Sunday, November 12, 2017

ACHA NDOA IKUTAFUTE. SOMA MAKLA HII

Kila Ukiamka Unamuomba Mungu Akupe Mume Na Kuna Wakati Unataka Hadi Kumkufuru Pale Unapokuwa Unasali Na Hakuna Matokeo Mazuri Ya Sala Zako.

Kila Unapolala Unaendelea Na Sala Zako Ukiamini Kabisa Kesho Atakupa Yule Ambaye Utaanzisha Naye Familia Na Kuwa Nae Kama Mumeo.


Kuna Wakati Unaamka Usiku Wa Manane Na Usingizi Unaisha Unaanza Kulia Na Unaanza Kufikiria Wenzako Walioolewa Na Wewe Upo HapoHapo Na Umri Unazidi Kwenda.

Unafika Hadi Wakati Unaacha Imani Yako Na Unaenda Kwa Mganga Mradi Tu Upate Mume Na Uolewe Kama Wengine.

Lakini Hufikirii Kabisa Kuhusu Huyo Mume Wa Mtu Uliyenaye Kwenye Mahusiano, Unaona Sawa Kabisa Unavyomtesa Mwanamke Mwenzako Na Watoto Wake, Wanashindwa Kupata Mapenzi Ya Baba Kwakuwa Muda Mwingi Umembana Na Hahemi Wala Kufurukuta.

Mungu Ni Wa Wote, Kama Wewe Unavyosali Upate Mume Wako Na Uje Kujenga Familia Ndivyo Ambavyo Yule Mama Anavyosali Ili Mume Wake Atoke Kwako Arudi Kwake Alee Familia Yake.

Muache Kwanza Huyo Mume Wa Mwenzako Halafu Usali, Ndani Ya Muda Mfupi Utasikilizwa Sala Zako, Mungu Habagui Na Huwa Anasamehe Na Kubariki Tena.