Si kazi yako kumfanya kila mtu akupende, sikazi yako kumfanya kila mtu kuvutiwa na muonekano wako, si kazi yako kumfurarahisha kila mtu. kazi yako pekee ni kuhakikisha unakuwa mtu bora kwa kadri ya uwezo wako, kuhakikisha unafanya matendo ambayo hata kama hayatamridhisha mwanadamu bali yatamridhisha na kumfurahisha Mungu.
Kinachotokea baada ya hapo hakikuhusu, kama hujafanya kitu cha kumuumiza mtu halafu akaumia kwa sababu ya kutokujiamini kwake au kujishuku kwake hilo halikuhusu. Kama hujafanya kitu kwaajili ya kumkera mtu halafu yeye akakereka kwakuwa hujafanya kama anavyotaka yeye hilo halikuhusu.
Kama umeongea kitu kwa nia nzuri halafu mtu mwingine akakuelewa vibaya na akakasirika hilo halikuhusu. Unawajibika na matendo yako na si namna watu wanavyoyachukulia matendo yako. Usipoteze muda wako kujuaribu kuwaridhisha watu kwani hata wao hawakuridhishi.
Utakosa muda wa kufanya yako kama kila unachofanya unageuka nyuma kuangalia nani kanuna nani kafurahi? Maisha yako yanakuhusu wewe tu na watu wako wa karibu ambao matendo yako yanaweza kuwaathiri na kukunyima furaha wanapokwazika. Chagua furaha maisha si magumu kiasi hicho.