Friday, December 21, 2018

SOMA HAPA KUJUA YANAYOWEZA KUMFANYA MPENZI WAKO AKATEMBEA NA RAFIKI YAKO!

Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.

Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.
Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita nilikuwa na kazi kubwa ya kumshauri rafiki yangu ambaye aliniletea mashitaka ya mpenzi wake kutembea na rafiki yake.

Nilipata wakati mgumu sana kwani nilipoongea na msichana akaniambia wazi kwamba, amekuwa hapati penzi alilotarajia kutoka kwa rafiki yangu.




Msichana huyo akaenda mbele zaidi na kusema kwamba, yule shemeji yake alionesha kumjali sana kiasi kwamba siku alipomtamkia kwamba anampenda ilimuwia ngumu kukataa.

Kuna kitu cha kujifunza hapa kwamba endapo utaishi na mpenzi wako bila kumdhihirishia kwamba unampenda kwa dhati, akitokea mtu wa pembeni akaonyesha kuwa kafa kaoza, tarajia kusalitiwa kama siyo kuachwa kwenye mataa.

Unapokuwa umeanzisha uhusiano na mtu, utambue ana watu wengi wanaomtaka lakini huenda anawakatalia kwa kuwa yuko na wewe, sasa ukionesha kutomjali, hawezi kuendelea kuwa muaminifu kwako. Atachepuka na hata kama ataendelea kuwa na wewe ni kwa kuwa labda hana ujasiri wa kukuacha.

Ndiyo maana leo nikaona nikupe sababu ambazo zinaweza kumfanya mpenzi wako akatembea na rafiki yako tena wakati mwingine kwa siri bila wewe kujua. 
Wewe mwenyewe
Endapo utakuwa umeanzisha uhusiano na mtu, wewe mwenyewe unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa. Usipoonesha kumpenda, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako akayaonesha hayo kwake, ni rahisi sana kukupiku.

Kwa mfano, endapo umekuwa na mpenzi wako lakini hata siku moja hujawahi kumpa zawadi au kumtoa ‘out’, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya hivyo, mpenzi wako atahisi yeye ni mtu sahihi kwake. 
Kujirahisi kwake
Wapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya kujirahisi kwao. Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mambo ya chumbani na rafiki wa mpenzi wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mpenzi wako lengo linakuwa ni lipi?
Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi. Hapa namaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi.

Kumuamini sana
Haishauriwi kumuamini sana rafiki yako kwani wengine wakipewa uhuru wa kuwa karibu na mashemeji zao, huchukulia kama fursa ya pekee.
Kwa mfano, unapomuamini rafiki yako kiasi cha kumruhusu aende na mpenzi wako baa, klabu au ufukweni ni kujitafutia matatizo.

Tunajua kwamba wapo marafiki waaminifu lakini tambua tu kwamba wengi wanapokuwa katika mazingira hayo ndipo huishia kusaliti na wakati mwingine bila kupenda.
Kwa nini nasema bila kupenda? Chukulia umemruhusu mpenzi wako aende baa na rafiki yako, wamekunywa pombe hadi wamelewa kisha rafiki yako anamchukuwa mpenzi wako kwenye gari kumrudisha nyumbani.

Wengi kwenye mazingira hayo uzalendo unawashinda. Kwa hiyo kama hutaki yakukute ya kusalitiwa, kama una tabia ya kumruhusu mpenzi wako kwenda baa na shemeji yake, acha mara moja.

Rafiki mnafiki
Unaweza kuwa na rafiki lakini kumbe ni mnafiki. Huyu ni yule ambaye mko pamoja lakini anajiapiza kwamba siku moja lazima atakuchukulia mpenzi wako. Huyu ndiye tunamuita rafiki mnafiki.

Kutokana na tabia hizo ndiyo maana matukio ya baadhi ya wanaume kuwatongoza wapenzi wa marafiki zao yamekuwa yakiongezeka. Pia wanawake wengi sasa hivi hawaoni hatari kuwatongoza marafiki wa wapenzi wao au wapenzi wa mashoga zao.

Penzi la kweli
Mfano Juma ana mpenzi wake aitwaye Asha na Juma ana rafiki yake aitwaye Jamali. Juma na Asha ni wapenzi lakini hawapendani kivile ila Jamali anaonekana kuwa na penzi la kweli na Asha na wakati huohuo Asha naye anahisi kuwa na penzi la kweli na Jamali.

Katika mazingira hayo usije ukashangaa siku moja kusikia Asha katembea na Jamali. Siyo kutokana na tamaa au ushawishi bali ni kutokana na uwepo wa penzi la dhati kati yao. 
Katika mazingira haya ndipo ambapo tumekuwa tukisikia fulani kamuacha mkewe kisha yule mke kaolewa na mwanaume ambaye alikuwa rafiki wa wanandoa hao.

Tamaa tu
Endapo utagundua mpenzi wako katembea na rafiki yako, kuna uwezekano ameshawishiwa kwa pesa au mali. Hii ni kwa sababu wapo watu ni dhaifu sana, yaani wao kusaliti wapenzi wao kwa sababu ya pesa, mali au tamaa zao za kimwili siyo kitu kigumu.

Ndiyo maana tunashauriwa kuwa na wapenzi ambao hawana tamaa za kijinga. Katika siku za mwanzo za uhusiano wenu ukigundua uliyenaye si mtu wa kuridhika na penzi unalompa, pesa na mali mlizonazo, mapema muonyeshe mlango wa kutokea kwani itakuwa siyo jambo la ajabu kusikia katembea hata na ndugu au rafiki yako.

TABIA 30 ZA MWANAMKE ANAYEWEZA KUKUFAA KATIKA MAISHA YAKO.

Mwanamke ni mama mwenye nguvu unajua kwa nini kwa sababu mwanamke alitoka katika ubavu wa mwanaume baada ya Mungu kufanya yafuatayo kwa mwanaume
A. Alimpa usingizi mwanaume 
B. Alimfanyia upasuaji
C. Damu ilitoka kwa wingi kwa mwanaume
D. Nyama ilitolewa kwa mwanaume 
E. Mfupa ulitolewa kwa mwanaume
F. Baada ya kufanyiwa hivyo mwanaume ndipo mwanamke akaumbwa akatoka mwanaume akakiri na kusema huyo ni mfupa katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu –hivyo ataitwa mwanamke napenda ujue kuwa Mwanamke amebeba uponyaji wa mwanaume na mwanaume amebeba vidonda kwa ajili ya mwanamke
Mwanamke ni mfupa mwanaume ni udongo hivyo mwanamke ni:
1. Ni nguvu ya mwanaume
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia 
6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla 
7. Mlinzi wa mwanaum 
 8. Chanzo cha baraka ya familia
9. Adui wa maadui wa familia
10. Sauti ya familia
11. Mponyaji wa familia yake na taifa 
12. Mlezi wa huduma
13. Mkombozi wa familia na taifa
14. Mwombezi wa familia,huduma na taifa
 16. Mficha siri wa Mungu
Baada ya kujua umuhimu wa mwanamke tunatakiwa kuangalia kiundani sana tabia 30 za mwanamke bora sio bora mwanamke tumeumia sana baada ya kuowa watu wasio sahihi katika eneo lilosahihi mwanamke bora ni mwamuzi wa familia ndio mleta mabadiliko katika familia mwanamke anayejua kwanini nipo hapa na ninafanya nini?
Mimi nimefanya utafiki kutokana na vitabu na maisha yanayotuzunguka nimeweza kugundua tabia 30 za Mwanamke anayeweza kunifaa mimi na wewe rafiki yangu tuziangalie kwa makini sana na kwa utafiki wa ndani:-
1. Moyo wa Mwanaume humwamini:
Moyo wa M wanaume humwanini Mwanamke bora sio bora Mwanamke, Mwanamke bora hujitahidi sana ili aweze kuaminika kwa mume wake maana Imani ni kitu muhimu sana katika mahusiano, mahusiano yakipoteza Imani hapo hakuna mahusiano, Mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kujiaminisha kwa Mwanaume kuwa yeye ni mtu sahihi na chaguo sahihi kwa Mwanaume wake. Moyo ndio unaothibitisha kuwa huyu ni mtu sahihi au sio sahihi 
Moyo ndio unamkubari mtu
Moyo ndio sauti ya mwisho
Moyo ndio chanzo cha upendo
Moyo ndio jibu la maisha yako ya mapendo
Moyo ndio chemichemi ya mapenzi
Moyo ndio unaoamini na kinywa husema yaliyo maamuzi ya moyo.
Huyu Mwanamke anatakiwa awe na jibu kwa Mwanaume- Upendo wa kweli hautambuliki kwa muonekano wa mtu bali upendo huambulika toka moyoni:- Hivyo Mwanamke bora ni Yule anayeweza kuushika moyo wa Mwanaume na kujiaminisha kwake.
2. Huondoa umaskini
Mwanamke bora katika maisha yako ni Yule mwenye mawazo mazuri ya kuondoa umaskini katika maisha yako- hana wazo baya, wengi wao wanatamani kuolewa ili awe na sifa mtaani kuwa ameolewa lakini ni tegemezi, hana wazo jipya la kubadilisha maisha yako. Hawa sio wanawake sahihi mawazo yake yanamtegemea mwanaume, wazo lake ni kuzaa watoto hana wazo la maendeleo, hajui maumivu ya maisha huwa wanarudisha nyuma ndoto zako kutokutimia kwa wakati wake. Mwanamke bora ni Yule mwenye mawazo ya maendeleo, mwenye hasira na umaskini mpenda mafanikio huyo ndiyo anafaa kuolewa
3. Kamwe hamtendei Mume wake mabaya
Mwanamke bora yaani niniamaanisha aliye sahihi ni Yule mwenye moyo safi kwa mume wake,
1. Hawazi mabaya bali mema kwa mume wake, 
2. Hawezi kumtendea mume wake mabaya, 
3. Hawezi kumuumiza mume wake, 
4. Hawezi kumtonesha vidonda mume wake, 
5. Hawezi kuumsaliti mume wake, 
6. Hawezi kumtendea yasiyo haki mume wake, 
7. Hawezi kumchafua mume wake na kumdharirirsha katika jamiii iliyowazunguka, 
8. Hawezikumtukana Mume wake,
9. Hawezi kushabikia maumivu na mateso ya Mume wake, 
10. Hawezi kuwa radhi na maadui wa Mume wake, 
11. Hawezi kuwa jeuri kwa Mume wake, 
12. Hawezi kumtendea Mume wake mabaya. 
13. Amejaa heshima kwa Mume wake, 
14. Adabu, 
15. Utu wema anatunza uthamani wa Mume wake 
16. Amejaa utiifu na upole kwa Mume wake 
17. Amejaa unyenyekevu na uaminifu kwa Mume wake, 
18. Amejaa amani na furaha ya kweli kwa Mume wake-
19. Anayeshinda uovu kwa wema, 
20. Mwenye upendo wa kweli kwa mume wake. Huyu ndiye Mwanamke unayeweza kumuowa au kuishi naye na ndio sifa ya Mwanamke anayehitajika katika maisha yako. Mwanamke huyu ataheshimika na kuthaminiwa na watu na hatakosa upendo wa dhati kutoka kwa Mume wake.
4. Hufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii
Mke bora sio bora Mke ni mchapa kazi ni mtafutaji kwa mikono yake mwenyewe ni mjasiliamali hataki kuwa mzigo wa familia, kwa mikono yake anajenga, kwa mikono yake anasomesha watoto wake, kwa mikono yake anatunza familia yake kwa mikono yake anaheshimisha familia, mfanya kazi kwa bidii asiyechoka usiku na mchana sio mvivu, kwa mikono yake anafanya hategemei fedha za Mume wake- huyu anafaa kuwa Mke sahihi katika maisha sio mlinda mlango ni mtafutaji anakufaa sana katika maisha, napenda kukwambia mapenzi sio kuzaa, mapenzi kama pesa hakuna hutaona udhamani ni wake pesa ni jawabu la kila kitu sasa Mwanamke anajishughulisha anafaa sana katika maisha yetu ya leo- mapenzi ni kusaidiana. 
Mwanamke sahihi hi Yule anayefanya kazi kwa mikono yake kwa bidii, Mwanamke ningependa kukushauri kuwa mali za Mwanammme ni mali za watoto na mali ya Mwanaume ni mali ya watu wengi, leo wanawake wengi wanateseka sana baada ya waume zao kufa wamenyang’anywa mali zao na ndugu wa kiume wanateseka sana kwa sababu walikuwa tegemezi kwa waume zao, Mwanamke wa kweli ni Yule mtafutaji na kuwawekea watoto zake mazingira mazuri ya maisha yao ya kesho.
5. Yeye ni kama meli ya biashara.
Mwanamke anafananishwa na meli ya biashara kwa sababu meli ya biashara inachukua bidhaa mbali mbali ndani yake, Mwanamke amebeba majukumu mengi sana katika maisha yake, mwanamke huyu ni:-
a) Mlinzi wa Mume wake.
b) Mzazi, mlezi mwenye watoto.
c) Mwangalizi mkuu wa familia yake na mazingira yake
d) Mwalimu Mkuu wa familia yake
e) Adui wa maadui wa familia yake.
f) Muombaji wa familia yake.
g) Kisima cha amani katika familia na ndugu wanaomzunguka.
h) Chanzo cha Baraka ya familia
i) Mficha siri ya familia- najua unajua kuwa Mwanamke ndio mficha siri wa familia anajua yote yanayofanyika ndani. Mwanamke ana majukumu mengi sana huku mtoto analia, baba naye anamwita huku watoto wanataka kusoma, wakwe wanataka chakula na mavazi huyu anatakiwa kusaidiwa lakini Mwanamke wa namna hii ndiye anayetakiwa katika maisha yako ndiyo maana amefananishwa na meli ya biashara malalamiko amepewa yeye matusi yeye, sifa njema yeye Mwanamke ni gari la familia. Nyumba yenye heshima inamuhitaji Mwanamke sahihi.


6. Huleta chakula chake toka mbali, 
Mwanamke bora hategemei kulishwa na Mwanaume anasifa yakutafuta chakula chake toka mbali, hulisha familia yake kwa pesa yake, anahakikisha kuna kila kitu kinachohitajika katika famila yake, tegemeo la Mume wake Mume humwamini, nguzo ya familia yake, huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu, huyu anafaa ni chaguo lililo sahihi katika maisha yako.
7. Huamka kabla ya mapambazuko.
Mke bora huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kupanga mambo yake ataamka na kufanya usafi ndani, mazingira yake kiujumla huandaa chakula mapema hupangilia kazi kwa waliomo ndani mwake hufanya hivi na wewe fanya hivi sio Mwanamke anayeamka saa tatu (3) asubuhi au saa nne (4) asubuhi huyo ni mvivu hafai kuitwa Mwanamke bora bali ni bora Mwanamke hafai hana faida katika kuchangia maendeleo maana hata maandiko matakatifu yanasema “Siku njema huonekena alfajiri” mafanikio, Baraka, amaendeleo, huanza asubuhi Mwanamke anyefaa utamwona anaamka asubuhi sana na kupangilia mambo yake sawa, watu wa nyumbani watakula muda sahihi, wataenda shule wakiwa wamejaa amani mwenye maneno mazuri juu ya watoto wake na familia yake kwa ujumla. Huyu ndiyo Mwanamke anayetakiwa katika maisha yako, sio wanaoamka muda wanaopenda, Mwanaume anaandaliwa chai na mfanyakazi wa ndani, nguo za mume wako zinanyooshwa na mfanyakazi, maji ya kuoga mume wako yanaandaliwa na mfanyakazi wa ndani wewe sio Mwanamke sahihi na hufai kuitwa Mke bora wewe ni bora mke.
8. Hufikiri kununua shamba kisha hulinunua.
Mwenamke bora katika maisha hana mtazamo wa kununuliwa shamba, gari, nyumba na chochote cha maendeleo yake na familia hufanya mwenyewe akipenda kitu hununua hanunuliwi huyu ndiye Mwanamke wa Biblia mbunifu wa maisha anayetazama mbali sana kwa fedha yake hufanya maendeleo makubwa sana katika maisha yake, huyu ndiye Mwanamke bora anayefaa katika maisha yetu ndiyo Mwanamke anayetafutiwa na watu wenye maendeleo. Anaishi Kwa Jasho Lake, anategemea jasho Lake Hulima, hufanya kazi ili awezekutimiza ndoto zake.
9. Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
Mwanamke bora huwa tayari kufanyakazi kwa nguvu sana kwa ajili ya familia yake, anajituma kwa bidii kwa kila shughuri anayoifanya, ni mama mwangaikaji, mwenye kiu ya kutimiliza ndoto yake, mwenye kutambua wajibu wake kitaifa na kifamilia, mwenye mtazamo wa mbali, mwenye kiu na maendeleo, mwenye mzigo na familia yake, adui wa umaskini, ujinga na maradhi, mwenye kujituma kabla ya kutumwa. Huyu ndiyo Mwanamke anayetakiwa kuwa nayo katika maisha yake, huyu ndiye mama wa kibiblia sio bora Mke ni Mke bora.
10. Mwenye kuthamini shughuri zake.
Mwanamke bora anathamini sana shughuri zake kuwa zinafaida anaikubali kazi anayoifanya kuwa inafaa, hana tama na kazi za wengine ana heshimu kazi yake sana, hatishwi na maendeleo ya wengine maana naye ni Mwanamke anayejiamini sana kuwa hata yeye atafika, mwenye matumaini na Imani kubwa kwa kile anachofanya. Huyu ndiye Mke anayefaa katika maisha hutasikia malalamiko, hayupo katika mashindano, hana tamaa mbaya ningependa kukushauri kuwa mwanamke anayekufaa sio Mwanamke akiona mwenzake amevaa nguo Fulani naye anataka huyo hakufai ni muharibifu wa maendeleo atakurudisha nyuma kimaendeleo, tafuta Mwanamke huyo hapo juu.
11. Hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
Mwanamke huyu mjasiliamali hata usiku hufanya mambo yake kwa ajili ya maendeleo, hukanda unga wa maandazi, hushona nguo, vitambaa, hupanga mambo yake kabla ya siku mpya, wenye kutambua wakati alionao, huyu ndiye Mwanamke anaye kufaa katika maisha yako na ni Mwanamke wa kibiblia.
12. Asiye mchoyo.
Mwanamke bora sio mchoyo hufungua mikono yake kwa wahitaji, Mwanamke mchoyo hakufai maana ananyima Baraka katika maisha yako, Mwanamke mchoyo ni mchawi wa maendeleo, Mwanamke bora ni mtoaji, mwenye huruma na wahitaji ni mlezi wa wengi, kioo cha fmailia mwenye roho ya msamaha, ni mama wa wote walio wake na wasio wake, kwa aliyembariki na aliyemlaani, hana ubaguzi, mwenye moyo wa mama wa kweli, mwangalizi wa wote. Huyu ndiye mwanamke unaye muhitaji katika familia yako- usifanye makosa huyu ndiyo Mwanamke wa kibiblia.
13. Hana hofu na maisha ya watoto wake.
Mwanamke bora huwa anahakikisha kuwa anawaandalia watoto wake maisha mazuri, anawapeleka shule, msimamizi wa maendeleo yao, mtetezi wa haki zao, anahakikisha watoto wake wanakuwa na nguo, elimu nzuri, afya nzuri, kazi nzuri na anawaandalia maisha mazuri watoto wake hivyo anauhakika na maisha yajayo ya watoto wake. Huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu.
14. Mwenye kujipenda
Mwanamke bora anajipenda sana, anajidhamini, ni mzuri sana, mwenye kujikubali mwenyewe, adui wa uchafu, hawezi huwezi kumkuta mchafu hata watoto wake wanaoga, anapiga mswaki, anapika mafuta yake mazuri, na anaweka na marashi mwilini ili anukie vizuri sana, anatamanika, mavazi yake mazuri sana, anamvuto aonekanapo wakati wowote nyumbani na nje ya nyumba yake, Ua la familia, huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anamvuto wa kuwanaye karibu, kutembea naye anayethanini usafi wa mwili wake kuanzia chumbani kwake hadi nje huyu ndiye Mw anamke ninayekushauri uwe naye, huyu ndiye Mwanamke wa kibiblia.
15. Mume wake hujulikana malangoni.
Mwanamke bora humtambulisha Mume wake malangoni, Mwanamke ni pazia ya nyumba, 
1. Pazia husitiri mambo ya ndani,
2. Pazia hupendezesha nyumba, 
3. Pazia mlinzi wa nyumba, 
4. Pazia huthaminisha nyumba, 
5. Pazia hutambulisha wakaao ndani ya nyumba, 
6. Mwanamke ni pazia ya Mume, 
7. Ndiye anayempendezesha Mume, 
8. Mlinzi wa Mume 
9. Ndiye anaye mthaminisha Mume, 
10. Andiye anaye mtambulisha Mume, 
11. Kioo cha Mume
12. Mwanamke ni pambola Mwanaume, kama nyumba ikikosa pazia ni rahisi maadui kutambua vilivyomo ndani na kuvamia, ikikosa pazia hukaribisha maadui, Mwanamke ni pazia la nyumba ndiyo anayemtambulisha Mwanaume hata kama huyo Mwanaume ni mjinga Mwanmke anauwezo mkubwa wa kumuheshimisha Mwanaume mbele za watu, Mwanamke ndio mlinzi wa Mwanaume. Mwanamke anayejua wajibu wake hawezi kuibiwa Mume hata siku moja 
“Sifa ya Mwanaume ni Mwanamke aliye naye”.
16. Mbunifu
Mwanamke bora nimbunifu wa maisha, hayuko nyuma huweza kufanya kitu na hufanya, mbunifu wa biashara, mitindo ya mavazi, hubuni na kuwauzisha wafanyabiashara, ni mtundu wa maendeleo, mwenye wazo jipy huyu ndiye Mwanamke anayehitajika.
17. Mwenye nguvu na kuheshimika
Mwanamke bora ana nguvu za maendeleo mwenye mali inayopatikana katika mikono yake mwenyewe na mwenye kuheshimika jamii inameshimu kwa maendeleo yake, inamthamini, inamuogopa, ni kioo cha wa mama wengine katika jamii inayomzinguka, mke bora anaheshimika na watu, ukiona unadaraulika unatakiwa kubadilika maana Mke mwema ana nguvu katika jamii na anaheshimika huyu huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha ya leo.
18. Hucheka afikiriapo wakati ujao (Future)
Mwanamke bora hana hofu na wakati ujao maana amekweisha udhibiti wakati ujao, Mwamnamke bora hutawala kesho hata kama hajaingia, hutawala jioni wakati ni asubuhi hivyo hana hofu na mambo ya kesho, Mwanamke bora anaucheka umaskini, magonjwa na ujinga huandaa mambo yake kwa wakati aliopo na kwa wakati ujao, huyu ndio Mwanamke anayetakiwa asiyekuwa na wasiwasi na kesho.
19. Hufungua kinywa Kunena kwa hekima.
Mwanamke bora amejaa hekima kinyuani SOPHIA - hekima ni kiongozi mzuri sana katika maisha, ni mlinzi, hekima ni mtawala, hekima ni utajiri, hekima ni heshima, 
1. Mwanamke mwenye hekima hashindwi kuuitawala nyumba yake.
2. Mwanamke mwenye hekima hatishwi na watu na maneno yao.
3. Mwanamke mwenye hekima ni malkia wa nyumba yake, 
4. Mwanamke mwenye hekima ni mkombozi wa familia yake.
5. Mwanamke mwenye hekima ni muamuzi wa haki katika familia yake,
6. Mwanamke mwenye hekima ni mdhibiti wa maovu katika famila yake.
7. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa famila, 
8. Mwanamke mwenye hekima huondoa hasira kwa Mume wake.
9. Mwanamke mwenye hekima ni wa kujivunia, 
10. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa ndoa yake/ huyu ndiyeMwanamke anaye tafutwa katika maisha yetu rafiki wa wote huyu ndiye Mwanamke anayehitajika katika maisha.
20. Huwashauri wengi kwa wema.
Mwanamke bora ni mshauri mzuri kwa wengine, mwenye kushauri mema wala sio mabaya kwa watu waliomzunguka yaani ni mponyaji wa familia za watu wengi hata taifa, ushauri wake hauna madhara kwa watu, kimbilio la wengi, sio mwenye mwenye kuharibu ndoa za watu, mchonganishi, mshirikina, muongo hapana, Mwanamke anatakiwa kutoa ushauri mzuri kwa wengi huyu ndiye Mwanamke tunayemuhitaji wengi.
21. Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake.
Mwanamke bora anakuwa makini sana na kila kitu kinachoendelea au kutendeka katika nyumba yake anakuwa mwangalifu sana mna mambo ya nyumbani kwake kwa sababu yeye ndiye msimamizi mkuu wa nyumba yke, anatakiwa awe na muda wa kutosha na nyumba yake, hapendi ujinga nyumbani mwake, mahali pa kuonya anaonya, mahali pa kufundisha nafundisha, yeye ndiye mratibu mkuu wa yote yanayotendeka nyumbani, yeye ndiye kiongozi wa nyumba yake, mtendaji mkuu wa nyumba yake ndiye mjenzi wa familia bora hivyo Mwanamke kama huyu anyejua mjukumu yake ndiye anayetakiwa katika maisha yetu, sio kila Mwanamke umuonaye anafaa.
22. Kamwe hakai bure hata kidogo
Mke bora hakai bure lazima atakuwa na kitu cha kufanya, huwezi kumkuta kwenye vikao vya umbea, anazunguka zunguka kwenye nyumba za watu, maana ana mambo ya kufanya hakai bure hata kidogo ni mchapa kazi, anajituma, mbunifu wa mambo, anautaratibu wa maisha yake. Mwanamke ambaye yupo yupo tu huyo hatufai,ni chanzo cha matatizo, umbea, muongo, tafuta Mwanamke anayechapa kazi yuko (busy) na shughuri za kifamilia, kiofisi mwenye maendeleo huyo ndiye Mwanamke anayefaa katika maisha.
23. Watoto wake huamka na kumshukuru.
Mke bora watoto wake wanafuraha naye, wanamshukuru sana mama yao, maana amewajengea maisha mazuri amewafundisha mambo mazuri, amewalea vizuri, watamuheshimu sana mama yao na kumpenda, watamlinda na kumtunza mama , mama wa kweli husifiwa na watoto wake, watoto wanajisikia amani wanapokuwa naye, mwenye maadili mema mbele ya watoto wake,. Mfano wa kuigwa kwa mambo mazuri anayowatendea watoto wake hivyo shukurani hazitaweza kundoka midomoni mwa watoto wake huyo ndiye Mwanamke anayetakiwa.
24.Mume huimba sifa zake
Mke bora Mume wake humsifia kwa sifa njema Mume hutangaza uzuri wa Mke wake, hutangaza mtendo mazuri ya Mke wake, hujivunia na anajisikia bahati kuwa na mke kama huyo, mwenye tabia njema, mtiifu, mpole katika maisha yake mwenye kujiheshimu, anyempenda mume wake na watoto zake, msema kweli, mlinzi mwaminifu, Mwanamke mwenye maendeleo huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu aliyekubarika katika moyo wa Mume wake mpenzi.
24. Mwenye kumcha Mungu
Mke bora ni Yule mcha mungu anayempenda Mungu mtu wa Ibada mwenye hofu ya Mungu anayeichukia dhambi, mpenda maombi na Neno la Mungu huyu ndiye Mke sahihi katika maisha, mwenye mzigo wa maombi kwa ajili ya Mume wake na watoto wake na wote waliomzunguka huyo ndiye chemichemi ya mabadiliko ya familia, mleta ukombozi wa fmailia huyu ndiye Mwanamke anayefaa katika maisha yetu ya leo.
25. Mwenye kupenda elimu.
Mke bora ni Yule anyependa Elimu. Elimu imegawanyika katika sehemu mbili. Kuna Elimu inayopatikani mashuleni na Elimu inaopatikana katika mazingira unayoishi, wazazi na jamii iliyokuzunguka Mke bora anapenda kujifunza mazuri kwa wengine, mafanikio yao, sio mjuaji, yupo tayari kurekebishwa na kubadilika, anayekubari kushauriwa huyo ndiye Mwanamke anayefaa maana ni msikivu na mpenda mabadiliko yenye faida
26. Huandaa chakula kwa familia yake.
Mke bora ni mpishi mzuri wa chakula katika familia yake hategemei wafanyakazi yeye ni Mwalimu wa wengine mume humsifia Mkwa kwa mapishi yake mazuri nay a usafi wa hali ya juu sana . mpendwa najua unajua kuwa kuna baadhi ya wake za watu hawajui kupika, sio mbunifu wa mapishi mchafu katika maandalizi yake huwa ni wake wasio bora, wanavunja nyumba zao, tafuta Mke ambaye hana chakula cha kukariri bali bali ni mbunifu wa mapishi ni msafi anayejipenda mwalimu wa mapishi huyo ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu ya leo.
27. Mwenye sifa njema.
Mke mwema anasifa njema katika jamii iliyomzunguka hana tabia za uzinzi na uasherati, hana tabia ya ulevi na matusi, hana tabia ya umbea na uchonganishaji, hana tabia ya kiburi na jeuri Mke mwema ni rafiki wa watu wengi amejaa shukrani na hana mawazo mabaya Mke bora hutambulika na matendo yake katikajamii inayomzunguka.
28. Mwenye kudhamini na kutunza upendo.
Mke bora anajua maana ya upendo na gharama zake, anajua maumivu na vidonda vya mapenzi, anajua nguvu ya upendondani ya mtu, anatambua hisia kali ya upendo, Mwanamke wa namna hiyo hataweza kukusaliti, atakuheshimu na kukupenda kweli kutoka moyoni mwake hatagawa upendo wakko kwa wengine, atalinda penzi lake kwa ajili yako, anaheshimu mwili wake huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anayejua kwanini umempenda yeye na umewaacha wengine mwenye tabia njema. Huyu ndiye Mama wa familia bora sio bora familia.
29. Mwenye wivu wa maendeleo
Mke bora ana wivu wa maendeleo hana wivu wa kijinga unaoweza kusababisha amani katika ndoa kuondoka .Mwanamke ni mponyaji wa ndoa yake ni kweli Mwanamke anatakiwa awe na wivu kwa Mume wake lakini vilevile lazima awe na Imani na Mume wake, kuna wivu unaoweza kuharibu amani ya nyumba lakini kuna wivu unaoweza kujenga nyumba. Inategemea Mama ana wivu wa namna gani sio wote walio karibu na Mume wako, wako katika mahusiano na Mume wako, Mwanamke bora hufanya utafiti wa jambo na kuwa na uhakika naolo na huliwasilisha kwa hekima sana. Wivu ni mzuri ukitumiwa vizuri na pendo la kweli lina wivu lakini uwe wa maendeleo katika maisha yenu.

Kumpata Mwanamke bora sio kitu rahisi lakini kupitia mafundisho ya vitabu vya Mungu, vitafungua ufahamu wako mkubwa na kumtafuta Mke sahihi kimungu.

KWA WADADA! Dalili 8 za mwanaume mwenye aibu na amekuzimia na Hataki kukwambia

Ukweli usemwe. Kila mwanamume ameumbwa kivyake. Kuna wale ambao mambo yao hupenda kuyaweka wazi na wengine ambao mambo yao hupenda kuyatia kikapuni. Kuna wale ambao hawapendi kujionyesha hadharani na kuna wale ambao mambo yao huyaweka kimbelembele.
mwanaume mwenye aibu

Tukija maswala ya kutongoza, kuna mitindo tofauti tofauti ambayo wanaume hutumia ili kufaniikisha lengo lao. Kuna ule msemo unaosema 'mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani, yaani unaweza kufuata njia tofauti tofauti kufika pahali lakini mwishowe utarudi pale pale sehemu moja, so kwa wanaume kila mmoja ana mbinu yake ya kutongoza. Usiwahi kusema kuwa mwanamume aibu hajui kutongoza akiwa na wewe, labda hio aibu yake ni moja wa mtego aliouweka spesheli wa kukunasa wewe.

So utajuaje kama mwanaume mwenye aibu amekuzimia lakini hataki kuonyesha?

1. Anaingiwa na wasiwasi akiwa na wewe
Ukiona mwanaume anaingiwa na kibaridi ama kupapatika akiwa kando yako ujue ni ishara ya kukuambia kuwa amekuzimia. Hii inatokea wakati mko pamoja halafu anaingiwa na wasiwasi mara anafanya hivi mara vile. 
2. Anapenda kuulizia marafiki zako kukuhusu
Mwanaume mwenye aibu akikupenda huwa anataka kukufahamu zaidi kukuhusu. Iwapo atashindwa kuongea na wewe moja kwa moja basi ataanza kuwaulizia marafiki zake kukuhusu. Ukiona mwanaume ana tabia kama hii ya kuulizia marafiki zako, lile la kufanya nikuonyesha ishara za kuwa uko huru kuongea nayeye wakati wowote ule anapojiskia huru.

3. Anakuwa na tabia isiyoeleweka akikuona
Owk wakati mwingine inatokea ya kuwa mwanaume mwenye aibu anashindwa kustahimili kuonyesha hisia zake hivyo kujaribu kuzificha ili usiweze kuzitambua. Lakini badala ya kuzificha, huibua tabia nyingine ambazo hazina mfanano wa kwake. Usishtuke ukiona akifanyika mambo ambayo si ya kawaida manake wewe ndio chanzo kikuu cha kufanyika hivyo. Yaani utakuwa umempagawisha kiasi cha kuwa anaweza kuanza kuchora miduara kwa mchanga akitumia miguu yake.

5. Anapenda kutabasamu na wewe
Wanaume wote kawaida wakipendezwa na mwanamke huwa wanatabasamu. Lakini kwa mwanaume mwenye aibu aliyekupenda huwa tabasamu lake ni tofauti. Mara nyingi atakuwa akitabasamu lakini mara kwa mara anashindwa kukuangalia usoni. Labda anaweza kukuangalia lakini pindi utakapomuangalia yeye atajifanya anaagalia kando. Hii ni baadhi ya tabia ya wanaume wa aibu hufanya wakati anapojaribu kukupendeza.

6. Anakuwa kimya ukiwa naye
Anaweza kuwa anaongea na marafiki zake sehemu flani, lakini pindi utakapotokea ananyamaza kabisa ama kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka. Hata usishangae iwapo atakataa kujibu salam zako kama umempata katika hali kama hii. Mara nyingi ukimkuta akiwa na maongezi na marafiki zake, atajifanya hata hakuwa akizungumza katika kuchangia maongezi.
7. Anabadilisha mwonekano wake
Ukiona kuwa mwanaume mwenye aibu ameanza kubadilisha mionekano yake kwa kuanza kuvalia nguo tofauti, mitindo mipya ya nywele nk akiwa na wewe, jua hii ni ishara ya haraka kuonyesha kuwa amekuzimia.  Kufanya hivi kwa kawaida ana makusudio ya kukuridhisha wewe. Labda anadhania ya kuwa kuna mtindo fulani ambao akiuvaa unakupendeza.

8. Anagugumiza akiongea na wewe
Mwanaume huyu hujamsikia akikwamakwama wakati anapoongea lakini ghafla unamskia akigugumiza anapoongea na wewe. Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa anaishiwa na maneno ya kukuambia na inakuwa vigumu kwake kuyatoa ama kutafuta maneno ya kukuambia.


So ni kitu gani kinachowafanya wanaume aina hii kuwa spesho kwa mwanamke?
Kuna wanawake ambao wanapenda wanaume ambao ni wa aibu kwa kuwa hawana mambo mengi. Lakini usishangae kumwona mwanaume aina hii akikuapproach akutoe mkale bata pamoja. Pia aina hii ya wanaume itafikia wakati fulani wanaweza kukushangaza kwa kufunguka na kugundua kuwa ilikuwa tu ni baadhi ya mbinu waliyotumia kukuteka kimapenzi.

MFANYE MWANAMKE AJIBU TEXT ZAKO ATAKE ASITAKE....MBINU HIZI HAPA


  
Unafukuzia mwanamke mzuri mnaanza kuzungumza. Mnachukua muda wa dakika 20 hadi 30 kuongea na yeye mara ya kwanza. Anapendeza na kuvutia, na unaona kama ni mwanamke ambaye ni yule aliyekuwa ndotoni mwako maishani mwako. Mazungumzo yenu yanaenda vizuri mpaka ukwamwomba namba yake. Baadaye unajaribu kumtumia text na hazijibu. Labda mnaeza kuchat kwa madakika halafu baada ya hapa anakataa kujibu texts zako. Unabaki ukijiuliza maswali ni kitu gani ambacho umefanya ambacho umekosea. Ok labda anaweza kuwa yupo buzy unampa muda kiasi ajibu text zako...unangojea masaa, siku, wiki mpaka inafikia wakati unagundua kuwa amekupuuza. Kwa nini hajajibu text zako?

So kwa nini hakujibu text zako?
Katika situation nyingi ni kuwa sababu kuu ambayo amekataa kujibu texts zako ni kuwa haukumpendeza mara ya kwanza ulipokutana naye. Ok labda sababu nyingine inaweza ni kuwa ameibiwa simu yake wakati alipokuwa akitext na wewe barabarani ama kitu kingine kama hicho, lakini hapa acha tumakinike na hatua ya kwanza uliokutana naye...yaani first impression ambayo unakudana na mwanamke yeyote.

1. Hakikisha unampendeza mara ya kwanza unapokutana naye
Anaweza kuwa hana muda mrefu wa kukaa na wewe ili akutambue zaidi so kile kitu ambacho unahitaji kufanya ni kuwa lazima uuonyeshe upendo wako kwa kuwa mpole, mkarimu na mtulivu. Hii itamfanya yeye kumakinika na labda kutaka kukufahamu. Hakikisha kuwa wakati unapoongea na yeye tumia mbinu za kuonyesha kuwa ungependa kukutana na yeye wakati mwingine. Kama hakuonyesha dalili zozote za kukuelewa basi hata kama atakupatia namba yake ya simu fahamu ya kwamba itakuwa ni kazi bure. [Soma: 
2. Taja sababu zako za kuongea na yeye
Mfano: Nimefurahia sana kuongea na wewe. Kusema kweli nimependa maonezi yetu machache. Nataka kwenda lakini naonelea wikendi nitakutext tukutane ili tuongee tena. Hapa utakuwa umeeleza ajenda yako kwake hivyo ukianza kuchat na yeye baadae haitakuwa vigumu kwake kukujibu.

3. Hakikisha kuwa unamtumia text wakati ufaao
Ukiomba namba ya simu kwa mwanamke inamaanisha kuwa wewe umeonyesha intrest kwake vilevile mwanamke akikupatia namba yake ya simu inamaanisha kuwa labda itakuwa amependezwa na wewe. Lakini je, ni muda upi unaotakikana hadi umtext mwanamke huyo.
Wanawake wanapenda kuona wanababaikiwa na kufukuziwa. So usijaribu kumtext hapo hapo wakati amekupatia namba yake. Hakikisha umejibatia shughli nyingi ili usahau kabisa kama uchukua namba kwa mwanamke. Masaa mazuri ambayo yangekuwa sawa ya kumtext ni baada ya masaa 24 baada ya kuchukua namba yake. Hii itamfanya mwanamke yeyote kujiuliza maswali ya kwa nini umechukua muda mrefu kumtext. Itamfanya kuingiwa na maswali ya kama: kwani hajapenda chat yangu? yuko na mwingine? nk. Ukichukua muda huu mrefu hadi kumtext, itakuwa rahisi kwake kukujibi.
 ONYO: Hakikisha ya kwamba haupitishi zaidi ya siku tatu kwani anaweza kukusahau kwa haraka ama kuona unampotezea wakati wake.

4. Kitu cha kuandika kwa text yako ya kwanza
Messages za kwanza ambazo utazituma kwa mwanamke zitachangia pakubwa kuona kama wewe uko uko interesting ama unaboa. Unaweza kuuharibu mchezo mzima kama iwapo utaanza kumtext na mambo ambayo hayana manufaa kwake. Kile kitu unachohitajika kufanya hapa ni kuonekana hauna haraka na ujaribu kutumia lugha za kirafiki. Mfano unaweza kujaribu kumtext swala ambalo aliligusia kwa chat iliyopita. Labda aliongea kuhusu kwenda shopping na nduguyake, so swali lakini linaweza kuwa: Je ile shopping yenu na nduguyako iliendaje?. Hii itamfanya kuwa interested na wewe manake ataona ya kuwa ulikuwa umemakinika wakati mlipokuwa pamoja. Hii itamfanya kujibu text zako mara kwa mara bila yeye kuchoshwa.

5. Jaribu kuhepa stori ambazo hazitafikia popote
Mara ya kwanza anaweza kukujibu lakini itafikia pahali atanyamaza. KUMBUKA: Siri kuu ya kumfanya mwanamke ajibu texts zako ni uwe makini kwake, yaani unamtext vtu ambavyo unajua yuko intrested navyo.

6. Weka wazi kuwa unataka mkutano
Acha stori za kumzungusha huku na huku kama wanaume wengine. Ukitaka akujibu text zako hakikisha ya kuwa unadhihirisha azma yako kwa kumwambia kuwa unataka kukutana naye.

7. Usikate tamaa
Kuna wanaume wengine kama wamekataliwa kujibiwa texts zao mara moja basi wanakasirika na wanaachana kabisa na kushungulika tena. Tatizo labda linaweza kuwa mwanamke anakupima akili aone bidii yako kwake. Kama tujuavyo tabia za wanawake ni kuwa hawapendi kuonekana kama ni watu wa kukubaliana na kila kitu hivyo basi wakati mwingine wanakuwa hawaeleweki. 
Ukiona mwanamke amekataa kujibu text yako kwa siku tatu, fanya kumtext tena huku ukionyesha kuwa hauna intrest naye sana vile halafu achana naye. Hii itamfanya yeye kuona una interest na yeye lakini hauna haraka. Baadaye anaweza kuanza chat yeye mwenyewe.
KUMBUKA: Kuna sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukataa kujibu texts zako. Labda umemtusi, hujampendeza, ni mwanamke mwenye haya nk. So hizi hatua zitategemea na vile imetokea katika situation yako.

MAANA YA HERUFI ZA MWANZO ZA MAJINA YENU



A; Haraka, Pupa ya MaishaWenye jina linaloanza na herufi ”A” ni Watu wanaopenda mambo makubwa, Wanajiamini, na wenye uwezo wa kutimiza malengo yao, Ni watu wenye tahadhari Katika kila jambo, Wachangamfu na wanaopenda Matukio. Wanapenda kuheshimiwa, Wanapenda mamlaka, Wana kiburi na ni Watu wenye hasira.
B; Inawakilisha Kazi, Pesa, Mapenzi, Ujenzi.Wenye jina linaloanza na herufi “B” ni Watu Wakarimu , Waaminifu na Wenye kupenda kazi. Ni watu Jasiri, Shujaa na Wakatili katika vita au pale wanapotaka kulinda vyake au vilivyo katika himaya au Mamlaka yao.
C; Inawakilisha Vurugu, Ndugu, Kuchanganyikiwa.Wenye jina linaloanza na herufi “C” ni Watu wa kubadilika badilika, Washindani, na hupenda kupigania Malengo yao wanayoyapenda. Ni watu Wabunifu, na wanaopenda Mawasiliano.
D; Inawakilisha Upole, Kuchelewa, Wazee, Cheo.Wenye jina linaloanza na herufi “D” ni Watu wanaopenda Usawa, na Kufanya Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na wenye kupenda Usafi. Ni jeuri na wenye Msimamo.
E; Inawakilisha Kisomo, Maendeleo, Watoto.Wenye jina linaloanza na herufi “E” ni Watu wenye roho nzuri, Wenye mapenzi, wenye huruma, wenye kupenda uhuru katika mapenzi na wachangamfu sana. Kinyume na hivyo ni watu wasiotegemewa na vigeugeu. 
F; Inawakilisha Kusahau, kupoteza,Kusoma mbali.Mwenye jina linaloanza na herufi “F” ni Watu wenye mapenzi, huruma, Roho nzuri na Uwezo wa kuwafariji watu. Ni Watetezi wa Watu na wenye huzuni na hisia kali wanapoudhiwa, Lakini ni wazito sana kufanya maamuzi ya haraka.
G; Inawakilisha Ndoa, kuunganisha,Mikutano, kufuzu Baada ya Ndoa.Mwenye jina linaloanza na herufi “G” ni Watu wenye Imani ya kidini na nguvu za kiroho, Wana Vipaji vya kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni watu wenye hisia kali, Wanaopenda kusoma au kujiendeleza, wakati mwingine wapenda upweke, na wakaidi kukubali ushauri wa watu wengine.
H; Inawakilisha kupoteza, kupata tena,Mafanikio, kutumia nguvu au kesi au vurugu.Wenye jina linaloanza na herufi “H” ni Watu wenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na nguvu zao binafsi, ni watu wanaojituma sana. wenye mawazo na fikra nyingi mengi lakini wana udhaifu wa kuwa wachoyo na wabinafsi.
I; Inawakilisha kubadilisha, kubadilika,kusafiri, Ugenini.Wenye jina linaloanza na herufi “I” ni Watu wenye kupenda Sheria na Mpangilio, wana Huruma na Utu. Ni Viumbe ambao wanajiamini sana katika mambo yao lakini wana hasira za Haraka Haraka.
J; Inawakilisha kuongoza, Siasa,Biashara, Ukubwa.Wenye jina linaloanza na herufi “J” ni Watu Wenye matamanio, Wakweli, Wakarimu, Waerevu na Wajanja, Wasiokubali Kushindwa na kutokana na tabia yao hiyo Hupata mafanikio Makubwa. Kasoro yao ni kwamba kuna wakati wanakuwa wavivu na waliokosa mwelekeo.
K; Inawakilisha kufuzu, kupitia,rafiki, kuungana.Wenye jina linaloanza na herufi “K” ni Watu wenye Ujeuri, wenye msimamo thabiti, Mashuhuri na wenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za Watu, wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengine hawana. Ni watu wasioridhika na hali ya kimaisha.
L; Inawakilisha kupingwa, kupingana,mafanikio baada ya shida na Safari.Wenye jina linaloanza na herufi “L” ni Watu wa Vitendo, wenye hisani na wanaopenda kujipanga vizuri kimaisha, wajihadhari na ajali za mara kwa mara kubwa na ndogo.
M; Inawakilisha Mabadiliko baada ya kurejea au baada ya Talaka.Wenye jina linaloanza na herufi “M” ni Watu Wenye kujiamini sana, wachapa kazi na hupata mafanikio, Ni watu waropokaji, wenye haraka na wepesi sana kukasirika.
N; Inawakilisha kukwama kipesa,mafanikio baada ya kurejea kazini au nyumbani.Wenye jina linaloanza na herufi “N” ni Watu wenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana, kasoro yao kubwa ni kwamba wana wivu sana.
O; Inawakilisha Uzazi wa watoto, kuleta bahati, Ushindi kimchezo au kimasomo.Wenye jina linaloanza na herufi “O” ni Watu wenye subira, wavumilivu na wenye bidii ya kusoma. Ni watu wenye kupenda kutumikia jamii na wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
P; Inawakilisha kupotelewa, Kuuguliwa, Wizi na Masomo ya Juu.Wenye jina linaloanza na herufi “P” ni Watu wenye Uwezo wa kuamrisha na Hekima Kubwa. Wana nguvu za kiroho lakini wanapenda sana kujitumbukiza katika mambo ya watu.
Q; Inawakilisha Ndoa, kufuzu baada ya kurejeanaWenye jina linaloanza na herufi “Q” ni Watu wenye kupenda mambo ya asili, Ni watu wasiolezeka au kutambulika tabia zao kirahisi na wana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana, hata hivyo ni watu walioopooza sana.
R; Inawakilisha Kuporomoka na kupata nguvu, kusafiri mbali na kushinda.Wenye jina linaloanza na herufi “R” ni Watu wenye Uvumilivu, wenye huruma lakini wana hasira za haraka, muda wote wanakuwa ni watu wanaopenda Amani na hawataki ugomvi.
S; Inawakilisha kufuzu Ugenini, Kupata mali na Magari.Wenye jina linaloanza na herufi “S” ni Watu wenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya Ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
T; Inawakilisha Kupata Utajiri na kujenga, Kesi, baadae kushinda Wenye jina linaloanza na herufi “T” ni Watu wenye kupenda ushauri wa kiroho, wanatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na wepesi kushawishika.
U; Inawakilisha Ushindi wa Pesa, Kunyanganywa mali na Kesi za mara kwa mara.Wenye jina linaloanza na herufi “U” ni Watu wenye bahati kubwa kwa ujumla, wanapenda uhuru katika mapenzi, lakini ni wabinafsi wenye tamaa na waliokosa maamuzi
V; Inawakilisha Utajiri wa Bahati Nasibu, kupewa, kuokota na ndoa nyingi. Wenye jina linaloanza na herufi “V” ni Watu wachapa kazi wenye bidii na wasiochoka, hata hivyo ni watu wasiotabirika.
W; Inawakilisha, Pesa, Kazi, ni rahisi kusaidia watoto wengi. Wenye jina linaloanza na herufi “W” ni Watu wawazi na wachangamfu kupita kiasi na wenye uwezo wa kumtambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye Tamaa na hufanya mambo ya hatari. 
X; Inawakilisha Kupata uzazi, Kupata jengo na UtajiriWenye jina linaloanza na herufi “X” ni Watu wasiopenda kuwekewa vipingamizi katika mambo yao, wanapenda anasa na ni rahisi kujiingiza katika mambo yasiyofaa na kujitoa uaminifu.
Y; Inawakilisha Kupata Bahati, Uandishi, Watoto na Uongozi.Wenye jina linaloanza na herufi “Y” ni Watu wenye kupenda uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na huwasababishia wao kupoteza bahati zao katika maisha.
Z; Inawakilisha kuuguliwa Watoto, vitu kupotea, Shida za Pesa na Kazi.Wenye jina linaloanza na herufi “Z” ni Watu wenye kupenda matumaini na Amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.

JE WAJUA? ;Wanawake Wengi Hupenda Kudanganya Mambo Haya?

post-feature-image
Najua sio raisi kukubali haya, lakini kuna aina ya wanawake ambao ni waongo sana, na hiyo inajulikana, hata kuwashinda wanaume ambao inajulikana wao ndo wajanja katika kudanganya kuliko wanawake, lakini leo tutaangalia vipengele ambavyo wanawake wengi huwa wanadanganya sana.

Umri

Wanawake wengi wanaamini wanaume wanavutiwa na wanawake wenye umri mdogo, wanawake walio na miaka kati ya 24-29 mara nyingi huwa wanashusha miaka 2 hadi 3 ili waonekane wadogo mbele ya wanaume.

Kutokuwa Na Mahusiano

Baadhi wa wanawake, husema wapo kwenye mahusiano hata kama hawapo,hii inatokea hasa kama mwanamke hamtaki mwanaume aliemtokea wakati huo na kisingizio kikubwa ni yeye kuwa katika mahusiano na huu ni uongo mmoja maarufu sana na Baadhi ya wanawake pia huwa wanaficha kama wapo kwenye mahusiano, hasa pale wanapotaka kuanzisha mahusiano mapya, huku wakiendelea kuwa na mahusiano na wanaume wawili kwa wakati mmoja.

Mara ya mwisho kukutana kimwili na mwanaume

Mwanamke hawezi kukwambia ukweli kuhusu hili hata kama alikutana na mtu kimwili jana, atakwambia miezi 4-8 iliyopita, hii ni kwasababu anaona ataonekana muhuni sana au Malaya, na wengi wao huwa wanataka kuonekana wasafi au tuite watakatifu. Kitu ambacho sio

Ameshakuwa na wapenzi wangapi

Uongo mwingine ambao ni maarufu ni kuhusiana na mwanaume wangapi ametoka nao, hapa sahau sana kwani huwezi kupata jibu sahii, sababu wanawake wengi huwa wanadanganya mahusiano yao ya nyuma, anaweza kukwambia wawili au watatu kitu ambacho inaweza kuwa zaidi ya hao. Japokuwa uongo huu hata wanaume pia wanadanganya

Kudanganya kuhusu vitu alivyozoea

Wapo wanawake wanadanganya kuhusu kutoka usiku, labda sio watu wa tungi/Gambe, sio watundu kitandani na kujidai ndo kwanza kuna mambo wanayaanza siku hiyo. Kujidai hawawezi hiki mara kile mara akwambie mie ndo mara yangu ya kwanza ilimladi vituko.

KWA WANAWAKE TU! Njia 14 Za Kujiweka Ili Wanaume Watamani Kukutongoza

Je umekuwa ukijiuliza kwa nini haukuwi approached na wanawaume kama unavyotaka? 
Owk....
Kando na itikadi ambazo umekuwa ukifikiria, kuapproachiwa ama kufukuziwa na mwanaume si gemu ya bahati nasimu ambayo mtu anaingojea ijitokezee.
Na pia kando na itikadi nyingi za wanawake wanazozifikia, si lazima ufanye kitendo kikubwa ama cha inadi ili mwanaume aweze kukutongoza.
Ukweli ni kuwa, kama unaielewa akili ya mwanaume na jinsi inavyofanya kazi kabla ya kuapproach mwanamke, unaweza kumfanya mwanaume yeyote kutaka kuongea na wewe dakika tano atakapokuja katika himaya yako.
So mbinu zenyewe ndizo zipi?
Zama nami...

Njia za kujiweka ili mwanaume apate nafasi rahisi ya kukutongoza

Kwanza jiweke nadhifu
Hii ni muhimu katika yote kama wataka mwanaume akutambue. Mwanaume kitu cha kwanza anachokiangalia huwa ni mwonekano wa mwanamke. Mwanaume anapoingia katika chumba, inamchukua sekunde ndogo zana kuamua iwapo anataka kuapproach mwanamke mfani au la.
Kama umevalia vizuri na unapendeza, itarahisisha kazi yako sana.
Pili usionekane kama una shughli
Usijishughlishe sana na simu yako, ama kitabu chako, ama kitu kingine. Unaweza kuwa umeboeka na unajaribu kujiweka buzy, lakini fursa iweza kuwa hivi, kufanya hivyo kunaweza kumfanya mwanaume anayetaka kukuapproach kuona ya kuwa uko buzy sana kiasi cha kuwa atashindwa kukufuata kwanu unaweza usiwe interested na maongezi yake.
Tatu ni kuwa mko ligi moja?
Hii inakinzana na hatua ya kwanza, lakini inaweza kuwa na tatizo iwapo unaoneka kama uko ligi tofauti na mwanaume. Kama utaoneka amakujiweka mtu wa hadhi ya juu wanawake watapenda kukuangalia lakini hawatakuaproach. Hii ni kwa sababu wanaume wengi hawapendi kudhalilishwa wakati wanapoamua kukuapproach....kiufupi ni kuwa ukiwa unavutia kupindukia wanaume watakuogopa.
Lakini tena, kuna wale wanaume ambao wanajiamini kupindukia ambao wanajua thamani ya kukuapproach, nao ni wanaume alfa, wanaume diriki, na pia wale wanaume mapleya.
Kama wataka kuteka atenshen ya mwanaume mzuri wa kawaida lakini anayeogopa kukuapproach, jaribu kutumia mbinu ya kuwa jamili na watu wanaokuzunguka. Huwa inasaidia.

Ujanja wa kumfanya mwanaume aweze kukuakuaproach

1. Jinsi utakavyovalia
Usivalie kana kwamba huna kitu cha kuficha. Utapata atenshen ya kila mtu lakini wanaume ambao wataamua kukuapproach ni wale ambao wanataka kulala nawe kwa usiku mmoja pekee. Enyewe kuvalia kwa kutamanisha kunasaidia kuteka atenshen ya mwanaume, lakini usivuke mipaka ya kawaida.
Kumbuka kuwa si lazima uonyeshe viungo vyako vyote vya mwili ili uweze kuteka macho ya mwanaume. Kama unavutia inatosha kumfanya mwanaume akugundue.
2. Unavyomuangalia
Mchungulie mara moja na nyingine, halafu mwangalie mara kwa mara. Hakikisha ya kuwa haujisahau ukamwangalia sana kupindukia ama atakuona kama wewe ni rahisi wa kuapproach na anaweza kukupuuza.
3. Mitindo ya kumwangalia
Kuna mitindo miwili mikuu ya kumwangalia mwanaume ili kumuonyesha ya kuwa umevutiwa naye. Unaweza kutumia mbinu zote mbili kulingana na vile unataka.
i) Kumwangalia polepole - wakati ambapo unaangalia pande zote, angalia upande wake na uyaangalie macho yake kwa sekunde kadhaa huku ukiweka tabasamu. Halafu pole pole zungusha kichwa chako uangalie kwingine. Mbinu hii ni ya kijasiri ya kumwonyesha mwanaume umevutiwa kwake.
ii) Kumwangalia kwa uharaka - hii ni mbinu ya kumwangalia kwa uharaka. Anza kumuangalia, ukiona kama anataka kukuangalia, ghafla angalia kando halafu utoe tabasamu ukiangalia chini. Mbinu hii inampa confidence na kukuona wewe ukipendeza.
4.Mfanyie kazi iwe rahisi
Inakuwa vigumu kwa mwanaume kumuapproach mwanamke sehemu ambapo yuko kundini na marafiki zake. Kama mawazo yako ni kufuatwa na mwanaume, hakikisha ya kuwa wakati mwingine unajipa time ukiwa pekeako ama zaidi uwe na rafiki yako wa kike mmoja.
5. Sehemu zifaazo
Si kila sehemu ni nzuri kufanya maongezi na mtu. Kama unataka mwanaume akuapproach, chagua sehemu ambayo si kila mtu ataanza kujeuza kichwa chake kutaka kujua ni nini kinachoendelea kati yenu. Sehemu za mkawahawa, supermarket, ama bookshop ni sehemu nzuri zaidi za kukutana na mwanaume kupiga stori.
6. Mpatie nafasi aongee na wewe
Hata kama uko katika group na marafiki zako halafu mwanaume akakugundua, mwonyeshe interest kwa kumuangalia kwa madakika. Ukiona kama yuko tayari kuongea na wewe, unaweza kujitenga na marafiki zako kwa muda. Aidha unaweza kuanza kuzunguka hio sehemu kiasi ama unaweza kujipeleka mahali ambapo itakuwa rahisi kwa mwanaume huyu kuzungumza na wewe.
7. Tabasamu
Onekana jamili, na nafasi ya wewe kufuatwa na wanaume itaongezeka mara dufu. Kupendwa kwa mwonekano wa kwanza ni kama baraka kwa mwanamke yeyote yule ambaye anataka macho ya mwanaume yamwone.
8. Usiboe
Kuwa mwanamke mwenye furaha na mwenye hisia chanya mahali popote pale utakapokua. Mwanamke mwenye shangwe huvutia mwanaume yeyote yule. Kama utaonyesha chembechembe za kuboeka, mwanaume anayetaka kukuapproach anaweza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwani ataona ya kuwa maisha yako huboesha na yasiyo na mwanga.
9. Usiwe mjeuri
Kama wewe ni mjeuri kwa yeyote, aidha weita ama mmoja wa rafiki yako, inaweza kutokea kuwa mwanaume ambaye anapania kukuapproach kusimamisha ari yake. Hakuna mtu anapenda mtu mjeuri, na hakuna mwanaume angependa kuapproach mwanamke ambaye anaweza kumpuuzia ama kumkataa.
10. Usitangamane na wanaume
Hii ni muhimu kwa mwanamke yeyote aelewe. Usiwahi kamwe kutangamana na marafiki zako wa kiume kama unataka kukuwa approached na mwanaume. Haitafanya kazi kamwe.
11. Mwoneshe kuwa uko intrested
Mwonyeshe kuwa uko interested kwake kwa kutaka kumjulia hali zaidi. Hata kama uko na marafiki zako mnaongea halafu amekaa karibu na wewe, mwangalie iwapo anakuangalia hata kama unawajibu rafiki zako.
12. Onyesha uanawake wako
Mwangalie mara kwa mara, halafu ukishika macho yake, peta nywele zako nyuma ya sikio lako. Inaweza kuonekana kama jambo dogo kwako, lakini kwa mwanaume ni kama kugonga ndipo.
13. Mtege
Pita mbele yake halafu mwangalie machoni mwake wakati unapompita. Mtese kihisia, ataipenda kuona atenshen yake.
14. Usilazimishe
Utakuwa unajiaibisha iwapo unalazimisha mambo. Wanaume si mabubwi, hivyo ukiwaangalia mara moja na nyingine ama kuwatabamia, wanajua kuwa uko tayari kuapprochiwa.
Ok hizi ni mbinu ambazo unafaa kuzitumia kama unataka mwanaume yeyote yule akunotice ama akufukuzie.