Friday, November 24, 2017

Jua dalili za mwanamke anayekupenda na kuvutika na wewe kimapenzi.

"Wanasayansi wamethibitisha mawasiliano ya watu wanaokutana kwa mara ya kwanza hutegemea zaidi ishara za kimwili, ambapo asilimia 55% huwa ni kwa kutumia ishara, asilimia 38% yakiwa maongezi ya kutumia sauti pamoja na asilimia 7% ikiwa vitu ambavyo haviendani kabisa na unachokiongea."
Utafiti uliofanywa na chuo kimoja kikuu nchini Marekani, imebainisha kama ukitaka kujua iwapo mwanamke amevutiwa na wewe, inabidi uangalie zaidi ishara kuliko maongezi, na hii kuhitimisha wanawake huongea tofauti na wanachomaanisha. kiumeni.com imekuandalia ishara kumi zilizothibitishwa na watafiti pamoja na wanasayansi ambazo mwanamke hufanya pindi anapovutiwa na wewe akiwa anajijua au hakiwa hajijui ili kukuonyesha kama amevutika nawe.
Jifunze ishara hizi na maisha yako ya kimahusiano yatabadilika kwa hali ambayo hautaitarajia.

 #10; Anashika au kupikicha nywele.
Kwa zaidi ya miaka 40, watafiti wamenyumbuisha tabia wanazozifanya wanawake kukujulisha wamevutiwa na wewe, iwapo mwanamke akizishika shika nywele zake kwa muda mfupi inaweza kuwa ishara ya kukupa taarifa ya kuwa anafurahia uwepo wako, ila akiendelea kuzichezea kwa muda mrefu inawezekana akawa katika hali ya kutokujiamini au hakuamini wewe.

 #9; Anauma midomo yake.
Tabia hii mwanamke huifanya ili kuhamisha fikra zako kuelekea kwenye midomo yake, inaweza maanisha ukienda na ukiwa mchombezaji mzuri mabusu yanaweza kuwa ya kufikia, inabidi uwe mwangalifu sana wakati wa kuitambua hii tabia na akiwa anauma midomo yake kwa muda inamaanisha amevutiwa nawe ila kuuma midomo mara kwa mara inaweza onyesha ndio mazoea yake, kwa hiyo kuwa makini kutofautisha kati ya hizo tabia mbili.

#8; Anacheka cheka, kukusumbua na kukuangalia kwa macho mazuri.
Hii tabia zipo pande zote mbili, hata wanaume pia huifanya ila kwa wanawake wanaweza pia kuitumia ili kukujua nia yako kwao, kwa hio usiichukulie kwa haraka sana inawezekana anakujaribu tu.

 #7; Anakukaribia sana kimwili.
Ukaribu tunao karibia watu inategemeana na mahusiano yetu kwao, ukimkaribia mtu sana huwa mara zote ni katika hali ya upendo, kwahio mwanamke akikukaribia sana inawezekana akawa anafanya hivyo ili upendezwe naye zaidi, inabidi kabla hujafanya maamuzi yeyote hakikisha umehakikisha mkaribio wake kwako sio wa hali ya kikawaida, na unaweza hakikisha kwa kusogea kidogo ili kumtegeshea kama atasogea tena huku ukiwa na tabasamu usoni.

#6; Anachangia unachozungumza na kuongelea kuhusu mambo yake binafsi.
Baada ya kufanya mazungumzo kwa muda na kunoga, jaribu kupeleka mambo mbele kwa kuanzisha mada ambayo inahusu maisha yako binafsi ila hakikisha mada isiwe ya ndani sana na isiwe inaelekea kana kwamba unataka kumjua kwa undani na maelezo yake yasiwe yanamlenga, hii itamfanya ajisikie huru na kutokuogopa, iwapo mambo yakienda vizuri na amevutika nawe utaona na yeye  anachangia kwa kutoa mada inayohusu mambo yake binafsi, watu huwa wanaongea kuhusu mambo ya ndani kwa watu wanaowapenda na kujisikia huru mbele yao.
Iwapo maongezi haya mkiyafanya huku mnakula chipsi kwa pamoja itafanya mambo yaende vizuri zaidi, kutumia vitu pamoja huongeza ukaribu na maelewano zaidi.

#5; Anakua na urafiki wa kimaongezi wakati mnaongea.
  Sahau kuhusu mistari ya kutongozea ulioifanyia mazoezi, ikija kwenye kuangalia hamasa ya mwanamke kwako, huangalii jinsi unavyomsifia, unaangalia mapokeo ya maneno unayomwambia, mwanamke akikujibu hata kama kwenye hali ya kukataa jambo, akikujibu kwa sauti ya upole na laini ujue amependezwa nawe, kwahiyo usiwahi kuondoka kutoka katika mazingira hayo au sehemu hio, ila akikujibu kwa sauti ya ukali, tafuta pakutokea.

Ili kuondokana na kupoteza muda kutongoza mwanamke ambaye havutiwi na wewe, jaribu kwa kuanza na maswali rahisi ambayo majibu yake ni rahisi, kwa njia hii utajua kama kapendezwa na wewe au vipi, kama hajapendezwa na wewe utaona anakuondoa kwenye maongezi ila aliyependezwa na wewe ataendelea na maongezi.

#4; Anakua katika mkao wa mwaliko kimaongezi.
Mwanamke akiwa amependezwa na wewe huwa anakua amekaa mkao wa mwaliko wa kimaongezi, akikuangalia anakua na macho ya kiurafiki na si ya ukali na hata ukiwa mbali utajua kwamba pozi na macho yake vinakuita.
                
#3; Anakua na ishara unazozifanya wewe.
Mwanamke akipendezwa nawe, atakua anajibu mapokeo ya ishara zako unazotoa, kwa mfano ukitabasamu na yeye utamuona anatabasamu vile vile, ukicheka na yeye atakufatiliza hivyo hivyo.
                
#2; Anapindisha kichwa kidogo na kutabasamu.
Watafiti wamebainisha mwanamke akipindisha kichwa kidogo na kuachia sehemu ya shingo yake kuonekana kidogo ikifuatiwa na tabasamu mara nyingi anakua amevutiwa na anachokiangalia.
             
 #1; Anachezesha macho.
Kukutanisha macho ni kitendo cha ukaribu kwa binadamu, kurudia rudia au kuendeleza kukutanisha macho huwa kuna maana kuu mbili, kwanza kuonyesha hali ya mguso kihisia, na pili kuonyesha hali ya jazba.
Ili kujua kama analo hitaji la kuongea nawe, angalia jinsi anavyochezesha na kukutanisha macho na wewe, utakuta mnakutanisha macho zaidi ya mara kadhaa na kukiwa na tabasamu nyingi, kama ukiona mmekutanisha macho halafu akaacha kukuangalia tena jua huyo hajavutika na wewe, na isiwe na shaka sana maana mara nyingi kitu hichi huweza kutokea bila ya wewe kukitambua.