Tuesday, October 29, 2019

HII NDIO APP YETU MPYA AMBAYO TUMEIFANYIA MABORESHO INA STORI NYINGI SANA


KWASASA UNAWEZA KUPATA ZILE STORI TAMU ZA MAPENZI KWENYE APP YETU MPYA UNAWEZA UKAIPAKUA SASA BONYEZA HAPA INAITWA KIJIWE CHA MAPENZI TWENDE HUKO KUNA STORI KIBAO 

Saturday, July 20, 2019

MAMBO MANNE YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA

Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia. Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa. Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa. Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano. Kuoga pamoja
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi. Kusifiana


Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako.
Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza. Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo. Kuelekezana
Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika. Zungumzieni maisha
Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa. Yapo mnayotakiwa kuyaepuka ili kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja kuyaeleza katika makala zinazokuja kupitia ukurasa huu.

Friday, December 21, 2018

Natumaini muwazima bukheri wa afya na mnaendelea vyema na mishemishe zenu za kimaisha kama kawaida. Mimi namshukuru Mungu niko poa tayari kuwaletea mada ambayo nimewaandalia kwa wiki hii.Leo nimeona nikuletee njia kumi ambazo unaweza kuzitumia katika kukabiliana na wivu uliopitiliza ili uweze kudumu na huyo uliye naye.

1. Jiulize ni kwa nini una wivu
Sababu ya wewe kuwa na wivu inaweza kutokana na kitu kilichowahi kukupata hapo nyuma. Inawezekana uliwahi kuwa na uhusiano ukavunjika sasa unaogopa na huo usivunjike kwa kuchukulia poa kila unachokiona kwa mpenzi wako. Hiyo inaweza kukusababisha ukawa na wivu.

Mara nyingi kama mtu aliwahi kuwa na mpenzi ambaye alikuwa akimsaliti huharibu ubongo wake na kukaa na wasiwasi wakati wote kwa mpenzi anayeingia naye tena katika uhusiano.

Cha kufanya hapa ni kujitambua kwanza kisha ujifunze jinsi ya kukabiliana na wivu ulionao.

Kuna watu wengi ambao wana wivu lakini utawajua kwa matendo tu hasa wanapokuwa na wapenzi wao.

2. Usimhisi mpenzi wako
Kama utakaa chini na kuhisi kuwa mpenzi wako ana jambo analifanya nyuma ya pazia, utakuwa umepungukiwa na uaminifu.

Je, kuna kitu kibaya aliwahi kukufanyia kikakufanya ukose uaminifu kwake?
Kama ubongo wako uko sawa hauwezi kukufanya wewe ukawa na wasiwasi wakati wote.

3. Muulize maswali unapojisikia
Ni sahihi kumuuliza maswali mpenzi wako ili mradi uhakikishe hayatamtibua na kusababisha ugomvi. 

Hii itasaidia kuwaunganisha lakini jaribu kuuliza katika hali ya upole na ikiwezekana kwa lugha ya kimahaba. 

Kama utakuwa na wasiwasi jaribu kumuuliza maswali machache ambayo una wasiwasi nayo.
Usiwe ni mtu wa kupaniki wakati wote.

4. Usifananishe kila kitu 
Hupaswi kufananisha kila kilichotokea kwako au kwa mtu mwingine, wala usifananishe jambo alilolifanya mpenzi wako wa sasa na kile alichokufanyia yule wa zamani.

Kila mtu ana hulka zake na tofauti yake. Usiruhusu kuwa na woga kwamba patina wako anaweza kupata mtu mwingine wa kukuzidi wewe wala usifananishe kipato na muonekano wa mtu mwingine unayehisi anaweza kumchukua mpenzi wako. 

Ukithubutu kuruhusu hali hiyo, huwezi kukabiliana na wivu.
Kumbuka kuwa dunia imeumbwa na watu tofauti tofauti kama tutaishi kwa hisia kuwa fulani ana kipato anaweza kumchukua mpenzi wangu, basi dunia itakuwa si sehemu ya kuishi.

5. Wasiliana naye mara kwa mara 
Mawasiliano ni njia nzuri ya kuukabili wivu. Tumia muda mwingi kujadiliana na mpenzi wako ni kwa nini una wivu wa kupindukia. Kwa kufanya hivi unaweza kupunguza uzito wa tatizo la wivu.

Watu wengi wamefanikiwa kuficha wivu wao kwa kutumia njia hii na kama hutamweleza mpenzi wako jinsi unavyohisi wivu hatoweza kukusaidia.

Wengi wao hushindwa kuvumilia pale wanapowaona wapenzi wao wamekaa na mtu wa jinsi nyingine mapozi tata lakini kama utamueleza ni rahisi kukusaidia kwa kujirekebisha au kukufanya uzoee.

Ongea na mpenzi wako sana, gombana naye kidogo, hali hii itakwisha taratibu.

6. Kuwa na ujasiri/ jiamini
Wivu unaweza kuongezeka kama utakuwa hujiamini. Unahisi hujiamini? Unahisi mpenzi wako anaweza kukuacha? Kama maswali yote hayo yako kichwani kwako, unatakiwa kuyajibu na kuyafanyia kazi.

Kama mpenzi wako atakuwa ni mtu wa kujichanganya na watu mbalimbali hii haimaanishi kuwa atakuacha au hakupendi, jiamini na ujipe moyo wewe ndiyo chaguo lake.

Kumbuka kuwa kuna sababu ya yeye kukuchagua wewe na kuwaacha hao waliomzunguka.

7.Chukulia wivu ni adui yako
Ni sawa bila wivu kabisa uhusiano wenu utakuwa na matatizo lakini ukiona sasa unavuka mipaka ni vyema ukauchukulia kama adui wa penzi lenu.

Mpenzi wako atakasirika kuona unamuonea wivu hata katika yale usiyostahili kumuonea wivu, ataona unamboa na kuhisi huenda siyo mtu sahihi kwake. Uko tayari mpenzi wako ajisikie hivyo? 

Kama hauko tayari basi wakati mwingine uchukie wivu, uchukulie ni adui anayeweza kukufanya ukamkosa huyo mpenzi wako uliyempenda. Ukifanya hivyo taratibu utapunguza na kuwa na wivu wa wastani unaoweza kuliboresha penzi lenu.

8. Jenga uaminifu kwake
Ni kweli wivu kwa namna moja ama nyingine kunaufanya uhusiano wako uwe imara lakini sasa unaweza kuuimarisha uhusiano wako kwa kujijengea mazingira ya kumuamini mpenzi wako.

Endapo utajenga mazingira hayo ya kumuanimi utashangaa hata kiwango cha kumuonea wivu kiasi cha kumfanya kuona ni kero kinapungua.

Amini kwamba hata akiwa mbali na wewe hawezi kufanya kitu tofauti kinachoweza kukukwaza. Na kama utashindwa kumuamini mpenzi wako basi unatakiwa kujiuliza kwa nini kwani lazima kutakuwa na tatizo. 

9. Mpe nafasi ya kujiachia
Unapoingia kwenye uhusiano, wewe umekua na hata huyo mpenzi wako atakuwa ni mtu mzima. Itakuwa ni jambo la ajabu endapo utamzuia kujichanganya na wenzake kwa kuhisi anaweza kukuzunguka.

Kama umempenda basi huna haja ya kutumia nguvu nyingi kumchunga kwani  kumchunga kwako kunaweza kumkera na kuhisi hayuko na mtu sahihi licha ya kwamba yawezekana unafanya hivyo kwa nia njema. Mpe uhuru wa kujichanganya.

10. Jifunze kutoka kwa wengine
Wakati mwingine yaweza kuwa rahisi kwako kujua kwamba unachokifanya ni sahihi au siyo sahihi kwa kuwaangalia wapenzi wengine. Je, wao wanaonesha wivu wao waziwazi au umeshawahi kumsikia mmoja wao akilalamika kukerwa na namna mwenzake anavyomuonea wivu mpaka inakuwa kero?

Kama hujawahi kwa nini usione kwamba una kila sababu ya ‘kuikontroo’ tabia yako ya kuwa na wivu kupindukia. Wivu sawa, lakini kupitiliza ndiko kusikotakiwa na endapo hutakuwa mwepesi wa kubadilika penzi lako linaweza kunyauka hivi hivi ukiwa unaliona.

Njia 31 ambazo zitamfanya msichana akupende zaidi na kufurahi


1. Mwambie yeye ni mzuri na sio uko sexy au hot 

2. Mshike mkono wake kwa kuwa unampenda na sio unazingua 

3. Mtumie sms nzuri ya kumwamsha asubuhi 

4. Cheza nae michezo mingi na mfanye ashinde yeye 

5. Mkumbatie mara kwa mara mgongoni kwa kumshtukiza 

6. Usijirushe na x wako wakati yeye hayupo hayo sio mapenzi 

7. Kama unaongea na binti mwingine mkiwa pamoja ukimaliza maongezi rudi na kumkisi mpenzi 

8. Mtumie sms au kumpigia simu na kumwambia unampenda 

9. Mtambulishe kwa marafiki na kuwaambia kuwa ni mpenzi wako 

10. Penda kuzichezea nywele zake na kuzisifia 

11. Jaribu kutoka nae hata kama atakataa 

12. Onyesha kuumia ukigundua watu wanammezea mate 

13. Mchekeshe kila mara kumfanya atabasamu 

14. Mfanye alale mikononi/mapajani mwako akijisikia kulala 

15. Kama amekuudhi wewe mkiss na kutomjibu vibaya 

16. Onyesha hisia zako kwake 

17. Kila mwanamke anahitaji zawadi tatu kutoka kwa mwanamme:(pafyumu,viwalo na mekapu seti) 

18. Mjali kama unavyowajali marafiki zako 

19. Mwangalie machoni mwake na onyesha kuvutiwa nae 

20. Tumia muda mwingi weekend kuwa nae kwakuwa unampenda 

21. Mkiss mvua ikiwa inanyesha bila kuwa na mwamvuli 

22. Mkiss kuonyesha wampenda 

23. Kama unasikiliza mziki mpe headphone ya pili nae asikilize 

24. Ikumbuke birthday yake na kumpa zawadi hii inamaana kubwa kwake 

25. Kila mara akikukosea jaribu kuonyesha haujaumia na unazidi kumpenda 

26. Kila mara mpigie simu na kumwambia huta uumiza moyo wake na unamjali na unapenda kuisikia sauti yake 

27. Mpe kila hitaji muhimu alitakalo 

28. Onyesha kujali vitu vidogo afanyavyo kwani itampa imani zaidi 

29. Usiwakumbatie mabinti wengine ukiwa nae 

30. Ukiwa na muda jaribu kuwa nae jirani atakujali kwa hilo 

31. Kama unamjali usimwambie ila onyesha kwa vitendo

MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!

 
Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo. 
Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza. 


1) Kuweka misingi ya kifamilia: 
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
– Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa 
2)Kujitegemea kiuchumi: 
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector. 
3) Kuwa na kitega uchumi: 
Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA. 
4) Makazi: 
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba. 
5)Uwe na professional qualification 
: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care! 
6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea: 
Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama “roba ya mbao” till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa. 
7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea: 
Kama we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe. 
8) Uwe na busara. 
Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.! 
9) Savings: 
Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale. 
10) Umjue Mungu: 
Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni masikini). 

NIKWANINI WANAUME HUCHEAT/KUWA NA MWANAMKE MWINGINE LAKINI HAWAKAMATWI

Wao hawatumii simu kuwasiliana

Msingi mkubwa wa wanaume wa aina hii wanatunza siri kuhusu wao wenyewe na familia zao, kazi zao hata majina yao wakati mwingine
HAWATUMII SABABU YA KUWA KAZINI
Mara nyingi mtu anaye cheat hutumia style moja ya kuwa kazi zinamfanya kuwa busy kumbe anatumia muda na hawala yake, hivyo basi wadanganyifu wa kiwango cha juu hawatumii sababu ya kuwa kazini kwani wanajua akianza kushtukiwa jambo la kwanza ni kuangalia muda anaotumia kazini.
HUHAKIKISHA MKE ANA FURAHA MARA ZOTE
Kwa kuwa atafanya kila njia kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha, hii ina maana kwamba mwanamke mwenyewe atajisahau na kujiona kuna amani kumbe ndani yake kuna udanganyifu mkubwa. Anaweza kukupa zawadi kila mara hasa akisafiri, anafanya kila kitu kuonesha anakujali kumbe anakuzunguka na inakuwa ngumu sana mwanamke kujua kwa sababu kila kitu anachohitaji anapata.
HAWATUMII SIMU
Wanaume wa aina hii si kawaida yao kuwapa mawahala namba za simu za mkononi, nyumbani au kazini. Wanajua kupitia simu za mkononi text message tu inaweza kuharibu mambo, acha kupigiwa simu kabisa. Pia wanajua wanawake ni rahisi sana likitokea jambo lolote ambalo hajaridhika au kukorofishana mara nyingi hupiga simu kwa wake wa hawa wanaume ili kuvuruga zaidi. Ndiyo maana hawatumii simu.
WANALIPA CASH BILA RISITI
Kawaida hawatumii credit card kulipia huduma zao kwani kuna bank huonesha matumizi ya pesa yako kwenye bank statement (hasa nchi zilizoendelea). Wanaogopa kwani kwenye account kunaweza kuonesha hotel na sehemu alienda na jinsi alivyotumia pesa.
Pia hawataki risiti kwani anaweza kujisahau akiwa nyumbani risiti ikakutwa kwenye mfuko wa suruali au wallet.
WANABANA MATUMIZI
Kawaida cheater mzuri hakopi pesa kwa ajili ya kustarehe na huyo mwanamke na pia anahakikisha matumizi yana balance na kuwa kama kawaida, hawana mambo ya ku-impress mwanamke kwa kutumia fedha nyingi hadi kukopa kwani wanajua matatizo ya kifedha yakitokea lazima atiliwe mashaka na kushikwa so mambo ya pesa wapo makini sana.
HAWADANGANYI OVYO
Hawana tabia ya kudanganya sana na mara kwa mara, kwani wanajua ipo siku data zitagoma bali wao huelezea uwongo unaofanana sana na ukweli ambao anayeambiwa anadhani ni ukweli kumbe ndani kuna uwongo.
Pia hawezi kueleza kitu hadi aulizwe pia anakuwa na majibu mafupi yasiyo na maelezo mengi ili kuficha data zaidi.
HAWATUMII MARAFIKI
Kawaida hawatumii marafiki au marafiki kuwasaidia kuficha siri zao. Wanajua marafiki kwa kuchemka au kwa makusudi wanaweza kufikisha habari kwa familia. Hujitunzia siri wao wenyewe na yeye tu ndo anajua kila kitu. Hata mwanamke ataambiwa asimwambie mtu na akimwambia mtu urafiki unakufa kwani anajua jinsi watu wengi wanavyojua issue basi uwezekano wa habari kuzunguka ni mkubwa.
WANAENDA MBALI
Kawaida cheaters wa aina hii si kawaida yao kutembea na majirani, marafiki, wasichana wa kazi au wafanyakazi wenzao au mtu yeyote ambaye yupo connected na mke wake, wao huenda mbali kabisa ambako hakuna mtu anawajua. Wanatumia ile principle kwamba ukiona mwizi anaimba jirani ndo kukamatwa kumekaribia, hivyo hawathubutu kuwa na wanawake wa karibu ambao jamii anaishi wanamfahamu.
KUMBUKA
Kuwa mwaminifu katika ndoa yako ndiyo jambo la misingi na muhimu si maisha yako tu bali hata familia, ukoo wako na jamii nzima.
Kumbuka kila mwizi ana siku yake ya arobaini hivyo basi hata kama hujagundulika ni vizuri kuacha hiyo tabia mapema ili uanze kujenga familia bora na yenye mafanikio pasipo wewe mwenyewe kuishi ndani ya guilt

MUHIMU:TAMBUA UTAMU WA MAPENZI NA JINSI YA KUULINDA KATIKA MAHUSIANO.

Kuna sababu za msingi kabisa kuelezea mambo ya kuzingatia ili kutambua vitu vitakavyokufanya ufurahie utamu wa ndoa yako. Kuishi na mke au mume sii kitu rahisi kama ambavyo watu wengi ambao hawako katika ndoa hufikiria. Hivi ni vipengere baadhi tu, wanandoa na wampenzi wanapaswa kuvitambua;

Kwanza kabisa ni kwambie kwamba utamu wa mapenzi sii lazima ufanye tendo la ndoa ama ngono, kuna mambo kibao ambayo moyo wa binadamu ukiyakosa huweza kukonda kama muathirika wa magonjwa hatari ya mwili. #"Upendo kutoka kwa yule umpendae", hili ndilo jambo kubwa la kwanza katika afya ya moyo ulio katika dimbwi la mapenzi.

Hakuna kitu kitamu kama kupendwa na ukapenda pia, kitendo hiki hufunga macho yote ya vishawishi vya dunia hii ya kidigitali. Usilazimishe upendo kwa mtu ambae unaonekana kuwa wewe tu ndiye unaye mjali wakati yeye hana habari na wewe. Ndio maana ukitaka kuingia katika ndoa lazima umtafute mtu unayempenda na anayekupenda ili muishi katika maisha yasiyo ya kushawishika kufuata matamanio mengine nje ya ndoa.

Kitu cha pili katika kufurahia utamu wa penzi ni #"amani" watu wengi wana wanaume na wanawake warembo, lakini hawafurahii mapenzi kwasababu hawana amani ndani ya nyumba. Utafurahia utamu wa mahusiano ya ndoa endapo utakuwa na moyo uliopondeka mbele za Mwenyezi Mungu, yani kuvumiliana katika changamoto za maisha.

Wapo watu wao ni maarufu kwa kuharibu mahusiano ya watu "tofauti na ndugu yako wa karibu" hakuna mtu anayefurahia kukuona unamwanamke mrembo ndani ya nyumba au mwanaume mtanashati ndani ya nyumba, na kwambia hili, jifunze kutunza siri za uzuri wa mkeo au mmeo. Kunawatu wanavitaka vitu hivi sana hata kwa gharama yoyote ile na popote vitakapopatikana vitanakuwa halali yao.

Kama mpenzi wako anakupa penzi tamu na la kistaarabu, basi haina haja ya kumueleza rafiki yako maana hujui yeye anakosa nini katika mahusiano yake na mwenzi wake. Pesa ni silaha kubwa sana katika mapenzi haya ya kizazi cha digitali, pesa zimekuwa na ushawishi mkubwa sana katika mapenzi hivyo unapaswa kuwa msiri katika mambo yako ya chumbani.

Cha msingi zaidi, hakuna mtu anayefurahi kusalitiwa katika mapenzi, kila mtu anatamani kummiriki mwenzi wake asipate wazo la kutoka nje ya mahusiano. Tunajua kabisa dunia hii kila siku tunakutana na wasichana warembo kabisa na pia tunakutana na wanaume watanashati sii kidogo, lakini kitu cha msingi ni kuyashinda macho na kuamini #"UKIONA VYAELEA UJUE............?