilimheshimu  naye alinipenda sana. Alinikutu bado msijacha yani bikra alifurahi zaidi alinipenda zaidi alinifungulia account alikuwa ananiwekea pesa za matumizi. Alinisomesha kuanzia format 6 mpka chuo.
Nilimtambulisha nyumbani wakamkubali alikuwa mpole mstaarabu mwenye busara na hekima zote. Maisha yalisonga, nilikuwa naenda kwake nafanya usafi wote napika kufua nguo. So kuna siku nilikuwa nasafisha ndani nguo ya ndani ya mwanamke ambayo si yangu. Niliumia sana nikarudi nyumbani nikawa sina amani kabisa na yeye hakunitafuta baade nikampigia simu nikamwambia nilichokiona.
Jibu alilonipa kwamba yeye ni mwaume anapesa na anauwezo wa kuwa na mwanamke yoyote atakaye mtaka kisha akatata sim . Ikapita kam wiki nikaenda kwake nikamuomba tuzungumze alinijibu kwadharau san nikashindwa kuvumilia nikaitafuna laini yangu ili asinitafute tena Kwa kweli maisha kwangu yalikuwa magum san. Matatizo yakaanza kunianda nilikuwa na mawazo san ikafikia kipindi nikagombana na ndugu yangu niliekuwa nikiishi nae .
Visa vilikuwa vingi sana hapo nyumbani, yule Mwanaume hakunitafuta tena Matatizo juu ya Matatizo Nikamfuata Dada yangu mkubwa nikamuadithia akaniambia nawaza nini Nikamwambia mi nataka kupanga akasema hawezi kuniruhusu mpaka aongee na mama kweli aliongea nae na wakaniruhusu nikapanga na kuanza maisha.
Mambo yalikuwa magum sana tena sana lakini nikaakimya sikuwaambia nyumbani Baada miezi mitatu nikapata kazi maisha yakawa mepesi kwangu. Siku moja nikiwa kwenye mishe mishe za maisha nikakutana na yule mwanaume. Tulikuwa hatujawahi kuwasiliana kwa miaka miwili tangu nikute ile nguo ya ndani.
Alinisalimia na tukaanza kuongea akataka tuongee kuhusu yale mambo lakini nilikataa nikamwambia tutapanga siku ya kuongelea hayo nikaondoka zangu.  Nimefika kwangu nikawa na mawazo san. Kila sik akawa ananijulia hali baada ya wiki mbili tukaonana tena na huyo mwaume alikuwepo nikaenda na aliniomba san msamaha na akasema ameshaachana na yule mwanamke bado ananipenda sana.
Alipiga magoti kwakeli nililia sana na nilikuwa bado nampenda nikamsamehe nikamueleza kwamba nimepanga akashtuka san akaniomba anichukue nikaishi nae kwake lakini nilikataa Baada ya miezi mitano tukiwa tunawasiliana wakati huo nilikuwa na mahusiano na mume wa mtu ikanibidi niachane nae.
Nikarudiana na huyo mchumba wangu cha ajabu alikuwa hataki kabisa kupajua nilipopanga Nikasema fine. Akawa ananilazimisha nikakae kwake lakini msimamo wangu ulikuwa mguu nilikataa katakata. Alikuwa na nyumbani nzuri ya kisasa alikuwa anaishi na wadogo zake so uwezo wa kwenda kukaa ulikuwaepo kwani yeye ndio mkubwa na nyumba ni yake lakini niligoma.
Baada ya msimamo wangu akaniomba tufunge ndoa nikakubali na tukaoana. Maisha ya ndoa yalikuwa matam san. Nikapata ujauzito Baada ya miaka miwili mambo yamejirudia yaleyale Kitu kidogo anafoka Ananituka hana time na Mimi tena kitandani tunaweza tukaa miezi hata sita bila kugusana na nikijaribu kumuliza ni makofi tu.
Japo ananijali kwa kula kulala na kuumwa lakini amekuwa mkali san Chochote nikitendacho endapo kimemkwaza ni kashifa tu kwangu anauwezo kutonisemesha hata wiki tatu. Najaibu kumuomba msamaha lakini wapi. Nikaamua kufanya uchunguzi kumbe karudiana na yule mwanamke wake wa zamani jamani naomba ushauri nifanyeje? Nakuomba usinitaje jina langu. Nisaidie kimawazo, ninafanya kazi hivyo naingiza kipato changu.