Saturday, July 14, 2018

Urembo: Jinsi ya kuifanya ngozi yako kuwa na afya na mng'ao kwa kutumia vitu vya asili


Uzuri wa ngozi sio rangi tu bali ni muonekano wa ngozi yenyewe kwamba ina afya na mng'ao unaoashiria afya njema.
Leo tushirikishane jinsi ya kufanya facial treatment kwa kutumia vitu vya jikoni kama kiini cha yai,machicha ya nazi,tango na limao.Treatment hii inaweza kufanyika Mara moja kwa wiki au kila baada ya wiki mbili, unaweza kufanya hata mara moja kwa mwezi ukipata nafasi kama unakuwa busy sana lkn matokeo mazuri utayashuhudia.

JINSI YA KUFANYA

  • Andaa maji masafi yenye joto kiasi unachomudu ktk ngozi yako, osha uso wako kwa hayo maji safi .
  • Kama una ngozi kavu au ya kati chukua kipande cha tango kidogo na upake yale maji yake usoni, kwa wenye ngozi ya mafuta unaweza kutumia kipande cha limao kwa kupaka maji yake. Chukua pamba au kitambaa laini na futa maji ya matunda usoni kwa mtindo wa kusafisha taratibu usoni.
  • Chukua machicha ya nazi na Anza kuusugua uso  na shingoni taratibu Mpaka uridhike uso wote umepitiwa na machicha yako hasa unapoona unang'aa kwa mafuta kidogo yaliyotoka kwenye nazi. Kisha pukuta yale machicha ubaki na uso unaong'aa bila vitu vyeupe yaani machicha.
  • Chukua kiini cha yai inapendeza ukitumia la kienyeji, au la kisasa lenye kiini cha njano iliyokolea angalau. Ili kiini kisijichanganye na ute wakati wa kupasua ,ligonge yai upande mmoja sio katikati na limimine ktk chombo mithili ya sahani ambayo unaona kiini katikati kisha unakichota na kuweka kando. Paka ule uji mzito wa njano wa kiini uso mzima bila kusahau shingoni na nyuma ya masikio na ngozi ya masikio.
  • Baada ya kupaka kiini cha yai unaweza kuendelea na shughuli zako huku likiendelea kukauka,linapokauka ngozi yako inakuwa kama inajivuta vuta.
  • Baada ya kule kuvuta kuisha inamaanisha yai limekauka kabisa. Osha uso wako kwa maji safi maji yawe ya baridi sasa.

JINSI INAVYOFANYA KAZI

  • Kuosha uso kwa maji yenye joto kunafungua matundu ya ngozi.
  • Tango au limao hutumika kama cleanser, unapokuja kujifuta taratibu unaondoa uchafu katika ngozi yako.
  • Machicha ya nazi yanatumika kama scrub, yanaondoa seli zilizokufa, kuifanya ngozi kuwa laini na kuipa mngao.
  • Kiini cha yai hapa kinatumika kama maski, matundu ya ngozi yanajifunga vizuri na kinaipa ngozi yako lishe kutokana na vitamins zilizomo kwenye kiini cha yai kama vitamin E.
  • Mwishoni unanawa na maji baridi ili kuruhusu matundu ya ngozi kujifunga na kuifanya ngozi ijiweke sawasawa.

FAIDA ZA HII TREATMENT

  1. Husaidia kutibu na kuikinga ngozi na chunusi,
  2. Kuipa ngozi mng'ao bila kutumia kemikali za sumu,
  3. Husaidia kupunguza mikunjo ktk ngozi yako(wrinkles zinapungua)
  4. Gharama ndogo kuifanya