Tuesday, November 14, 2017

Kuvumilia Mateso Kwasababu Ya Pesa Hakukufanyi Kuwa Mke Bora Bali Kahaba Anayeteswa



Najua ni maneno makali lakini nilazima yasemwe, kuna idadi kubwa ya wanawake ambao wapo kwenye ndoa, si kwasababu ya upendo bali kwasababu ya pesa. Hilo si jambo baya kwani maisha yenyewe mafupi, umezunguka hakuna wakukuoa au yupo na haeleweki poteli ya mbali kula hela utampenda mbeleni.
Lakini kama mwanaume uliyeko naye anakupiga, anakunyanyasa anakusaliti kila si na huna furaha halafu unajidanganya kuwa ndoa ni uvumilivu, wakati hata humpendi huyo mwanaume upo naye kwasababu ya pesa zake basi hata kama una ndoa inakufanya kuw akahaba anayeteswa

Labda ili unielewe kabla ya kutoa mapovu na kunilaumu kuwa nimetukana nichambue maana ya neno “Kahaba” tafsiri hii nimeitoa kutokana na neno la kizungu Prostitute ambayo humaanisha “…a person, typically a woman, who engages in sexual activity for payment”.
Hapa wanamaanisha kuwa ni mtu (hata mwanaume anaweza kuwa kahaba) hasa mwanamke ambaye hujishughulisha na masuala ya kimapenzi kwaajili ya malipo. Kwamba unafanya mapenzi kwaajili ya pesa, hapa hawajataja idadi ya wanaume ambao unapaswa kujishughulisha nao au kama mko kwenye ndoa au la.
Kwa manaa hiyo basi kama wewe ni mwanamke umeolewa na mwanaume ambaye humpendi na unapenda pesa zake, kwa maana kuwa uko kwake kwasababu anakupa hela, anakununulia chakula mavazi na kila kitu basi wewe ni kahaba.
Hivyo hivyo kwa mwanaume kama umeoa mwanamke kwasababu ya pesa na humpendi bali unafanya mapenzi ili upate pesa zake basi wewe ni kahaba. Lakini kama nilivyosema sijambo baya, nijambo baya kama unapigwa au unayanyasika hapo ndipo unageuka na kuwa kahaba anayepigwa.
Wakati kahaba wa mtaani yeye husimama au hukutana na mwanaume wakafanya mapenzi akalipwa na kila mtu kwenda kivyake. Wewe unakua na mwanaume, anafanya mapenzi na wewe mnaendelea kuwa pamoja mkiishi kwenye nyumba moja, lakini ukimuudhi anakupiga na kwakua unahitaji hela zake unavumilia na upo tayari kuvumilia kipigo ili uishi tu kwenye nyumba nzuri.
Kuna wanawake wanaovumilia vipigo kwakuwa wanapenda, yaani hawajali hata kuhusu pesa, ingawa sikushauri kuvumilia lakini wewe hauko kwenye kundi hili. Hapa nazungumzia wale ambao wanapigwa wanakasirika lakini mume akirudi anamnunulia nguo au mkufu anamsamehe, hasamehi kwasababu anafurahia kupigwa bali kwa sababu ya ule mkufu au nguo.
Lakini kuna wale ambao anamfumania mumewe kila siku na wanawake tofauti, lakini kwakuwa anapewa pesa basi huvumilia. Huyu hana tofauti na wale wanaojiuza, kwani wanaojiuza hutembea na wanaume tofauti tofauti na kulipwa nao, lakini yeye hutembea na mwanaume mmoja ambaye ana wanawake tofauti tofauti na kulipwa na huyo mwanaume mmoja huku akiwa sawa na ametembea na wanawake wote wanaotembea na yule mwanaume.

Hapoa nikimaanisha kuwa, ingawa unatembea na mume wako tu ambaye unajua ana vimada 20 lakini kama wale vimada ishirini kila mmoja akiwa na gonjwa lake yatakusanywa kwa mumeo na utapewa yote wewe. Hii ni sawa na yule kahaba wa mtaani aliyekusanya magonjwa ya wanaume ishirini.
Najua kwamba kama uko kwenye hali hii ushaanza kutukana na kuniona nimeandika vitu vya uongo, unajipa moyo kuwa unavumilia ndoa kwakuwa mna watoto, lakini ukweli nikuwa kama humpendi huyo mwanaume na hufurahii mnapofanya mapenzi acha kuwasingizia watoto, unavumilia kwasababu ya pesa.
Kwa mwanaume kufanya mapenzi na mwanamke ambaye hakuvutii na humpendi wala si shida kwakuwa hisia zetu si za kuunga unga zipo tu. Lakini kwa mwanamke kufanya mapenzi na mwanaume ambaye anakutia kichefu chefu ni kazi yaani hata hafurahii kwakuwa hisia zao ni za kuunga unga.
Hivyo kama unavumilia kufanya mapenzi na mwanaume kwa miaka kumi ambaye humpendi kwasababu tu ya pesa, hongera, lakini kama umevumilia na kipigo, manyanyaso basi pole na amka. Acha uvivu jishughulishe na tafuta cha kwako.
Vumilia ndoa kwasababu unampenda mtu, unafurahia kuwa naye hapo hata ukimuomba Mungu atakuelewa na kukubariki, anaweza kumbadilisha. Lakini kama unavumilia kwaajili ya pesa hata Mungu harakusikiliza kwakuwa hata wewe si msafi.
Unapoomba ushauri kwa mwanamke mwenzako akakuambia kuwa ndoa ni uvumilivu hata nayeye anavumilia hembu muulize sababu za yeye kuvumilia kwake ili usije kuwa unashauriwa na mtu ambaye amekubali mwili wake kutumika kwa mapenzi na kipigo kwaajili ya pesa!
Kwamba upo na mtu ambaye anavumilia kupigwa ili aendelee kuendesha gari zuri na kuringishia mtaani. Mtu ambaye anakubali kuipigwa kwasabu ya iPhone 6, mtu ambaye anakubali kupigwa kwasababu ya Brazilian hairs. Huyo atakuwa anajipa moyo tu kuwa ni mke wa mtu lakini ukweli ni mfanyakzi wa mtu.
Huna ulemavu wowote, una akili timamu halafu bado unajiuliza “Sasa nitafanyaje…nitaenda wapi?”. Acha kumkufuru Mungu aliyekupa nguvu na akili, siku huyo mwanaume akikuambukiza magonjwa, siku akikutoboa macho, akikuvunja miguu na kuw a mlemavu ndiyo utakosa kweli pakwenda.
Lakini pia huyo mwanaume anajua uko kwake kwaajili ya pesa ndiyo maana anakufanyia anachotaka. Mwanaume akijua unampenda kweli ni rahisi kubadilika kama unamvumilia lakini akijua unapenda pesa zake hana sababu ya kubadilika kwani ashajua unachotaka hivyo atahakikisha unakuwa nacho kila wakati.
Anajua akikupiga, ukimfumania akakuletea mkufu wa dhahabu unasahau, anajua akikupiga na kukupa ada ya ndugu zako unafurahi, sasa ana sababu gani ya kubadilika zaidi ya kuendelea kutafuta pesa tu ili kukuridhisha. usidhani nayeye ni mjinga hajui nini unapenda zaidi kwake pesa au yeye?