Tuesday, November 14, 2017

Hata Kama Anakuhudukia Kwa kila Kitu Hana Haki Ya Kukufanyia Anavyotaka Yeye

Mwanaume kukuhudumia kila kitu, mwanaume kuwa mume wako haimaanishi ndiyo ana ruhusu ya kukutumia anavyotaka. Baadhi ya wanawake hudhani kwamba kwakuwa kakupangia chumba, kwakuwa kakutolea mahari, kwakuwa kakuoa, kwakuwa anawasomesha ndugu zako na kukufanyia mambo mengine mengi basi ana haki ya kukufanya chochote anchotaka.
 
Ana haki ya kutembea na marafiki zako, anahaki ya kutembea na wadogo zako, anahaki ya kutukana na kudharau ndugu zako, ana haki ya kukupiga, anahaki ya kuwapa michepuko yake namba zako za simu, anahaki ya kukudhalilisha mbele za watu, anahaki ya kukuingilia kinyume cha maumbile, anahaki ya kukuingilia bila ridha ayako na mambo mengine kama hayo.
 
Hakuna mwanaume mwenye haki ya kufanya kitu chochote kwako kama hutaki akufanyie. Kumbuka wewe si bidhaa, wewe si kuku kwamba amekununua na anaweza kukuchinja, kukupika, kukuchemsha au hata kukukatakata na kuwapa mbwa wake.
 
Wewe ni mpenzi wake, mke wake na kubwa kabisa wewe ni mwanamke. Anapaswa kukuheshimu na wewe hupaswi kuruhusu akufanyie vingine. Unapomruhusu kukuvunjia heshima katika mambo madogo ndiyo hivyo hivyo unalea ugonjwa na hatakuheshimu milele.
 

Lazima kuwa na mipaka na mambo ambayo anataka kufanya na wewe na mambo anayokufanyia, hata kama anakupa pesa nyingi kiasi gani ni lazima uwe na uwezo wa kumuambia hili hapana. Nilazima uweze kumuambia Baba nilizaliwa bila pesa, nilizaliwa bile mume lakini nilizaliwa kama mwanamke niheshimu.