Kua na ngozi laini na yenye afya ni matamanio ya kila mtu, bahati mbaya hakuna uchawi katika hili, ili uwe na ngozi inayovutia na nzuri lazima ufuate kanuni za afya ikiwemo kufanya mazoezi kunywa maji mengi na kula vyakula vinavyotengeneza ngozi yako kuwa nzuri..
Vyakula vingi ni vizuri kwa afya ya binadamu lakini leo nataka kuongelea vyakula vinavyofanya baadhi ya ngozi za watu kua laini sana kulio wengine, wasanii marufu wa nje na ndani ya nchi hutuhumiwa sana kwa kutumia kemikali kuboresha ngozi zao lakini sio kweli na hii ndio siri yao.
Maparachichi: haya ni matunda ambayo yamekua yakifahamika miaka mingi kwa kuboresha ngozi, tunda hili lina vitamin e, potassium, folic acid na mafuta. Mchanganyiko huu hufanya ngozi kua laini sana na kupunguza uwezekano wa magonjwa ya moyo na kiharusi.
Machungwa: haya yana maji mengi ambayo huupa mwili maji na vitamin c ambayo ni moja ya vitamin nzuri sana kwa ngozi ya binadamu.
Zabibu; matunda haya huongeza maji mwilini lakini kazi yake kubwa ikiwa kuzuia madhara ya jua ambayo yanatokea kwenye ngozi..
Samaki; tafiti mpya zimeonyesha kwamba omega 3 ambayo inapatikana kwenye samaki huuzuia seli za kansa kusambaa mwilini na kuifanya ngozi kua laini kama ya mtoto mdogo…
Mboga za majani; hizi ni kama mchicha, spinachi, matembele na zingine nyingi za kijani zina mchanganyiko wa vitamin A, C, K ambazo pia huongeza kinga ya mwili na kuuia madhara makali yatokanayo na mwanga wa jua..