Friday, November 24, 2017

KILA UNAPOJARIBU KUMUACHA UNASHINDWA?, SOMA HAPA

Kuna watu wana Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija wa Oxygen yangu ya kutumia kesho?? Kama nilizaliwa peke yangu kwanini nisiweze kuishi wewe ukiondoka??
Maneno ya mkosaji haya, usiyasikilize kamwe! Unapoamua kufanya Maamuzi magumu usisikilize kingine chochote, Follow your heart. Wengi wamegeuzwa watumwa kwa kuamini they cant live bila watu fulani, kisa wamezoeana, au wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano, unahisi kama hutaweza... Hamna kitu kisichowezekana, Mungu ameumba kusahau, utapona maumivu na utasonga! Hakuna destiny rahisi ya Kimapenzi bila kufanya maamuzi magumu, lasivyo Jiandae kuwa mtumwa wa mtu fulani, binadamu fulani ambaye naye amegundua wewe ni dhaifu na anatumia udhaifu wako kukutesa maisha yote...
Amua leo, Uwe mtumwa wa mtu au utengeneze furaha yako kwa Kumove on kupata Lover of you life